Habibu Haji Kyombo njia nyeupe Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

kibol

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2012
Posts
4,521
Reaction score
2,747
Taarifa kutoka katika klabu hiyo zinaeleza kuwa Habibu Kyombo alifanyiwa vipimo hivyo jana majira ya saa 7:00 mchana katika makao makuu ya klabu ya Mamelodi Sundowns nchini Afrika Kusini na sasa kinachoendelea ni makubaliano binafsi ya mchezaji na klabu hiyo.
" Tunamshukuru Mungu kwa hatua hii, hatua kubwa kwa klabu yetu na kubwa kwa mpira wa nchi yetu, Kyombo amefungua mlango, wengine wanafuata kupitia Singida United, kikubwa kujitambua na kuvumilia (Self determination) ," imeeleza taarifa ya Singida United iliyotolewa katika mitandao ya kijamii.
Habibu Kyombo anakuwa mchezaji wa pili kwa Singida United kuuzwa nje ya nchi msimu huu, mchezaji wa kwanza ni Ally Hamis Ng'anzi aliyefuzu vipimo katika klabu ya MFK VySkov inayoshiriki ligi daraja la pili, nchi ya Jamhuri ya CZech.
 
Inaonekana viongozi wa singida united hawajazubaa kama wa yanga

Kitu kidogo tu utasikia bakuli la kuichangia timu
Wao wako busy kuparurana tu, wenzao wanauza wachezaji nje ya nchi, poor chura fc.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…