Habari za CHADEMA zazimika kama mshumaa Mitaani

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu watanzania,

Siasa Ni sayansi na ukikosea katika kanuni huwezi ukafanikiwa kupata jibu hata Kama utakesha usiku mzima unakokotoa, Baada ya kufunguliwa na kuruhusiwa kwa mikutano ya hadhara chadema waliingia majukwaani na mitaani kichwa kichwa, waliingia bila Sera Wala ajenda, waliingia na kupanda majukwaani bila hoja za kugusa maisha ya Watanzania.

Chadema waliingia na kukurupukia majukwaani kwa kuwekeza kwa watu binafsi badala ya ajenda na Sera za kugusa maisha ya watu, waliwekeza katika mapokezi ya viongozi wao kana kwamba ndio Mahitaji ya watanzania, hakuna walichozungumza kilichoteka hisia za Watanzania, Hakuna Sera waliyokuja nayo iliyo weka mijadala mitaani.

Sasa Chadema wamekataliwa mitaani na mioyoni mwa watanzania,wamepuuzwa na kukimbiwa na watanzania,wamebaki hawana pumzi tena, habari zao zimeyeyuka kama mshumaa,wamebaki watu wa kuunga unga na kuokoteza vihabari, wamebaki watu wa kupiga vipicha Kama watalii, wamebaki Ni watu waliokata Tamaa na kupoteza matumaini ya kisiasa, hawaamini kilichowatokea, hata mikutano imeshindikana Kuendelea na kufanyika maana walizoea ujanja ujanja na ubabaishaji kwa miaka mingi.

Hawaaminiki na yeyote, hawakubaliki na kundi lolote, hawasikilizwi kokote Wala hawaungwi mkono na yeyote mwenye Akili Timamu, Watanzania Walishapoteza Imani juu Yao,hawawaamini Tena, safu yao ya kiuongozi Hakuna mwenye kuiamini wala kuisikiliza wala kuiheshimu Wala kuwafuatilia mambo yao, ni chama kilicho bakia hewani kwa sasa maana hakina mizizi katika kundi lolote Wala uungwaji mkono kutoka kokote.

Huo ni mwanzo tu maana kipigo chenyewe Ni mwakani na mwaka kesho kutwa ambapo watakwenda kuvuna aibu ya Karne pale watakapokutana na kupambana na CCM hii iliyo imara na madhubuti kuwahi kutokea na inayokubalika na kila mtanzania na kila kundi ikiwepo viongozi wao, pona yao labda wakimbie uwanjani kwa visababu vya kuokoteza, mbali na hapo lazima chadema wakafundishwe kuwa siasa ni sayansi na CCM Ni chama kilichojaa wanasayansi wabobezi na nguli wa mikakati.

Kazi Iendeleee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627
 
Hata wewe ? unashabikia ujinga ?kweli Wajinga mnazidi kuongezeka
Huo ndio ukweli japo Ni mchungu lakini ndio uhalisia wenyewe kuwa kwa Sasa Chadema Imepoteza muelekeo na dira,Imepoteza ushawishi kwa watanzania,hakuna anayeiamini chadema kwa Sasa maana kila mtu anatambua kuwa Ni wababaishaji tu na wasaka tonge
 
Yaani umejishusha kiasi mpaka same level na kina Johnthepaptist... This is too low Bro!!
Duh...!. Kiukweli kabisa mimi sina level yoyote humu, nikipenda bandiko lolote kwa hoja yake, nachangia hoja bila kujali aliyepandisha bandiko ni nani!. Ninachoangalia mimi ni hoja tuu iliyo mezani bila kujali imeandikwa na nani!.
P
 
Duh...!. Kiukweli kabisa mimi sina level yoyote humu, nikipenda bandiko lolote kwa hoja yake, nachangia hoja bila kujali aliyepandisha bandiko ni nani!. Ninachoangalia mimi ni hoja tuu iliyo mezani bila kujali imeandikwa na nani!.
P
Sawa Mkuu, nimekusikia. Ila kuna hizi cheap Propaganda aka propaganda uchwara sometimes hakuna haja ya kuzishabikia. Zimechangia kushusja hadhi ya JF.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…