mwanaharakati7
Member
- Apr 22, 2011
- 7
- 3
Mimi ni MTANZANIA niliyefanikiwa kujiunga na chuo kikuu cha dodoma (udom) mwaka juzi kwa bahati nzuri nimefanikiwa kupata mkopo 100% ni kweli fedha imeongezeka lakini haitakuwa vizuri mimi niongezewe na wengine wakose kabisa haikuwa dhamira yetu.Sisi ndiyo tumesababisha wadogo zetu wa mwaka wa kwanza kukosa kabisa mikopo wakati serikali yetu inafedha nyingi tu za kutusomesha wote,sasa tuamueni moja tuwasaidie wadogo zetu ili nao waweze kupata elimu,ebu fikiria zaidi ya wanafunzi 1000 wamekosa mikopo wengine tunaosoma nao wanarudi nyumbani kwa sababu hawana fedha za kujikimu..Tuacheni unafiki, kuna watu hawana mikopo jaman isiwe kigezo cha kuongezewa sisi hela ndio inatuvunja nguvu ya kudai haki za wengine,isije ikathibitisha kauli kuwa "mwenye nacho anaongezewa asiye nacho anajimwa"kwel hata ALAH anakataa.Tusije tukaonekana ni WANAFIKI mbele ya jamii na ahera pia kisa tumeongezewa bumu kumbukeni hata wao wanatutega kwa hili.SASA tuungane vyuo vyote TANZANIA kupinga hili swala kwa sababu kila chuo kuna watu hawakupata mikopo,UDSM wameanza,tuungane jamani ili hata alah asituone wanafiki pia kuongezeka kwa bumu isiwe sababu ya kutowasaidia wenzetu.SISI NDIO VIONGOZI WA NCHI YETU.Nasisitiza kuanzia jumatatu tarehe 15/11/2011 vyuo vyote TANZANIA tuungane kupinga hili swala kwa kutoingia darasani.Kila mtu anaongozwa na nafsi yake pamoja na mungu mmoja.