Karibu Bi Chausiku, mimi kwa jina naitwa Nyani Ngabu, meya mstahiki wa mji huu wa Jamiiforums.com. Nakukaribisha kwa mikono yote miwili na jisikie uko nyumbani. Endapo ukiwa na swali au maswali usisite kuniuliza kwani mimi ni mwenyeji wa siku nyingi tu hapa. Nimeshapitia kila aina dhoruba, misukosuko na mikikimikiki ya kila aina na ninazijua njia za hapa kama ninavyokijua kiganja cha mkono wangu kwa hiyo naweza kukwambia kwa uhakika kabisa ni njia ipi yenye makorongo na ipi ilonyooka.
Karibu sana.