Hadi Marehemu Diego Maradona akizikwa kuna Watanzania nao wanaweza Kutunukiwa Shahada ya Juu ya Uwongo

Hadi Marehemu Diego Maradona akizikwa kuna Watanzania nao wanaweza Kutunukiwa Shahada ya Juu ya Uwongo

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Tangia Taarifa ya Kifo chake itangazwe rasmi Jana na Watu kuanza kutoa Rambirambi ( Pole ) zao ama hakika kila ninaposikiliza Vipindi mbalimbali vya Redioni hata kama siyo vya Michezo nimegundua ya kwamba Watanzania ni Waongo sana hasa katika Kuelezea jinsi wanavyomjua Marehemu Diego Armando Maradona.

Mtanzania #1 aliyehojiwa

Ndugu Mtangazaji nakuambia namjua Diego Maradona tokea akicheza Kombe la Dunia miaka ya 60 huko nchini Taiwan

Mtanzania #2 aliyehojiwa

Nimesikitika mno tu kwa Kifo chake Diego Maradona kwani nilibahatika Kuonana nae Mubashara ( Live ) katika Television.

Mtanzania #3 aliyehojiwa

Nimeumia mno na Kifo chake Maradona kwani mwaka 1959 akicheza Kombe la Ameica ya Kusini alifunga bonge la Goli

Mtanzania #4 aliyehojiwa

Nakumbuka nilikaa nae katika Siti moja ya Ndege ambapo kutokana na Unene wake na Kunibana nilimwomba Rubani niweke Kigoda njiani nikae

Mtanzania #5 aliyehojiwa

Marehemu Diego Maradona alikuwa ana uwezo wa Kupiga Chenga Wachezaji wote Uwanjani kisha akahamia kwa Mashabiki na Kuwapiga Chenga

Mtanzania #6 aliyehojiwa

Niliwahi Kukaa katika Ukumbi Mmoja na Marehemu Diego Maradona huko Marekani na alipoondoka alinipa Pesa ya Kununua Ice Cream

Mtanzania #7 aliyehojiwa


Namkumbuka Marehemu Diego Maradona kwani nje tu ya Kucheza Mpira kwa Umahiri wake wote pia aliwahi kuwa Rais wa nchini Argentina 1950
 
Tea
Screenshot_20201126-232931.jpg
 
Hii ya maradona ni cha mtoto,wapo wanaosimulia vita ya kagera,eti waliingia mtukula,entebe mpaka jinja japo walikuwa ni migambo wakamfurusha idd amin,kuna wanaopenda kujitwisha sifa za uongo waonekane ni wajuaji
 
Maradona nilisoma nae darasa moja shule ya msingi, alikuwa na tabia ya kuwachungulia wasichana kwa kuweka kioo chini
 
Back
Top Bottom