Hadithi: Mpangaji

MPANGAJI 15
By CK Allan

Walijitahidi kuwakwepa waandishi wa habari pale Nairobi na kisha kufanya hivyo hivyo pale uwanja wa ndege na hatimaye walipofika JKNIA tayari Mr K alikua ameshaanda utaratibu wote
“tafadhali sema kitu mr Sele je wewe ndio mtoto wa Bwana Lukas, unayeitwa Gift?”
“nitasema kila kitu muda mfupi ujao kila kitu kitakuwa wazi” alisema Sele akiingia kwenye gari na kuelekea sasa yalipo makao makuu ya kampuni yao maeneo ya Buguruni Chama
Walifika muda mfupi na kumaliza taratibu zote na kisha wakaingia kwenye chumba cha mikutano na kuanza mahojiano
Sele alieleza yote kuanzia mwanzo wa maisha yake huku baadhi ya matukio akijizuia kutoa machozi,
“sasa ni kwanini ukakaa kimya muda wote huo kipindi chote hicho labda kwanini usingetoa taarifa hizo mapema?” lilikua ni swali kutoka kwa mwandishi mmoja, hata hivyo kabla ya kujibu mr K alimzuia kidogo kisha akawakonyeza wafanyakazi baadhi ambao waliondoa kitambaa kilichokuwa mbele yao na kuonekana tv kubwa hivi kisha sasa Mr k akaunganisha na simu yake na sasa mbele yao alikua yupo Doren akiwa ametulia katika chumba chake
Baadae Sele akaletewa kifaa kidogo cha kupazia sauti na wakaanza maongezi yao
“okay nataka kujibu ilo swali la mwandishi hapo ameuliza kwanini tulikaa kimya muda wote huo? Si ndio?” Doreen aliongea sasa akiwa anaweka sawa kifaa chake cha mawasiliano
“iko hivi, mwaka mmoja kabla ya baba yetu kuwa raisi alikuja siku hiyo tukiwa tunaishi kule mikocheni alitueleza wazi wazi kuwa anatarajia kuwa Raisi na akataka tumuunge mkono, na kama mjuavyo uraisi sio wa mtu ni wa nchi, uraisi ni taasisi na ndio maana tulikubali kuvumilia hayo yote mpaka wakati huu” alisema Doreen huku sasa waandishi wakimsikiliza kwa makini
“mnadhani tungejitokeza hadharani kipindi Raisi akiwa madarakani kitu gani kingetokea? Nadhani wote mnafahamu!” alisema Sele akikazia
“sasa lengo lenu ni nini katika hili?” aliuliza mtangazaji mmoja
“sisi tunaeleza ukweli na yale tunayoyajua na kutokana na sababu tulizoshauriana na wanasheria wetu hatuwezi kuweka hapa ushahidi ila tunao kwamba mama yetu, dokta James, faith na mr Alex hawakufariki katika ajali ya moto bali waliuwawa kwa kupigwa risasi” alisema Sele

“taarifa ilisema kwamba wewe ambaye sasa Unajiita Sele ni kwamba ulifariki katika ajali ile ya moto, na kaburi lako lipo! Unataka kusemaje?”
“waliofanya hayo mauaji wanajua kwanini sababu ya kufanya hivyo na mimi ndie GIFT LUKAS TUPPA” angalieni hata sura yangu na baba! Lakini upo ushahidi mwingi sana, zaidi sana sifanyi haya kwasababu ya kuhitaji mali, nyie mnafahamu kampuni yangu inaingiza kiasi gani na taarifa hizi zipo wazi, kwasasa hata mtoto bado sina niko na mke wangu tu hapa, kwahiyo sina njaa ya kufanya nimchafue mheshimiwa Raisi” alisema Sele huku akimuaga dada yake huyo ambaye alirudi kulala, ilikua ni usiku wa manane kwa muda wa kule Italia
Baada ya maswali mengi Gift alirudi nyumbani kwake akiwa na mke wake sasa kusubiri kitakachojiri baada ya hapo , sasa Nchi nzima ilisimama kwani tayari habari zilikua zimesambaa kila kona ya nchi kama moto

