Hadi sasa hii ni baadhi ya misaada na mikopo Serikali iliyokopa

Hadi sasa hii ni baadhi ya misaada na mikopo Serikali iliyokopa

Mkwawe

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2016
Posts
3,132
Reaction score
5,508
JAMHURI YA MUUNGANO WA KOREA TANZANIA DOLA BILIONI MOJA..

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Korea kwa kutenga kiasi cha dola za Marekani Bilioni 1 zitakazotolewa kwa njia ya mkopo nafuu kwa Tanzania kupitia Mfuko wa Shirika la Maendeleo ya Kiuchumi (EDCF), kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kipindi miaka mitano

Dkt. Nchemba ametoa shukrani hizo jijini Dodoma, alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri anayesimamia uratibu wa masuala ya Sera wa Korea Mheshimiwa Moon-Kyu Bang, alipokutana na kufanya mazungumzo naye akiwa katika ziara ya kikazi nchini.

"Septemba mwaka 2022, Tanzania na Korea tulisaini makubaliano yatakayoiwezesha Tanzania kupata mkopo wenye riba nafuu wenye thamani ya dola za Marekani bilioni moja ambapo Tanzania itakopa mkopo huo kwa riba ya asilimia 0.01 kwa mwaka na kuulipa kwa kipindi miaka 40 ambacho kimeambatana na kipindi cha neema cha miaka 15"

Dkt. Nchemba ameishukuru Korea kwa kuahidi pia kusaidia utekelezaji wa miradi miwili mipya ukiwemo mradi wa maji na usafi wa mazingira mkoani Iringa wa Iringa na ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Binguni-Zanzibar, ambayo italeta manufaa makubwa kwa Wananchi.

Chanzo: Msasa
*****

ABU DHABI: Serikali ya #Tanzania na Falme za Kiarabu (UAE), kupitia Mfuko wa Maendeleo wa #AbuDhabi zimesaini Mkataba wa Mkopo wa zaidi ya Tsh. Bilioni 70 kwaajili ya Ujenzi wa njia ya kusafirisha Umeme kutoka Benaco hadi Kyaka, Kagera na Upanuzi wa Kituo cha Kupoza Umeme Kyaka, unaokadiriwa kugharimu Tsh. Bilioni 298.5

Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema, Mkopo huo utaongeza nguvu kwa kujumuisha na Fedha za Mfuko OPEC Fund for International Development uliotoa Tsh. Bilioni 150, Mfuko wa Maendeleo wa Saudia Tsh. Bilioni 32.5 na Serikali ya Tanzania iliyochangia Tsh. Bilioni 6

Soma https://jamii.app/MkopoAbuDhabi

#JamiiForums #ForeignLoans #Governance
*****

UCHUMI: Tanzania imesaini Mkataba wa Msaada wa Tsh. Bilioni 82.4 zilizotolewa kupitia Shirika la Invest International la Uholanzi ikiwa ni sehemu ya gharama za Mradi wa Uendelezaji Bonde la Msimbazi, utakaogharimu Tsh. Bilioni 651.2

Kati ya Fedha hizo, Benki ya Dunia (WB) itatoa Tsh. Bilioni 500 na Serikali ya Hispania itatoa Tsh. Bilioni 82.4 kwa Mkopo wa Riba nafuu unaotarajiwa kuondoa mafuriko kwa kujenga njia za kuelekeza Maji, Kingo za Mto, kudhibiti kujaa mchanga na mmomonyoko wa udongo kwenye Mto

Pia, Fedha zitatumika kupanua na kujenga Daraja la Juu (Flyover) katika eneo la Jangwani pamoja na kuhamisha Kituo Kikuu cha Mabasi Yaendayo Kasi cha Jangwani kwenda eneo la Ubungo Maziwa

Soma Uholanzi yaipa Tanzania Msaada wa Tsh. Bilioni 82 kwaajii ya Ujenzi wa Daraja la Juu Jangwani

#JamiiForums #Governance #JFHuduma #Economy #ServiceDelivery
*****
ALERT 🚨 🚨 🚨

Tanzania imesaini mkataba wa mkopo wa masharti nafuu wa $1bn (trn 2.3/-) na Korea Kusini ili kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo kuanzia 2022 - 2025. Fedha hizi zimepigwa hakuna miradi yoyote imetekelezwa Wala hakuna plan yoyote 📌📌

