Habari njema kwa wenye magonjwa sugu

D Metakelfin

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2017
Posts
3,399
Reaction score
3,666
Wanasayansi nchini Marekani wamefanikiwa kupambana na maradhi yaliyokuwa sugu kwa dawa za kupambana na vijidudu yaani antibiotics tatizo ambalo lilikuwa tishio dhidi ya sekta ya afya duniani.

Watafiti wameiboresha dawa ya sasa, Vancomycin kwa kutengeneza aina nyingine ya dawa
Vancomycin ilikuwa ikipoteza uwezo wake wa kupambana na bacteria aitwae enterococci ambaye husabisha madhara kwenye njia ya haja ndogo na vidonda.

Aina mpya ya dawa hii ina nguvu mara elfu moja zaidi na hushambulia vijidudu kwa njia tatu tofauti, kiasi cha vijidudu kushindwa kupambana na dawa hiyo.


Inakadiriwa kuwa vijidudu vilivyokuwa vikipambana na dawa za antibiotics husababisha vifo takriban elfu hamsini kila mwaka nchini Marekani na barani Ulaya.

source:BBC
 
cure for cancer ndio inasubiriwa.....!
 
Taarifa haijakamilika, au tuwekee chanzo tufuatilie wenyewe.
 
Big up kwa hao wanasayansi wa kimataifa, sasa cjui dawa hiyo itatufikia lini huku kwetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…