Jj football
New Member
- Mar 8, 2018
- 4
- 8
Ni hivi juzi tu Benchi la ufundi la Ngorongoro Heroes limewaita wachezaji wataotuwakilisha dhidi ya DR Congo kwenye Mechi za kufuzu Africa kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 20.
Nilishangazwa sana na baadhi ya wachezaji kutokuwepo kwenye kikosi hicho hasa Abdulnasry(Aspire),Daud Aboud,Adolph Mtasingwa na Wengine wengi lakini kilichonishangaza Zaidi ni kutoona jina la Habibu Kyombo wa Mbao Fc.
Nilijua labda Benchi la ufundi Taifa starz wanampango wa kumuita timu ya Wakubwa kutokana na kiwango bora alicho onesha msimu huu mpaka kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi December.
Maajabu ya Musa, jina la kijana huyu halipo Taifa stars wala Ngorongoro Heroes itayopambana na timu ngumu ya DR Congo.
Labda ufinyu wa Bajeti ndio unasababisha wachezaji wanaocheza njee kutojumuishwa kwenye vikosi vya timu zetu za Taifa ndio maana imekuwa ngumu kuitwa kuitumikia nchi yao hata hawa waliopo ndani kama Habibu kyombo nao hawaitwi duu!
Habibu Kyombo ndio kwanza ana umri wa miaka 18. Je mchezaji huyu mdogo atakuwa na moyo wa kizalendo kuitumikia timu yake ya Taifa kama Tff imeanza kumletea figisu figisu kwenye umri huu?
Tulikosea kwa Yusuph Poulsen mchezaji pekee mwenye asili ya Tanzania anayecheza Bundesliga na atayewawakilisha watanzania kwenye world cup lakini bado tunarudia makosa yaleyale kila siku.
Unadhani Ghana wasinge watuma wawakilishi wao njee hasa ulaya kuwashawishi wachezaji wao wanaocheza soka ulaya kama wakina Kevin Prince Boateng wangefanya vizuri Kombe la Dunia.
Mwisho, Napenda kumnukuu Yussuph Poulsen "Sikuchagua kuichezea Taifa stars kwasababu sikuwai kupokea offer yoyote kutoka Tanzania" Mwisho wa kunukuu.