Uchaguzi 2020 Hadi sasa kimkakati CHADEMA wameizidi CCM

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Uchaguzi ni takwimu, mikakati na mipango ambayo inaonekana wazi kwa macho na isiyoonekana. Kwa inayoonekana ni wazi kuwa....

Pamoja na CCM kuwa na kila kitu kinachotakiwa kwenye kampeni, magari, viwanja, pesa you name it, lkn haina tofauti kubwa na Chadema inayotumia resources chache ilizonazo kwa makini.

Hadi sasa CHADEMA imezindua kampeni katika Kanda kuu zote za Tanzania bara na Zanzibar, huku CCM mgombea wao akizunguka kwenye mikoa michache ya kanda ya kati na Ziwa Victoria tu.

Chama cha Mapinduzi kimehodhi vyombo vyote vya habari TV zote, redio zote, magazeti yote lkn habari zinazo trend zaidi ni za mgombea wa CHADEMA Tundu Lissu.

Katika kuuza sera CCM wamekuwa wakijitetea zaidi kuliko kutangaza sera zao, mfano juzi mgombea wa CHADEMA alihoji ajira leo serikali imetangaza ajira 13,000 za walimu, Lissu kaongelea bima ya Afya kwa wote Magufuli na Majaliwa nao wanasema watatoa bima bure wakati haipo kwenye ilani yao.

CCM imetandaza mabango ya picha kubwa kubwa za mgombea wao nchi nzima karibu kila ukuta huku Chadema ikionekana kutokuwa na mabango lkn mwitikio wa wahudhuriaji hauna tofauti yoyote.

Pamoja na CCM kuwatumia wasanii wote wa Tanzania na wa nchi jirani ya Kenya bado haijawasaidia kuonyesha nguvu ya chama tawala na kikongwe kwenye kampeni yao.

CCM pesa wanayo vyombo vyote vya dola ni vyao, nini tatizo, inawezekana ni kampeni meneja na timu yake ya kampeni, ni wazito au wamefungwa kutoa maamuzi ya haraka.

Katika tathimini yangu kwa siku hizi za mwanzo wa kampeni CHADEMA imewazidi CCM kwa pointi ingawa siyo nyingi sana.
 
Napenda sana Chadema mnavyojipa moyo.

Kwa taarifa yako kampeni ya mkoa mmoja aliyofanya magufuri ni sawa na mikutano yenu yote Chadema iliyofanya katika kanda zote mpaka sasa. CCM ni chama kubwa nadhani leo umeiona vizuri mwanza. CCM KIRUMBA hakukuwa na sehemu ya kutema mate ndani na nje acha kule gola milimani.
 
Hivi nyie bado mna mawazo ya kushindanisha na ccm.CCM wamemaliza kampeni leo pale Mwanza mnazoleta humu ni porojo tu.Fuatilia channel ten saa hivi Magufuli yuko zake Mwanza anapunga upepo na punde kapiga simu kwenye mkutano wa kampeni kule Rombo kaongea na wananchi na kuomba kura kwake kwa mbunge na madiwani. Chadema achaneni na Magufuli mtatapika damu
 
Tayari kule Rombo kura mbunge Prof Mkenda na kwa Chumaaaa Magubaba, madiwani kura za kumwaga.Magufuli sasa anatumia video conference kuhutubia mikutano ya mbali, sasa hivi kaungana na jembe number2 KK Majaliwa kuhutubia wana ROMBO. MAGU ON FIRE
 
Sawa umejiuliza kwanini shule hazijafunguliwa leo wakati watoto walitakiwa wawe madarasani, hizo ndizo strategy nazosema CCM wanafeli ikiwa ni pamoja na kulinganisha idadi ya watu na chama kama CHADEMA kisicho na uwezo wa kufunga shule.
 