“Lukas nilikuambia hawa watoto wako wa mtaani watakuja kukuvua nguo, ona sasa, angalia sasa huwezi kutoa sura yako nje, nilishakuambia umalaya utakuponza angalia sasa!” alisema mama Joan akimfokea mzee Tuppa
“sikiliza hili jambo tulishaliongea na kila mmoja ataubeba msalaba wake mwenyewe!” alisema mzee Tuppa akiingia ndani kwake akiwaza namna ya kufanya
Tangu juzi alipomsikia na kumuona kijana wake Gift alikumbuka zile nyakati alipokuwa anamtembela mama Doreen kule mikocheni, hakika mama Doreen alikua mwanamke aliyempenda sana , ama tuseme walipendana, alienda kwenye kabati na kutoa apicha yake na kuingalia tena huku akilia
“nisamehe mama Doreen nilishindwa kukulinda” alisema huku mikono yake ikitetemeka na machozi yakimtoka
hakua na jinsi alimuita mlinzi wake Joshua na kumtaka akamuite mzee Lwakare huyu alikua ni Rafiki yake lakini pia alikuwa ndie mshauri wake hususani katika mambo magumu yaliyokuwa yanamtatiza kama hilo huyu alikua ni jaji mstaafu na kwasababu ya kazi yake na ukaribu wake angeweza kumsaidia katika suala hili
hakuwa akiishi nae mbali sana na hivyo alifika alifika baada ya muda mfupi na kuingia ndani ya nyumba, mzee Lwakare aliyafahamu hata mahusiano ya mzee Tuppa na mama Doreen hata kabla ya hapo hivyo alijua nini haswa anatakiwa kumshauri rafiki yake huyo!
********************************
Sele alikuwa amejituliza nyumbani kwake tayari alikua ameshachukua likizo fupi kazini kwake ili amalizane na jambo hili kwakuwa tayari suala hili lilikuwa la muda mrefu, ilikua yapata majira ya saa tano asubuhi wakati simu yake ya mkononi ilipoita,
“kaka kama uko karibu na Tv angalia weupe tv” ilikua ni sauti ya Jose
Haraka Sele alikimbilia sebuleni na kuwasha Tv,
“kwahiyo sisi kama Polisi tumeanza uchunguzi wetu rasmi kuhusiana na suala hili na kama tulivyowaambia mzee Tupa, mzee wetu yuko tayari kabisa kutoa ushirikiano wote ambao utahitajika, kwasababu kumbukeni kazi yetu sisi polisi ni kudeal na uhalifu haiwezekani mtu atoke hadharani kuwa mama yake aliuwawa kwa kupigwa risasi halafu sisi kama polisi tunakaa kimya” Inspekta wa polisi ndugu Yakobo sasa alikua anaongea na kisha akakaribisha maswali kutoka kwa waandishi wa habari
“Suala hili mnalipa uzito gani na pengine mnataka kufanya jambo gani haswa?” mwandishi mmoja alikua anauliza
“kama nilivyosema suala hili tumelipa uzito wote na kama unavyoona nimekuja mimi mwenyewe kulitangaza kuonyesha kuwa ni suala nyeti na polisi hatuwezi kusema tunafanya mambo gani, lakini niseme hata sasa tuko kazini na siku si nyingi kila kitu kitakuwa wazi kabisa’ alihitimisha inspekta wa Polisi
“huu ni ujinga, mtaanzia wapi sasa!” alijisemea Sele akizima Tv, baada ya masaa mawili kengele ya mlangoni iliashiria ugeni, Sele alienda kwenye mfumo wake kutazama wageni aliona gari jeupe aina ya Toyota hillux ikiwa imesimama nje ya nyumba yake na mtu mmoja aliyekua nje getini.
Alitoka nje na kuangalia ambapo waliingiza gari ndani na kisha wakashuka watu wawili huku dereva akibakia kwenye gari Sele aliwakaribisha ndani sebuleni.
“mimi ni afande Michael, na huyu ni Afande Claude” jamaa mmoja alisema huku wakitoa vitambulisho vyao
‘ndio karibuni sana” alisema sele akikaa vizuri kwenye sofa yake
“sisi tumekuja nadhani kama ulikua ukiangalia ile press ya mheshimiwa Yakobo utaona kwamba tumekuja kwa jambo hili’ alisema Michael
“Ndio nawasikiliza” alisema Sele
“sisi tunaomba ushirikiano wako ,kwanza utupe taarifa zote ambazo wewe unazo na baadae itakuwa kazi yetu sisi polisi kumalizia suala lililobaki” alisema Michael
“okay tunaweza kufanya hivyo hakuna shida” alisema Sele huku akiwa anawatilia shaka wale watu pengine walikua ni polisi kweli lakini kutokana na masaibu yaliyomkuta hakutaka kuamini mtu yoyote hivyo aliwataka radhi na kisha akatoa simu yake
“sawa lakini kwanza inabidi niwasiliane na mwanasheria wangu ili nikitoa maelezo nae awepo” alisema Sele huku wale jamaa wakitazamana
“ah ni sawa tu lakini sasa huoni tutachelewa sana Bwana Sele?” alisema Michael
“hakuna shida atafika ndani ya saa moja” alisema Sele
“sasa tufanye hivi twende kituoni ili tukafanyie mahojiano kule ili kuokoka muda kwahiyo tutampigia sehemu tutakayokuwa”
“sehemu tutakayokuwa? Ina maana hamjui tunapoenda?” sele aliuliza
“unajua Sele suala hili ni siri na ndio maana umeona hata Uniform hatujavaa hivyo twende tu utajua hapo baadae” alisema Yule jamaa mwingine
“okay nipeni dakika kadhaa” alisema Sele huku akitoka na kwenda chumbani na kisha akabadili nguo na kisha akamuaga Esta kuwa anakwenda kituo cha polisi mara moja kuna maelezo anaenda kutoa, Esta alimtaka kuwa makini na watu hao kwani bado walikuwa hawajatimiza lengo lao,
Sele alitoka kisha akafuatana na wale jamaa na kuingia kwenye Gari,mtu mmoja alitangulia kwenye Gari kisha na yeye Sele alifuata na mwingine akaingia na sasa Sele alikua katikati ya wale jamaa wawili mwanzoni wakatia anaingia alidhani ilikuwa imetokea bahati mbaya tu, lakini baadae alikuja kugundua hii imefanyika makusudi kabisa na wakati anajiweka sawa tayari Yule jamaa aliyejiita Michael akatoa bastola na kumuwekea kichwani
“lete simu zako zote” alisema sasa
“unafanya makosa sana jamaa”, alisema Sele huku akitoa simu zake na kuwakabidhi sasa safari ya kuelekea kusikojulikana ikaanza huku wale jamaa wakiwa kimya na hatimaye wakafika barabara kuu ya kuelekea Kawe, Michael akatoa kitambaa cheusi na kumpa Sele ajifunge usoni
Sele alitii na kukiweka kitambaa kile usoni, na sasa hakuweza kujua uelekeo wa gari zaidi ya kuhisi tu, na hatimaye alihisi gari ikiingia kwenye jengo moja hivi na kisha akavuliwa kitambaa na kuachwa atembee mwenyewe, tayari walikua kwenye sehemu ya kupaki magari katika jengo moja hivi
 
