HabariLeo kufungiwa?

.....Subiri akina FMES, Mwanakijiji na akina Halisi walete uthibitisho na the dataz, otherwise huu utakuwa "udaku!"

Udaku? Au natafsiri vibaya. Vyombo vya habari vimeandika na kuonyesha taarifa hiyo jana. 1. BBC saa 12 jioni, na 2. ITV taarifa ya habari jana saa 2 usiku. Wanapita huku hawa, watuambie waliandikaje jina la Mkuchika na kutoa taarifa zake? Ama ndo kujiuliza kama nako huku( Habari Leo) atawafungia, wakajisahau na kumtaja?
 
Hawa wahariri na waandishi wao wa habari njaa zinawasumbua.
 
Fidel, nataka kuanzisha bendi ya muziki wa bakurutu, naona hako kangedele/nyani katanifaa kwenye safu ya rhythm. Malipo- ndizi mbivu. Naamini utasaini 'deal'

-------------------
sema na watu upate kiatu
 
Swali ni kwa nini hawajafungiwa mpaka sasa hivi, double standard?
 
MwanaHalisi alisema wakasema mchochezi sasa imefika mahali pa wao kuukata mti wakiwa wameukalia wacha waumane yangu mambo .
 
Hongera habari leo. Mimi sioni lolote la maana wabunge wanaolalamika nikiwa mmoja wao nje ya bunge
kwa maana ya kwamba ukila lazima unajua tena..... na sisi jamani tunataka uwazi au kushabikia mambo kwa sababu ya precedent? Waziri Habari kafanya kosa la kwanza. Na je, tumruhusu kufanya kosa la pili kwa kisingizio cha equalization or rationality or justice or fairness? No way. Kosa ni kosa.

Hawa wabunge na Waziri wote wanakiuka haki ya msingi kama ilivyo katika katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nayo sio nyingine ila haki ya mtu kuzungumza au kueleza chochote kile alicho nacho bila kuingiliwa na mwingine. Na wewe ukiona umesemwa vibaya kuna MAHAKAMA nenda kawashtaki huko au nenda Baraza la Habari au nenda Jukwaa la Wahariri kama hutaki kuonana na majaji na mahakimu.....

Watanzania wenzangu, hii si miaka ya kujipendekeza kwa serikali kwa sababu ya kutaka ujiko tu. Tuwe kwa kweli kwa faida yetu na kizazi chetu kwa kutazxama ujinga uliotokea Kenya, Zimbabwe, Egypt, Ethiopia na nchi nyingine zilizoishiwa utu na ubinadamu miongoni mwa viongozi. Hii ni miaka ya kuwa huru kuzungumza na kusema chochote kinachokukera kwa sababu walioko madarakani wanashindwa kazi. Hawaiwezi nchi na ni rahisi sana kwao kugeuka kuwa madikteta ili kuficha udhaifu na kukosa kwao uwezo wa kuleta mabadiliko wananchi wanayoyatarajia.

Bunge wala serikali haviwezi kudai heshima wasiyoistahili. Wote hawa wameshindwa kupata heshima na imani zetu kwa kuwa wanatuharibia maisha na matarajio yetu eti.
 
Binafsi nilivyomuelewa Ole Sendeka ni kwamba alihoji uhalali wa hao habari leo kuwa huru bika kufungiwa wakati wao ndio wameandika uchochezi kuliko mwanahalisi.hapa anampima huy waziri wa michezo .nafikiri olesendeka ameona /amegundua kubenea anaonewa.na ndio mana anataka kuona hatua gani zitachukuliwa juu ya gazeti lao.
 

Mbona hatujasikia Habari Leo wakitatkiwa kupeleka utetezi kwa nini wasifungiwe? Au hapa kwetu sheria ni Msumeno kwa wasio connected?
 
Naona Halisi & Co. hawajafika bado kuweka mambo sawa hapa,

tehe tehe tehe, hii kitu imenipa raha sana. lol
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…