Tetesi: Habibu Kyombo na Onyango wanukia Singida Fountaingate

Tetesi: Habibu Kyombo na Onyango wanukia Singida Fountaingate

Soloma TV Online

Senior Member
Joined
Jun 26, 2023
Posts
104
Reaction score
291
Wachezaji wa Simba HABIBU KIYOMBO NA JOASH ONYANGO wanaweza kujiunga na Timu ya Singida Fountaingate ya Singida.

Wachezaji hawa wanaweza kuondoka iwapo tu Simba itawapa mkono wa kwa heri au hata kuwatoa kwa mkopo.

Joash Onyango amekuwa akiomba kuondoka klabuni hapo kwa muda mrefu na hilo kwa sasa linaweza kufanikiwa.

Kwa upande wa Habib Kiyombo hajafanikiwa kuwa na msimu mzuri ndani ya timu ya Simba hivyo lolote linaweza kutokea kwake.

Baada ya hayo kufanikiwa kwao itakuwa njia nyeupe kwa walima ALIZETI wa mkoani Singida kuwatia mikononi mwao.
 
Bado kwa Habib Kiyombo atakuwa amependelewa sana kwenda hiyo timu. Maana yeye ni mchezaji anayeng'ara kwenye timu ndogo.

Alifanya vizuri akiwa Mbao FC na Mbeya Kwanza. Nje ya hizo timu mbili, hakuna mahali pengine alipo onesha maajabu.
 
Kyombo karidhika sana pale Simba, anahitaji changamoto mpya. Tumpeleke Mashujaa halafu awe chini ya uangalizi maalumu wa yule mpuuzi aliyefungiwa, ajue maisha ya mwanaume ni harakati siyo kuchekacheka tu halafu juhudi zero.
 
Hahahahaha akakutane na mike.
 
Kyombo alikosea kuja Simba

Simba walikosea kumtoa Singida
 
Back
Top Bottom