Habari: Naomba msaada, nina Project Proposal ila sina sehemu ya Kuiwasilisha

anonymousafrica

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2016
Posts
611
Reaction score
640
Habari mwana au wana JF, baada ya masomo yangu shahada ya kwanza ya mawasiliano ya umma na uandishi wa habari nimeweza kutoka na utaalam fulani wa kuandika proposals mbalimbali.

Hapa karibuni nimeandika proposal itakayoweza kunisaidia kuanzisha jarida la wanawake. Jarida lenye mambo mengi siwezi elezea yote lakini dhumuni kubwa ni kuandika taarifa za wanawake mbalimbali ambao ni wawajibikaji.

Hii itasaidia kuamsha wanawake wengine ambao wamekatazwa.hawaoni njia au wanaona hawastahili kufanya shughuli zozote za uzalishaji. Wanafunzi, wanawake kwenye taasisi na waliojiajiri pia.

Project yangu imeisha (kimaandishi) mpaka ''budget'' ipo vizuri lakini sina sehem ya kuiwasilisha kwakua idea ya kufanya kitu ninayo ila uwezo wa kuanzisha na kusimamia peke yangu siwezi.

Uwezo wangu ni kurecord na kukusanya datakudesign jarida na kupangilia masuala yotekiufupi utekelezaji kwangu sio shida. Shida ni gharama .

Ahsante naomba msaada wako
 
hamachiachamwashambwa@gmail.com tuma humo hiyo proposal
 
Kuwa makini,watakuja wakujidai wanataka kukusaidia na baadae wataiba wazo lako na kukwambia halifai kisha watalifanyia kazi na kupiga pesa.
 
"kwakua idea ya kufanya kitu ninayo ila uwezo wa kuanzisha na kusimamia peke yangu siwezi"

"kiufupi utekelezaji kwangu sio shida... shida ni gharama tu"

Hapo kwenye hizo kauli mbili naona kama zinapishana labda utoe ufafanuzi kidogo
 
"kwakua idea ya kufanya kitu ninayo ila uwezo wa kuanzisha na kusimamia peke yangu siwezi"

"kiufupi utekelezaji kwangu sio shida... shida ni gharama tu"

Hapo kwenye hizo kauli mbili naona kama zinapishana labda utoe ufafanuzi kidogo
neno moja

HELA
 
"kwakua idea ya kufanya kitu ninayo ila uwezo wa kuanzisha na kusimamia peke yangu siwezi"

"kiufupi utekelezaji kwangu sio shida... shida ni gharama tu"

Hapo kwenye hizo kauli mbili naona kama zinapishana labda utoe ufafanuzi kidogo
kutekeleza namaanisha kutengeneza jarida katika mfumo wa document
 
Tuwasiliane nikupe sehemu za kupeleka.
 
Sikia TAFUTA NGOs yoyote ambayo inadeal na mambo ya empowerment kama Tamwa, tawla cjui afu waelekeze waoneshe hio project kama nzuri watainuanua au unaweza pata kazi kabisaa.
 
Sawa mimekuelewa Jitahidi uwe unaangalia Organisation ambazo zinatoa Finding kwa ajili ya projects mbalimbali utapata ambazo unakidhi vigezo unaaply.

Mfano hii wanatoa funding kwa ajili ya kuwajenga wanawake na wasichana na wanatoa kila mwezi kama unaweza kupitia kujua kama unakidhi vigezo vyao.

www.hervoicefund.org
 
Pia Zile Magazine huwa ni Pure Business na wengi huwa wanaendesha kupitia yale matangazo mule ndani na makala mbali mbali.
 
Pina Proposal huwa inakuwa na kila kitu hadi jinsi ya kuanza na unaanza anzaje project. So napata shida kwamba una Proposal ila umeshindwa kuanza na kama sikosei hata pesa unadai unazo.

Je Proposal imekaaje hadi haina kipengele cha kuanza Project.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…