MPANGAJI 16

By CK Allan
Jengo lilionekana kama lipo chini ya ardhi hivi na Sele aliangaza huku na huku ili kuweza angalau kuhisi kama alishawahi kuwepo kwenye jengo lile kabla, akili zake sasa zilikiri kabisa kuwa ile iikuwa ni mara ya kwanza kwa yeye kuwepo katika jengo lile walishuka ngazi kuelekea chini zaidi na kutokea kwenye eneo moja hivi kama ukumbi na kisha wakasimama hapo huku Sele akionyeshwa chumba cha kuingia na wale jamaa wakasimama nje Sele alisogea na kuvuta kitasa cha mlango na kuingia ndani, kwa sekunde kadhaa hivi alisimama akiduwaa baada ya kuona sura iliyokuwa mbele yake, hakuamini lakini ilikuwa ni kweli,
Ndio, baba yake mzee Lukas Tuppa alikuwa amesimama mbele yake wakitazamana macho kwa macho! Hatimaye baada ya sekunde chache, mzee Lukas sasa alishindwa kujizuia na kuanza kutoa machozi kisha akamsogelea na kumkumbatia
“I’m so sory Gift, I’m so sory!” alisema mr Lukas sasa akiwa amemkumbatia mwanae huyo, gift nae alijikuta machozi yakimtiririka na kuna namna Fulani alijikuta hasira alizokuwa nazo zikiyeyuka,
Baada ya muda kidogo Gift alikaa kwenye kiti na mzee Tuppa nae akakaa kwenye kiti kingine kisha akaanza hotuba yake fupi
‘najua sina haki yoyote katika hili lakini naomba sana unisikilize Gift, kipindi kile ulikua mdogo sana, nisingeweza kukuambia kila kitu, but only God knows jinsi nilivyoishi kwa kipindi chote hiki bila uwepo wenu’ alianza mzee Lukas sasa hotuba yake huku akimuangalia Gift ambaye alikua ameinama tu huku mikono ikiwa kwenye mashavu
“but why, kwanini lakini baba? Kwanini?” alisema Gift
“nilijitahidi sana kuwa na ninyi lakini mama yako mkubwa alizuia jitihada zangu zote, najua wewe ni smart, unajua mambo mengi na katika hili naomba ujue kuwa vyovyote ilivyo sikuagiza na wala sihusiki na kifo cha mama yako!” alisema Mzee Lukas
“kwanini umenileta hapa?” aliuliza Gift sasa akisimama
“nimekuita hapa kukueleza jambo moja tu kuwa, nipo pamoja na wewe katika kila hatua utakayoamua kuchukua mwanangu, sijui itakavyokuwa na itatokea nini lakini naamini jambo hili litakuwa na mwisho mzuri, je unapanga kufanya nini?” aliuliza mzee Lukas
“hata mimi sijui nitafanya nini ila naamini nitafanya jambo!’ alisema Gift
“sikiliza Gift, aliyemuua mama Yako ana mkono mrefu sana na vita hii haitakuwa Rahisi kwako ingawa nakutakia kila la kheri!” alisema mzee Lukas akimkumbatia tena mwanae huyo
“nitahakikisha unashinda katika hili Gift” alisema mzee Tuppa, Gift alitoka nje na wale jamaa bila kuuliza walitoka na kutoka nae mpaka nje ya jengo kisha wakamfunga tena kile kitambaa na kuingia kwenye gari baada ya mwendo kama wa dakika kumi hivi walimtoa tena kile kitambaa na kumrudishia simu zake kisha wakamuacha maeneo ya Tazara njia panda,
Gift alisimama barabarani na kisha akawasha simu zake na kusoma jumbe mbali mbali pamoja na kuangalia waliomtafuta katika masaa hayo kadhaa ambayo hakuwa hewani
Ni sekunde chache tu tayari simu yake ilionyesha ishara ya jumbe kuingia, alisoma zote haraka haraka huku sasa akiwa katika hali ya tahadhari kwanza alikuta taarifa kuwa mke wake alikua amempigia lakini jambo ujumbe mmoja ni ule uliomshangaza kuwa kuna mtu anajaribu kufungua mlango wake nyumbani kwake!
“haiwezekani! Haiwezekani!” alisema sasa akijaribu kumpigia Esta ,
Hakupatikana! Alijaribu zaidi ya mara mbili na tayari alijihakikishia kuwa hakupatikana!
Sasa alichanganyikiwa akipungia mkono boda boda iliyokuwa mbele yake..
‘twende haraka,!” alisema

