Dr. Chapa Kiuno
JF-Expert Member
- Sep 11, 2009
- 443
- 18
</SPAN>
Maumivu ya tumbo wanayopata wanawake wakati wa kipindi cha hedhi wamepatiwa dawa
Friday, October 09, 2009 8:07 AM
Habari njema kwa wanawake, wanasayansi nchini Uingereza wamegundua dawa ya vidonge ambayo inazuia maumivu ya tumbo wanayopata wanawake wanapokuwa kwenye hedhi.
Kipindi cha hedhi huwa ni kigumu sana kwa wanawake wengi duniani kutokana na maumivu makali ya tumbo wanayopata wakati wanapokuwa kwenye siku zao.
Wanasayansi nchini Uingereza wamegundua dawa za vidonge ambazo zitazuia maumivu hayo na hivyo kuwafanya wanawake waendelee na maisha yao ya kawaida bila maumivu yoyote.
"Maumivu ya tumbo wakati wa hedhi yanayojulikana kitaalamu kama Dysmenorrhoea huwaathiri wanawake wengi duniani na hadi sasa kulikuwa hakuna tiba au njia ya kuyaondoa maumivu hayo", alisema Dr Jim Phillips toka kampuni ya Vantia Therapeutics iliyoko mji wa Southampton ambayo ndiyo iliyogundua dawa hiyo.
"Tunaweza kusema kuwa huu ni ugunduzi mpya wa kwanza kwani hakuna tiba nyingine yoyote zaidi ya hii", alisema.
Dawa hizo za vidonge zilizopewa jina la VA111913, zimefanyiwa majaribio na zimeonyesha mafanikio makubwa sana na zimethibitishwa kuwa ni salama.
Dawa hizo zitaingia madukani baada ya miaka minne.
Zitafanyiwa majaribio tena na wanawake 128 wa nchini Uingereza na Marekani wenye umri kati ya miaka 18 na 35.
Wanawake watakaojitolea kujaribu dawa hizo ni wale wanaosumbuliwa na maumivu makali sana ya tumbo kutokana na hedhi kiasi cha kwamba hushindwa kuendelea na maisha yao ya kawaida. Wanawake hao watapewa dozi ya dawa hizo wakati wa kipindi cha hedhi zao.
Dawa hiyo hufanya kazi kwa kuifanya homoni ya vasopressin, ambayo huifanya misuli ya ukuta wa uterus kusinyaa wakati wa hedhi iwe katika hali yake ya kawaida na hivyo kumuepusha mwanamke na maumivu hayo.
Takwimu zinaonyesha kwamba maumivu ya tumbo wakati wa hedhi huwaathiri asilimia 80 ya wanawake duniani katika baadhi ya vipindi vya maisha yao.
Wanawake wengi hujaribu kupunguza maumivu hayo kwa kufanya mazoezi ya kulainisha misuli ya tumbo, wengine hujikanda tumbo wakati wengine hushindwa kuvimilia maumivu hayo na hutumia dawa za kupunguza maumivu kama vile paracetamol, aspirin na nyinginezo.
Source: Daily Mail