Habari njema kwa vijana Tanzania

Habari njema kwa vijana Tanzania

kitongoroso

Member
Joined
Nov 3, 2013
Posts
29
Reaction score
4
Tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana nchini linaweza kupunguzwa kwa kiasi kikubwa kwa ujio wa mikopo yenye riba nafuu nchini. Mikopo hiyo ambayo itaanza kutolewa rasmi kwa awamu ya kwanza mwezi wa 12 mwaka huu itakuwa na masharti nafuu sana ikilinganishwa na aina nyingine za mikopo ambayo ilishawahi kutolewa nchini.

Akizungumza hayo mjini Arusha afisa mikopo hiyo kutoka Tanzanian Small and Medium Enterprises ndugu Victor Tesha alibainisha baadhi ya sifa hizo kuwa ni:-

1. Riba kwa mikopo hiyo itakuwa ni asilimia 3 tu
2. Wakopaji watakopeshwa vifaa vya uzalishaji tofauti na mikopo mingine ambayo hupewa fadha cash.

Aidha hii itakuwa ni fursa nyingine kwa vijana wajasiriamali kuimarisha mitaji yao kwa aina hii ya mkopo kwa kubuni miradi na kupatiwa vifaa kwa ajili ya miradi yao. Ndugu Tesha pia alifafanua kuwa pamoja na kupatiwa mikopo hiyo kutakuwepo na close monitoring ya miradi yenyewe ikiwa ni pamoja na vijana hao kupatiwa ushauri elekezi ya namna ya kuimarisha miradi yao ili waweze kurejesha mikopo hiyo kwa wakati.

Masharti mengine ya mkopo huu ni kuwa ni kwamba kwa vijana ambao hawana mradi wowote ambao upo tayari kwa ajili ya kuuendeleza wanaweza kupata mkopo huo endapo tu wataunda vikundi vya watu kumi vinavyotambuliwa kisheria na kupatiwa vifaa vya kuanzisha mradi walioukusudiwa.

Kama vijana watatumia fursa hii vizuri tatizo la ukosefu wa ajira unaweza kupunguzwa na vijana wakajenga uwezo kiuchumi nchini. Vijana Itumieni fursa hii. Unaweza kuipata habari hii kwenye gazeti la the guardian la jana.



attachment.php

Ndugu victor Tesha Afisa mikopo
 

Attachments

  • jf ts.jpg
    jf ts.jpg
    40.8 KB · Views: 581
  • jf.jpg
    jf.jpg
    204.8 KB · Views: 177
  • tes jf.jpg
    tes jf.jpg
    72.2 KB · Views: 180
kaka mgeni hapa bongo hizi eee... zinaweza kuwa propaganda, kama ni mpango ilishafanyika zaman sana alafu bado tuko vile vile

teacher wang aliniambia, kijana if you want to succesed you have to be your own as your own lfy, as your desission, as your own strategic. huyo tesha awez leta mabadiliko kwa vijana
 
Few issues from me;

1. Hela unayokopeshwa kwa 3% imetoka wapi? ni ya serikali? ni ruzuku? ni msaada? au ni kutakatisha hela kiaina?
2. Hiyo taasisi inatoa mizizi yake wapi? ni kampuni? who are the owners? where is the company/entity/institute profile?

Ni vizuri kuona kuwa kuna mipango kwa ajili ya ajira kwa vijana. Lakini tunahitaji kujua sustainability ya hii mipango ikoje ili tuone itatusaidia kwa kiasi gani
 
hata mm sikumuelewa mkuuu huyu hiyo riba ya 3% imetoka wapi ilihali vijana wenyewe hawana hata kamtaji ka kuanzisha mradi

na kwanini hiyo riba inakuwakubwa utadhani riba ya mabenki?

mm nimeshangaa sana tena sana kijana wa kitz hamka usiyumbishwe na wengine ambao wanataka kuchumia ktka migongo ya vijana kisa kutokuwa na ajira ni bora mtu kujipanga na kupigania wewe mwenyewe mpaka kinaeleweka
Few issues from me;

1. Hela unayokopeshwa kwa 3% imetoka wapi? ni ya serikali? ni ruzuku? ni msaada? au ni kutakatisha hela kiaina?
2. Hiyo taasisi inatoa mizizi yake wapi? ni kampuni? who are the owners? where is the company/entity/institute profile?

Ni vizuri kuona kuwa kuna mipango kwa ajili ya ajira kwa vijana. Lakini tunahitaji kujua sustainability ya hii mipango ikoje ili tuone itatusaidia kwa kiasi gani
 
mikopo mingi ni kupeana umasikini na sio kupunguza umasikini maana mtu unakopa na unakuja kuwa mtumwa wa kurudisha deni ulilonalo na sio kuendeleza mradi ulioanzisha!!!
 
Back
Top Bottom