kitongoroso
Member
- Nov 3, 2013
- 29
- 4
Tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana nchini linaweza kupunguzwa kwa kiasi kikubwa kwa ujio wa mikopo yenye riba nafuu nchini. Mikopo hiyo ambayo itaanza kutolewa rasmi kwa awamu ya kwanza mwezi wa 12 mwaka huu itakuwa na masharti nafuu sana ikilinganishwa na aina nyingine za mikopo ambayo ilishawahi kutolewa nchini.
Akizungumza hayo mjini Arusha afisa mikopo hiyo kutoka Tanzanian Small and Medium Enterprises ndugu Victor Tesha alibainisha baadhi ya sifa hizo kuwa ni:-
1. Riba kwa mikopo hiyo itakuwa ni asilimia 3 tu
2. Wakopaji watakopeshwa vifaa vya uzalishaji tofauti na mikopo mingine ambayo hupewa fadha cash.
Aidha hii itakuwa ni fursa nyingine kwa vijana wajasiriamali kuimarisha mitaji yao kwa aina hii ya mkopo kwa kubuni miradi na kupatiwa vifaa kwa ajili ya miradi yao. Ndugu Tesha pia alifafanua kuwa pamoja na kupatiwa mikopo hiyo kutakuwepo na close monitoring ya miradi yenyewe ikiwa ni pamoja na vijana hao kupatiwa ushauri elekezi ya namna ya kuimarisha miradi yao ili waweze kurejesha mikopo hiyo kwa wakati.
Masharti mengine ya mkopo huu ni kuwa ni kwamba kwa vijana ambao hawana mradi wowote ambao upo tayari kwa ajili ya kuuendeleza wanaweza kupata mkopo huo endapo tu wataunda vikundi vya watu kumi vinavyotambuliwa kisheria na kupatiwa vifaa vya kuanzisha mradi walioukusudiwa.
Kama vijana watatumia fursa hii vizuri tatizo la ukosefu wa ajira unaweza kupunguzwa na vijana wakajenga uwezo kiuchumi nchini. Vijana Itumieni fursa hii. Unaweza kuipata habari hii kwenye gazeti la the guardian la jana.
Ndugu victor Tesha Afisa mikopo