Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
Mchumba anapochumbiwa hiyo nayo huwa ni ahadi.....
Ahadi inapoota mbawa aliyeahidiwa huachiwa maumivu.......
Mwaahidi aweza kuwa na sababu za kigugumizi lakini...
Mwathirika wake hataki kusikia akiamini amedhulumiwa......
Sasa awavutia pumzi hadi watakapopeana migongo.
Mwaahidi aweza kujitetea ya kuwa kapata "second thought"..
Au hata wazazi waweza kutumiwa kuziba mashimo............
Lakini kwa mwathirika huo utetezi ni hila ya kumkatili tu.....
Mwathirika ashindwa kuelewa ni wapi alikosea au kapungukiwa na nini?

Mwathirika sasa abubujikwa na chozi na hasira kumkereketa.....
Atakacho sasa ni kujibu mapigo na mtesaji wake kuwajibishwa..
Mwaahidi sasa ataka shwari na kuwa yote yawekwe kapuni......
Mwaahidi amfariji mwathirika wake kuwa atapata mwingine.....

Mwathirika ajibu mapigo kwa kujipatia kijana nadhifu...
Taswira ya kijana yazidi hata ya yule nduli wa mwathirika............
Lakini ghadhabu ya kisasi kamwe siyo kikamilifu hadi mnufaikaji atakapowajibishwa
Mnufaikaji ni yule aliyempora mwathirika na muarobaini ni kukumbushia na zilipendwa

Msaliti naye kanuna baada ya kusikia mapigo ya mwathirika.....
Mnufaikaji yeye hana khabari na dhoruba kwani hamjui mwathirika........
Kweli kisasi chamwuumiza mwenye nacho na wala siyo mkusudiwa........
Kwani kosa la mnufaikaji ni lipi kwani dhoruba hata hazijui?