Habari za Kifo cha Magufuli zilivyonifikia nikiwa Gerezani

Zanzibar umeitaja kinafikitu hapo, unautoto mwingi sazingine ndio mana wanakutulizaga.
 
Ukiishatambua kuwa pamoja na mengine yote, iwe ni madaraka, utajiri, au umaarufu wowote, bado wewe ni mwanadamu ambaye upo sawa na mwingine yeyote katika mwanzo na mwisho wako, hakika utaheshimu utu na ubinadamu wa mwenzako.

Kila mwanadamu, bila ya kuangalia alizaliwa mazingira duni au ya kifahari, wote tunazaliwa tukiwa sawa. Na mwisho wa maisha yetu, bila ya kujali mwingine mauti yanamkuti akiwa kwenye hospitali ya kifahari, na mwingine kwenye zahanati, lakini wote mnafanana katika maana moja kuwa miili yenu haina hisia tena, wala hamjimudu.

Kiuhalisia, kufanana kwetu wanadamu kupo katika mwanzo na mwisho wetu. Hapo katikati, tunatofautiana sana. Ukishayajua hayo, huwezi kuudhulumu wala kuudunisha ubinadamu wa mwenzako.

Pole sana Mdude. Ni ngumu sana mwanadamu kuyasahau na kuyasamehe mambo mabaya na magumu uliyowahi kutendewa, lakini ni katika kusamehe ndipo nasi tunasamehewa. Hivyo nakuomba, uyasimlie haya katika maana ya kutukumbusha wajibu wetu kama wanadamu, na wala siyo kwa nia ya kuonesha chuki kwa waliotutendea ubaya.

Hadithio lako lina msaada mkubwa sana kwetu tuliobakia katika Ulimwengu huu. Marehemu amemaliza safari yake hapa Duniani, yaliyobakia ni kati yake na Muumba wake.

Tunaomba: Mungu utujalie neema ya kukuona wewe katika nafsi za wenzetu, hasa wale tunaoona tuna uwezo wa kuwakomesha au kuwakomoa.
 
Sikuona shida ya magufuli kulingana na lawama anazoelekezewa zaidi nyinyi wanaharakati kufanya harakati zenu bila staha, ajabu wewe aliyekutoa gerezani ulianza mapambano nae kwa kumwambia wembe uliomyolea magufuli ndio huo huo utakao tumia kumnyolea yeye!

Sasa kwa kauli kama hizo ulitegemea magufuli awe kiongozi wa namna gani dhidi ya watu kama nyie?
Yule mzee alikua na huruma sana.
 
Akaunti ya wakili inafungwa ili ashindwe kusafiri kumtetea mteja wake ! huu ni ukatili wa kishamba sana !

Mdude na Lisu, kuishi kwao mpaka sasa, ni kwa sababu Mungu aliamua kwaonesha wanadamu kuwa yeye akitaka mwanadamu asife, inakuwa hivyo.

Waliompiga risasi Lisu, walijiaminisha kuwa kwa namna ile walivyomchakaza, alikuwa tayari amekufa. Alipofikisglhwa hospitali wakajiaminisha kuwa hata kama alikuwa hajakata roho, ilikuwa ni suala la masaa tu kabla ya hilo kukamilika.

Mdude, walijua kuwa amekwishakufa tayari, wakamtupa kichakani, lakini Mungu alimwamsha, na bado yupo, akiwa na afya njema. Na siyo ajabu, walioamini kuwa walikuwa wamemwua watakuwa wametangulia wao au hata kama bado ni hai, Mdude anaweza kushuhudia vifo vyao.

Lisu yupo, tena mbele ya macho ya walioamini kuwa wamemwua. Mungu amewaweka hai baadhi ili waendelee kuyayashangaa maajabu ya Mungu, huku wakiishi bila amani wakiwa katika woga mkuu.
 

Mwanadamu hastahili kuishi au kuwa huru kwa hisani ya mwanadamu mwenzake. Kama mtu amekosea, kuna taratibu zilizowekwa katika jamii, ndizo zinazotakiwa kufuatwa, na siyo vinginevyo.

Kuhakikisha watu hawaonewi, Rais Samia ni wajibu wake wala siyo hisani au huruma.

Tunaposema kuwa Rais Samia aliwaachia walionewa toka magerezani na mahabusu, tusisahau pia kuwa ndiye aliyemwonea Mbowe, na kumsotesha mahabusu kwa karibia nusu mwaka. Bila ya msaada wa wazungu waliotoa shinikizo kwa Samia, hatujui mwisho wa Mbowe ungekuwaje. Na ni huyo huyo Samia ndiye asiyetaka nchi iwe na sheria nzuri ya uchaguzi wala tume huru ya uchaguzi, wala katiba nzuri ya nchi. Hivyo, Mdude kutoa kauli kali dhidi ya Rais Samia, alikuwa sahihi kama ambavyo ni sahihi hata sasa kumpa angalizo Rais kwa usanii wanaoufanya kuhusiana na demokrasia.

Kama unataka haki, kuna ubaya gani kuwa na chombo neutral kisicho na mwelekeo wa kuegemea kokote? Watu kama Mdude au Lisu ni wachache sana Duniani, watu walioamua kuyatoa maisha yao sadaka kwaajili ya wengi.
 
We nae ni mnafiki unafurahia wapalestina kuuliwa na waisrael huku unajifanya kumponda magufuli kwa kutotenda haki! Unasimamia kipi hasa?

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Duh
 
Hakika
 
G
Gereza gani limeruhusiwa simu mpuuzi wewe!
 
Ndio unachokoza mamlaka ili urudi kule kuna kitu ulikipenda uraiani unakikosa!
 
Dishi limeyumba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