Tayari kule Rombo kura mbunge Prof Mkenda na kwa Chumaaaa Magubaba, madiwani kura za kumwaga.Magufuli sasa anatumia video conference kuhutubia mikutano ya mbali, sasa hivi kaungana na jembe number2 KK Majaliwa kuhutubia wana ROMBO.MAGU ON FIRE
Anahutubia kwa video conference Tanzania?
 
Kwa hiyo?
Ccm inaondoka! Ila hutaumia Kwa sababu, sera za CHADEMA za kudumisha diplomasia zitakugusa hata Wewe, kwa mfano uraia pacha! Mboga mboga wote hawapendi mahusiano ya kimataifa, kitu ambacho kama hakita kuathiri Wewe kitathiri watoto wako unaozaa huko unakobeba box!
 
Kwanza JPM ilikua si lazima afanye kampeni kazi za serikali zina lala, Yeye ilitakiwa ahutubie wananchi akiwa kama mgombea wa CCM siku moja kabla ya uchaguzi. Kazi nzuri alizofanya zimesha mrudisha tena ikulu.
Tatizo unaangalia kampeni mtandaoni.
 
Ndio Maana Mimi nataka Magufuli Endelee kuwa Rais ili Vijana wenye Ufahamu na Ujinga Wa Makusudi mpate Ufahamu Unajua Nguvuu ya MABANGO na matangazo OBAMA ALIKUWA NA UHAKIKA WA USHINDI ILA HAKUACHA KUWEKA MABANGO ALIPOGOMBEA MHURA WA PILI HAKUWACHA KUWEKA MATANGAZO REDION NA KWENYE TV MABANGO YANA NGUVU SANA BIASHARA BILA MATANAGZO HUKWAMA COCA MPKA LEO WANAMABANGO NI SODA YENYE UMRI MKUBWA INGEJIACHIA LAKINI INAJUA UMUHIMU
 
CCM kama imewatupa magwiji wa siasa Abdulhaman Kinana, Nnape Moses Nnauye na January Makamba, then lazima mikutano yao ya kampeni idode sana.

Na pale kidogo wanapoonekana kuhema, basi ndo utambue kuwa wametumia nguvu na pesa nyingi sana kuliko kawaida.

Hapa Shinyanga na siku mbili tatu zilizopita nilikuwa Tabora, utashangaa jinsi ambavyo mgombea wao amechafua mandhari ya miji hii kwa kubandika mipicha mikubwa mikubwa yenye sura mbaya ya mgombea wao.

Kwa ufupi wanatumia fedha nyingi sana tena za wizi kutoka ktk hazina ya nchi.

Ni wazi kuwa fedha wanayotumia kwenye kampeni hizi ni ile 1.5trn na pesa za mauzo ya vitambulisho vya wamachinga a.k.a wajasiriamali!

Huu ni uthibitisho kuwa chama hiki kinaishi kwa taabu na kamba iliyokining'iniza kukipa pumzi ya mwisho inaweza kukatika wakati wowote.
 
Niliwai sema na nasema tena Tundu Antiphas Lissu ni sawa na Mfalme Daudi na Magufuli ni sawa na Mfalme Sauli.

Sauli alikuwa na majeshi, fitna na fedha za kumshinda Daudi ila Daudi alikuwa na Mungu tu na Mungu aliweza kumshindia vita dhidi ya Sauli!
 
Kwanza JPM ilikua si lazima afanye kampeni kazi za serikali zina lala, Yeye ilitakiwa ahutubie wananchi akiwa kama mgombea wa CCM siku moja kabla ya uchaguzi. Kazi nzuri alizofanya zimesha mrudisha tena ikulu.
Jiandae kwenda nae chato baada ya sisi wananchi kumstaafisha rasmi hapo 28 October 2020.
 
Nani kasema Chadema wasiweke mabango wasitangazwe kwenye TV, hata wakitaka TV gani itakubali, ninachosema pamoja na kunyimwa access hizo zote bado wanaenda sambamba na CCM wenye access hizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…