Nguvu moja
JF-Expert Member
- Oct 20, 2017
- 3,371
- 2,713
Niwatakie maandalizi mema na baraka tele members wote wa Jf, katika kuukaribisha mwaka mpya wa 2018, na kuuaga mwaka 2017 kwa amani tele mwenyezi mungu atubariki sote kwa pamoja, kama yupo yoyote, niliemkwaza kwa lolote lile, mpaka nikamkosesha amani moyoni mwake kwa wana Jf, yoyote naomba msamaha wa dhati kabisa kutoka ndani, ya moyo wangu, binadamu atujakamilika, mapungufu ayakosekani na mimi kwa upande wangu, sina kinyongo na yoyote humu ndani, moyo wangu mweupe na msafi kabisa kwa watu wote, kwanza nina furaha kubwa sana ya kuwemo humu ndani, kuna mengi sana ukiwa, Jf vya kujifunza na ukiweza kuishi humu, kwa amani basi popote unaweza ukaishi na watu vizuri sana tu, Jf ina mambo mengi sana ya kumfundisha na kumuelimisha, binadamu yoyote yule wa kawaida, baada ya kusema hayo kwa uchache, nataka utuambie sasa kitu gani uwezi..ukakisahau kilicho, katika kumbukumbu yako kilichotokea 2017, na unataka vitu gani...visitokee mwaka 2018. Na umejipangaje kuupokea mwaka 2018?