...........hadi watakapopeana migongo!

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
219,468
Reaction score
911,184
Mchumba anapochumbiwa hiyo nayo huwa ni ahadi.....
Ahadi inapoota mbawa aliyeahidiwa huachiwa maumivu.......
Mwaahidi aweza kuwa na sababu za kigugumizi lakini...
Mwathirika wake hataki kusikia akiamini amedhulumiwa......
Sasa awavutia pumzi hadi watakapopeana migongo.

Mwaahidi aweza kujitetea ya kuwa kapata
"second thought"..
Au hata wazazi waweza kutumiwa kuziba mashimo............
Lakini kwa mwathirika huo utetezi ni hila ya kumkatili tu.....
Mwathirika ashindwa kuelewa ni wapi alikosea au kapungukiwa na nini?
Sasa awavutia pumzi hadi watakapopeana migongo.

Mwathirika sasa abubujikwa na chozi na hasira kumkereketa.....
Atakacho sasa ni kujibu mapigo na mtesaji wake kuwajibishwa..
Mwaahidi sasa ataka shwari na kuwa yote yawekwe kapuni......
Mwaahidi amfariji mwathirika wake kuwa atapata mwingine.....
Sasa awavutia pumzi hadi watakapopeana migongo.

Mwathirika ajibu mapigo kwa kujipatia kijana nadhifu...
Taswira ya kijana yazidi hata ya yule nduli wa mwathirika............
Lakini ghadhabu ya kisasi kamwe siyo kikamilifu hadi mnufaikaji atakapowajibishwa
Mnufaikaji ni yule aliyempora mwathirika na muarobaini ni kukumbushia na zilipendwa
Sasa awavutia pumzi hadi watakapopeana migongo.

Msaliti naye kanuna baada ya kusikia mapigo ya mwathirika.....
Mnufaikaji yeye hana khabari na dhoruba kwani hamjui mwathirika........
Kweli kisasi chamwuumiza mwenye nacho na wala siyo mkusudiwa........
Kwani kosa la mnufaikaji ni lipi kwani dhoruba hata hazijui?
Sasa awavutia pumzi hadi watakapopeana migongo.
 
mbona tunatoneshana vidonda jamani......

Wajaman Smile....................hata wewe kinda una vidonda...nilifikira kauli yako kuwa bado mweupe kabisa ni kweli?[MENTION]@Smile[/MENTION]
 
Huyo wakwanza alidhani mwenzake kuachwa hatapa na yeye wakwake??sasa yanini anune kwani hakujua aendelee na maisha yake na huku muhathirika na kijana wake!!
 
Yaani mimi siku hizi ananiudhi na haya mathread yake yenye ukweli mchungu! Halafu anakutag; ili uyasome hata kama hutaki!

Kaunga mbona wanichanganya hivyo..................nilifikiri umo ndani ya merikebu shwari sasa hizi hisia zako zaniacha na maswali mengi na sina majibu.......[MENTION]@Kaunga[/MENTION]
 
Huyo wakwanza alidhani mwenzake kuachwa hatapa na yeye wakwake??sasa yanini anune kwani hakujua aendelee na maisha yake na huku muhathirika na kijana wake!!

nduli mara nyingi hufikiri anachoona yeye hakifai basi sote tutaona hivyo...kumbe ganda la mwua la jana chungu kaona kivuno..............[MENTION]@KakaKiiza[/MENTION]
 
Merikebu shwari unaipata pale unapoamua kuwa 'the captain of your own ship'. Don't let your happiness rotate around others. Ati mi naona mwenza anaekufa huku anakupenda anauma kuliko anaekuacha kwa sababu ya green pastures! I always think of a more worse scenario and thank God ( ndo campus ya ship nnayoendesha baharia le mutuz mie,lol)
 
Yaani mimi siku hizi ananiudhi na haya mathread yake yenye ukweli mchungu! Halafu anakutag; ili uyasome hata kama hutaki!
sio fair bwana ..... kama leo asubuhi hii siku yangu ishaharibika....
 
ni mgeni na hili....siwezi simama:car:
 

King'asti.wengi hatuko hivyo....................tupo tayari kuwaachia wengine wawe manahodha wa merikebu zetu na wanapotupeleka kusiko huishia malalamiko na visasi tupu........[MENTION]@King'asti[/MENTION]
 
ni mgeni na hili....siwezi simama:car:

Vaislay.lisemwalo lipo kama halipo jua lipo njiani laja....................yatakukuta tu.......[MENTION]@Vaislay[/MENTION]
 
sio fair bwana ..... kama leo asubuhi hii siku yangu ishaharibika....

ukweli sasa siyo fair deal.......................kesho nitakuja na uongo wa kuwapendezeni. [MENTION]@Smile[/MENTION]
 

Ili uwe successive captain wa sheep yako, uwe Solo; usitegemee assistance from anyone or thing! Sometimes hata maprogram ya computer yanatudisappoint!
 

Kumbe na wewe ni malenga. Big up sikujua kuwa nshomile nao wanakijua kiswahili. Ila haya mambo yamekutokea wewe au unawasilisha kilio cha waathirika wa haya mambo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…