Kabla ya hapo serikali ya Korea ilitoa mikopo ya masharti nafuu yenye thamani ya $140m kuanzia 2021 hadi 2023.
*****
#UCHUMI: Serikali ya Tanzania imesaini Mkopo wa Tsh. Bilioni 32.5 kutoka Mfuko wa Maendeleo wa #SaudiArabia kwaajili ya ujenzi wa njia ya Msongo wa Umeme wa Kilovolti 220 yenye urefu wa Kilometa 167 pamoja na kuboresha eneo la Benaco - Kyaka

Mradi wa Kyaka- Benaco umekuwa ukitekelezwa kwa msaada wa Fedha kutoka katika Muungano wa Nchi Zinazouza Mafuta/Petroli (#OPEC) ambao tayari umechangia Tsh. Bilioni 150.3, Mfuko wa Maendeleo wa #AbuDhabi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (#UAE) Tsh. Bilioni 75.1 na Serikali ya Tanzania Tsh. Bilioni 6.

Soma Tanzania yakopa Tsh. Bilioni 32 Kutoka Saudi Arabia wakati wezi wakiiba mabilioni

#JamiiForums #Governance #Accountability #TanzaniaEconomy

*****
#HABARI: Serikali ya Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Korea zimesaini Mkataba wa Mkopo nafuu wa Shilingi bilioni 422.16 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Binguni, Zanzibar.

Mkataba wa Mkopo huo umesaimiwa Jijini Soeul na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu Mwamba, kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na kwa upande wa Korea umesainiwa na Mkurugenzi Mtendaji Mwandamizi na Mjumbe wa Bodi wa Benki ya Exim - Korea, Mr.Hwang Kiyeon.
Chanzo: ITV

*****

SERIKALI YASAINI MKOPO WA MASHARTI NAFUU TSH. TRILIONI 1.264 KUTOKA BENKI YA DUNIA

Wizara ya Fedha na Mipango leo Februari 28, 2023 imesaini Mikataba ya Mikopo miwili yenye masharti nafuu na Benki ya Dunia (WB) kwaajili ya kuboresha Huduma endelevu za Maji, Usafi wa Mazingira Vijijini na Afya ya Mama na Mtoto.

Kati ya Fedha hizo, Tsh. Bilioni 689.51 zitatumika katika Mpango Endelevu wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini ambazo ni Mkopo wa Masharti Nafuu wa IDA, na Tsh. Bilioni 574.59 zitaenda kwenye eneo la Mradi wa Afya ya Mama na Mtoto.

Kwenye picha ni Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba (Mb) na Mkurugenzi Mkazi wa @worldbanktz, Bw. Nathan Belete wakibadilishana Mikataba miwili ya mkopo wenye masharti nafuu na msaada wa dola za Marekani milioni 550 (sh. trilioni 1.264) kwa ajili ya kuboresha sekta za maji na afya ya mama na mtoto, wakishuhudiwa na Naibu Waziri wa @wizara_afyatz, Mhe. Dkt. @dr_mollel (kulia), jijini Dar es Salaam.sasaKisasaZaidi
Chanzo: Msasa
*****
BENKI YA DUNIA YAIKOPESHA TANZANIA TSH. TRILIONI 1.8

Mkopo huo uliotajwa kuwa wa masharti nafuu pamoja na Misaada mingine unalenga kusaidia Uchumi na Sekta ya Afya Nchini

Mkopo unatarajiwa kuanza kuingia Desemba 23, 2022

Soma https://jamii.app/MkopoTZ

#Governance
*****
BENKI YA DUNIA (WB) YAIKOPESHA TANZANIA TSH. TRILIONI 2.3391

Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu amesema WB imeidhinisha mikopo ya masharti nafuu itakayotumika kwa Miradi ya Maendeleo ikiwemo uboreshaji wa Barabara za Vijijini na Fursa za Kijamii (RISE)

