Habari Njema Katika Vita Dhidi Ya VVU/UKIMWI

md4doctor2000

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2012
Posts
736
Reaction score
315
Kuna uwezekano kuwa janga la ukimwi huenda likadhibitiwa ifikapo mwaka 2030, kulingana na ripoti iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ukimwi.

Ripoti hiyo imesema kuwa idadi ya visa vya maambukizi mapya na vifo kutokana na HIV, vimeendelea kushuka.

Hata hivyo, shirika hilo linataka juhudi zaidi za kimataifa kufanywa kwani za sasa hazitoshi

Na shirika la misaada la Medecins Sans Frontieres limeonya kuwa watu wanaoishi na virusi hivyo hawapati dawa za kutosha.

Kwa mujibu wa shirika hilo watu milioni 35 wanaishi na virusi vya HIV.

Ripoti hiyo ilionyesha visa vipya vya maambukizi milioni 2.1 vilitokea mwaka 2013. Idadi hii iko chini kwa asilimia 38 ikilinganishwa na mwaka 2001.

Vifo kutokana na HIV pia vimepungua kwa asilimia 5 katika miaka mitatu iliyopita. Kwa sasa watu milioni 1.5 hufariki kutokana na ugonjwa huo kila mwaka.

Afrika Kusini na Ethiopia zimepiga hatua katika kupunguza vifo vya wagonjwa wa HIV.


Source: Habari njema katika vita dhidi ya HIV - BBC Swahili - Habari


Sent from Samsung Galaxy Note 3
 
Nilidhani dawa imepatikana ili nizitupilie mbali hizi Rough riders..

Kumbe ni mpaka 2030...🙁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…