habari waungwana

habari waungwana

Mbunge wa CCM

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2009
Posts
475
Reaction score
25
habari waungwana.
leo nimejiunga rasmi uwanjani hapa JF. ni matarajio yangu kuwa tutaendelea kuwasiliana na ndugu wote na kubadilishana mawazo na michango mbalimbali kwa maendeleo yetu kama binadamu na nchi/taifa letu kama mahali ambapo Mungu alipenda tuishi sisi na vizazi vyetu.

kama lilivyo jina langu, ndivyo ilivyo dhamira yangu pia. niko katika matayarisho ya kugombea ubunge katika uchaguzi mkuu ujao. sina shaka kuwa wana JF watanisaidia kwa namna moja au nyingine ktk kufikia azma yangu hii kupitia mchango yao ya mawazo, ushauri nk.

nimekuwa nikitoa mawazo yangu siku za nyuma kupitia tovuti ya gazeti la Tanzania Daima, lakini cha kushangaza wahusika wameamua kufunga fursa ile bila hata kuwashirikisha wadau. nadhani yoyote mwenye kujua faida za kupashana habari hawezi kamwe kufikiri kupunguza fursa za habari na majadiliano.

nashukuru sana na natangaza rasmi kuwa sasa nimeingia JF

Mungu ibariki Tanzania
 
Kumbe wewe umejiunga hapa ili tukusaidie kufanya kampeni zako kaaaz kweli kweli
kwa hiyo unagombea kupitia chama Kipi???
 
Karibu jamvini, sera zako ni zipi, tuzijue mapema, same question as FL1 unagombea kupitia chama kipi?
 
karibu jamvini kama waugwana wanavyonena....ukweli na uwazi ndio dira humu
 
Back
Top Bottom