Habari ndio hiyo au mnasemaje

DR HAYA LAND

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2017
Posts
23,928
Reaction score
63,499
..Hiyo Internet ya Ofisini unavyoikomoa, umefungua blogs zote kwa mpigo, YouTube, Skype, Twitter, Facebook na Unadownload Videos! Wakati boss wako siku nzima amefungua emails tu.
Basi ndio hivyo hivyo housegirl/Houseboy wako ulomuacha home naye kashika Remote zote za DSTV, Deki, TV na StarTimes, Kawasha feni kaisogelea, nje kuna taa zinawaka, anampasia nguo Boifrendi wake muuza mkaa, anakunywa maji yako ya Kilimanjaro afu anarudishia ya bombani, maziwa anatumia anaongeza maji, na kama hujafunga chumba chako, ujue sasa hivi amejilaza kwenye kitanda chako na anajaribisha nguo zako.
Yes we si una fujo za mjini uko online, sasa na wenzio wana fujo za kijijini off-line home kwako. Ngoma Droo...
 
ndo nini sasa ?
kama hauna hausgeli inakuwaje ??
 
havina uhusiano , unaweza ukawa cmpo tu at ur ofc lakn hous girl akafanya madudu uko hm
 
Havina uhusiano wowote,

Sasa "house girl" kushika remote za hivyo ving'amuzi kuna ubaya gani?

Sasa si tulilipia ili vitumike!

Acheni tabia za kimaskini na dhana mbaya kwa mahouse girl.

Nyie ndio mnaokaa na mikate kwenye fridge mpaka inaoza.
 
Teknolojia hua haidanganyi...
Ofisini unawekewa programs za Ku monitor internet n.k kama Wireshark
Boss anakua anakuchora tu,na ukikutana na bosi ana akili kama zangu naiba na password zako.

Home nafunga tu CCTV cameras au kamera za siri kabisa..
Nikijua unapenda kudokoa nini si nakuwekea dawa ya kuharisha ktk icho kitu.
 
Bora hausi geli achezee vyote hivyo
Hausi geli wengine huchukua miswaki yenu na kusugulia vyoo[emoji3]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…