bee steve wnner
New Member
- Oct 29, 2017
- 2
- 0
MAPAMBANO ya serikali dhidi ya rushwa, yametajwa kuipaisha Tanzania mbele ya wafanyabiashara na wawekezaji wa nje wakiwamo wa Ujerumani, ambao baadhi wameonesha nia ya kuwekeza katika madini, nishati na viwanda vya dawa.
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Dk Abdallah Possi alisema hayo juzi mjini hapa katika mahojiano na wandishi wa habari wa nchini waliofika ubalozini, wakiongozana na washiriki wa Tanzania wa tamasha la Jubilee ya miaka 500 ya Mapinduzi ya Martin Luther katika Kanisa la Kikristo.
Akizungumzia mikakati ya ubalozi katika kuitangaza nchi kwa wawekezaji na watalii, alisema taswira nzuri ya Tanzania mbele ya mataifa ya nje, inafanya wawekezaji wengi wawe na uhakika wa kupeleka mitaji yao.
“Wapo wanaouliza maswali mengi tu na hata waliokuja nyumbani (Tanzania)... miongoni mwao wapo wenye interest (nia) na madini lakini sana sana na nishati. Wengi hapa ni wale wenye nishati ambayo ni rafiki kwa mazingira,” alisema Balozi Possi.
Balozi Possi ambaye pia anawakilisha Tanzania katika nchi za Uswisi, Austria, Poland, Czech, Slovakia, Romania na Hungary, alisema hivi karibuni alipokwenda katika jimbo la Hamburg, alikutana na wafanyabiashara walioonesha nia ya kwenda kuwekeza kwenye dawa.
“Walisema wanataka kwenda (kuja) Tanzania mwezi ujao ili wakajionee wenyewe ni maeneo gani wanaweza wakawekeza... taswira ya Tanzania kwa Ujerumani ni nzuri sana... naona raha,” alisema.
Akizungumzia mapambano dhidi ya rushwa yanayoongozwa na Rais John Magufuli yanavyoipaisha Tanzania na uhusiano wake katika uwekezaji, Dk Possi alisema Wajerumani ni watu ambao kwa tabia wanapenda uwazi na watu wasiopenda rushwa. Alisema bahati mbaya nchi za Afrika, kumekuwapo taswira mbaya ya kwamba viongozi wake wanakula rushwa na wanastarehe.
“Wanapoona serikali yoyote inachukua hatua kupambana na rushwa kwao inawapa confidence,” alisema. “Ujerumani ni nchi ambayo wanapenda kufuata utaratibu ...wanapoona mtu mwenye msimamo, ni kitu kizuri.
Hata ninapokuwa miongoni mwa mabalozi wenzangu kwenye hafla yoyote, huwa najiona vizuri nikiwa na bendera yangu,” alisema. Mikakati uwekezaji Akizungumzia mikakati ya ubalozi ya kuvuta wawekezaji, alisema wanafanya kazi kwa karibu na taasisi mbalimbali ikiwamo Taasisi ya Wafanyabiashara wa Kijerumani wenye nia na mipango ya kuwekeza Afrika (Africa Verein).
“Hata juzi juzi kulikuwa na kundi lilikwenda (Tanzania) na wengine watakwenda Novemba... Nilikwenda Hamburg, wameonesha nia kwenda kuwekeza kwenye dawa,” alisema.
Mkakati mwingine hususani kuhusu kuvutia watalii, alisema ni kufanya kazi na kampuni mbalimbali kuhakikisha kunakuwa na mawasiliano ya moja kwa moja nchini ili watalii wasipitie mawakala wa nchi nyingine hali ambayo hufanya safari ya mtalii kuwa ghali.
Alishauri hoteli za Tanzania bila kujali ngazi ya nyota, zihakikishe zinatumia teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama), kwa kuwa na tovuti zitakazorahisisha mawasiliano ikiwamo kupata taarifa zao na kufanya malipo ya huduma.
Mikakati ya ubalozi kuhusu kuvuta wawekezaji na utalii ni kutumia matamasha mbalimbali. Hata hivyo alisema mkakati huo haujapangwa sawa. “Ila tunaangalia namna gani kuwepo na ziara za mabalozi... nitapanga na watu wanaohusika na utalii kama vile kampuni binafsi au Tanapa kuona kama tunaweza kupeleka mabalozi wa nchi kadhaa waliopo hapa waende kuona Tanzania,” alisema.
Juzi alipokuwa akiapisha viongozi, Rais Magufuli alimuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Adolf Mkenda aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji akafanye mabadiliko katika wizara hiyo. Alisema anataka kila balozi baada ya kipindi fulani, aeleze ameleta kitu gani cha uwekezaji katika Tanzania.