Soma Benki ya Dunia yaikopesha Tanzania Tsh. 2.3 trilioni

Juni 6 2021

*****

IMF yaikopesha Tanzania Sh358.9 bilioni ya utekelezaji wa bajeti

Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) imeridhia kuikopesha Tanzania dola milioni 153 (Sh358.9 bilioni) kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa bajeti yake ya Serikali.
Taarifa ilitolewa na Shirika hilo kupitia kwenye tovuti yake, imeeleza kuwa fedha hizo zinafanya jumla ya mkopo kufikia dola milioni 305 (Sh715.5 bilioni) kati ya dola bilioni 1.04 (Sh2.4 trilioni) zilizoidhinishwa kwa Tanzania, 2023. Imeongeza kuwa licha ya kuwepo kwa changamoto za kiuchumi duniani lakini Tanzania inachukua hatua nzuri kwenye eneo hilo, hivyo imeitaka mamlaka kufanya kazi ili kuongeza mapato ya ndani, kupunguza urasimu na kukabiliana na rushwa ili kujiimarisha zaidi kiuchumi.
Aidha, IMF imetoa angalizo kwa Tanzania kujiimarisha kwa kuboresha ufanisi wa matumizi ya fedha na kukwepa malimbikizo ya madeni ya ndani. Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi wa IMF, Antoinette Sayeh amesema kwa sasa deni la Tanzania bado ni himilivu na la wastani.

April 26 2023

*****
JAPAN YAIKOPESHA TANZANIA SHS BILIONI 174.8

Tanzania na Japan kupitia Shirika lake la Ushirikiano wa Kimataifa (@jica_direct_en ), zimetiliana saini mikataba mitatu ya mkopo nafuu na msaada wenye jumla ya Yen bilioni 10.15 sawa na shilingi za Tanzania bilioni 174.8, kwa ajili ya kuendeleza kilimo na uvuvi, ambapo katika sekta ya kilimo, mkopo huo utatumika kununua pembejeo za kilimo ikiwemo mbolea, utoaji wa mbegu bora na kuongeza uzalishaji wa mazao ya mpunga, ngano na alizeti, huku sekta ya uvuvi itanufaika na msaada utakaotumika kufufua Shirika la Uvuvi Tanzania (@taficotz ), kwa kununua meli ya kisasa ya uvuvi na miundombinu ya kuhifadhi samaki.
April 27 2023

*****
UCHUMI: Bodi ya Utendaji ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) imeidhinisha jumla ya Dola za Marekani Milioni 935.6 (Tsh. Trilioni 2.45) kwaajili ya Serikali ya #Tanzania ikiwa ni ukamilishaji wa Mapitio ya 3 ya Mpango wa Upanuzi wa Mikopo kwa Tanzania (ECF) ulioisainiwa Julai 2022

Kwa mujibu wa taarifa ya IMF, Dola Milioni 149.4 (Tsh. Bilioni 392.17) kati ya Fedha hizo zitaenda kwenye Bajeti ya Serikali na Dola 786.2 (Tsh. Trilioni 2.06) ni kwaajili ya Miradi ya Kukabiliana na Mabadiliko ya TabiaNchi

Awali, Julai 2022, Bodi ya Utendaji ya IMF iliidhinisha utaratibu wa nyongeza wa Miezi 40 chini ya Mpango wa Upanuzi wa Mikopo (ECF) kwa Tanzania uliowezesha makubaliano ya kupata mkopo wa Dola za Marekani Milioni 1,046.4

Soma IMF yaidhinisha Tsh. Trilioni 2.45 kwaajili kusaidia Tanzania kukabiliana na Mabadiliko ya TabiaNchi na Bajeti

#JamiiForums #Governance #Economy #Accountability

*****

Tanzania imepokea msaada wa nyongeza wa Yen za Japan Milioni 548 (Tsh. Bilioni 8.9) kwa ajili ya mradi wa ukarabati wa Bandari ya Kigoma baada ya marekebisho ya mikataba miwili ya msaada kati ya Tanzania, Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) na Ubalozi wa Japan

Mikataba hiyo imesainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, Balozi wa Japan nchini Tanzania, Yasushi Misawa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan Tanzania, Hitoshi Ara kwa niaba ya Japan

Dkt. Mwamba amesema, awali Serikali ya Japan kupitia mikataba iliyosainiwa Februari 4, 2022 ilitoa msaada wa Yen za Japan Bilioni 2.73 (Tsh. Bilioni 44.42) kwa ajili ya ukarabati wa Bandari hiyo, hivyo jumla ya msaada waliotoa ni Tsh. Bilioni 53.35.

Soma Tanzania yapokea msaada wa Tsh Bilioni 8.9 kwa ajili ya mradi wa ukarabati wa Bandari ya Kigoma

#JamiiForums #JFUchumi #Economy #Diplomacy

*****
 
Back
Top Bottom