Salam.
Hii inatokana na mafanikio makubwa ya Yanga iliyoyapata na inayopanga kuyapata mengine..ndio maana hii habari ya yanga ya kutakiwa 'uongozi kuondolewa' imekuwa kubwa sana.
Kama yanga ingekuwa na migogoro kama siku za nyuma wala hii habari isingekuwa kubwa namna hii.
Nchi nzima leo ilikuwa Inasubiri saa nane mchana kutatoka habari gani huko Jangwani.Nahic hata kazi za kujenga uchumi kwa siku ya leo bongo zitakuwa zimelegalega kiasi fulani.Hata madeni leo yanaweza yakawa yamesamehewa kudaiwa na wenye madeni kupumua kidogo na kupata nafasi ya kujitafuta.
Ila kuna kitu cha kujifunza kwa hizi klabu mbili kubwa kuwa kuna suala la wazee viongozi na viongozi vijana kunatakiwa kuweka mambo sawa kwani kunaonekana bado kuna kukinzana kuwa nani mwenye timu.
Mimi toka nazaliwa nasikia kuna wazee wenye timu mpaka leo bado tu nasikia kuna wazee.Sasa nafasi yao iko wapi kama ipo basi ieleweke na wakae sawa na vijana Ili kujenga soka imara la taifa na sio malumbano kila kukicha.
Watanzania wengi walichoshwa na matokeoa mabovu ya vilabu vyetu hasa kimataifa,lakini kwa hiki walichofanya simba na yanga kwa miaka hii michache kimewatia moyo mashabiki na kuna mazuri yanaonekana kama yanataka kuja,sasa kama hii migogoro ikiendelea ya wazee na vijana basi hayo mafanimko tuyahasau katika soka la kimataifa.
Kwa sasa kila mtu anatamani kuziona simba na yanga zikicheza mechi mbalimbali kutokana usajili zilivyofanyika,wengine wanatamani hata ligi ianze kesho mradi waone wachezaji wao wapya.Sasa naona kunaibuka tena mpira wa nje ya uwanja sijui kama tutafika ngoja tusubiri tuone.
Alamsiki.