Hackers kiboko wameiba pesa nyingi balaa

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
620
Reaction score
1,240
Hackers kiboko wameiba pesa nyingi balaa



Benki kuu ya Uganda (BOU) inasema inasubiri ripoti ya uchunguzi toka kwa polisi nchini Uganda juu ya tukio la wizi wa Fedha zaidi ya dollar milioni $17, Sawa na billion 62.4 za Uganda.

Taarifa inaonyesha kikundi Cha watu kadhaa wa uhalifu mtandaoni ambao wanajiita "WASTE" toka kusini mashariki mwa Asia, walifanikiwa kuingia kwenye mifumo ya network ya IT na kufanikiwa kuchukua kiasi Cha shilingi bilioni62.4.



Inaonyesha mifumo ya usalama ilikua haina nguvu nakupelekea Kikundi Cha WASTE kuweza kuingia kwenye mfumo wao kiurahisi.

Bado haijajulikana kama lengo la Waste ni kuchukua tu pesa bilioni 62.4 au walikua wanatafuta kitu kingine ndo wakaamua kuchukua tu izo pesa.

Naibu mkurugenzi wa benki kuu ya Uganda (BOU) Dkt Natamba Bazinzi, alisema inasubiri ripoti kamili kuhusu tukio hili toka Polisi Kwani imepita wiki mbili toka tukio litokee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…