Gift alifika nyumbani na kukuta geti lake liko wazi, haraka sana alijitosa ndani huku akiita jina la mke wake, ni sasa aligundua bado mtu wa boda boda alikua anampigia honi nje kuashiria malipo yake, aliingia ndani na kutoa elfu 10 na kumpa huku akirudi ndani haraka, aliingia kwenye chumba chake cha ulinzi na kuanza kuangalia matio yaliyopita,
Kumbe wakati wakiwa wanatoka na akina Michael gari nyingine iliingia muda mfupi na walionekana na alishuka mwanamke mmoja na mwanaume kisha waliingia ndani na Esta alionekana kwenda kufungua geti waliongea kidogo huku Esta akiwakaribisha ndani ambapo baada ya muda aliingia Yule mwanamke pekee huku Yule mwingine akiangalia huku na huko bila shaka alihisi kulikua na kamera eneo hilo baada ya dakika kadhaa Esta alionekana akitoka na Yule mwanamke kisha akarudi mlangoni na kuufunga na kupiga hatua moja kisha wakaingia kwenye gari, hakukua na purukushani yoyote, na kisha wakaingia kwenye gari na kuondoka
“inamaana hajatekwa?” aliwaza Sele
“lakini hawa ni akina nani?” alisema huku akirudisha nyuma kipande cha video wakati Esta anafunga mlango aliangalia kwa muda kidogo kisha akatoa simu yake alikagua ule muda ambao alitumiwa ujumbe mfupi kuwa kuna mtu anajaribu kufungua mlango wa nyumba yake akaona ni muda ule ule wakati Esta anafunga mlango!
Haraka wazo likamjia Esta alifanya makusudi kukosea zile password ili sele apate ujumbe huo vile vile alijua kabisa wale jamaa walikuwa wanajua wanaonekana kwenye kamerza za ulinzi ndio maana wakafanya waliyoyafanya “kumteka Esta Kistaarabu’ aliwaza sasa Sele akienda kwenye kabati lake na kutoa bastola yake na kuiweka kiunoni kisha akatoka nje na kuingia kwenye gari lake na kuliwasha hakufika mbali sana simu yake ikaita na haraka aliichukua na kuiweka sauti kubwa
“hello Gift tuko na mke wako hapa, naamini unataka kumuona akiwa hai tena” sauti ya upande wa pili ilisikika
“nyie ni akina nani, na kwanini mmemteka mke wangu?’ Gift aliuliza akiwa amehamaki
“wewe fuata maelekezo yetu tu na mke wako atakuwa salama” ile sauti ya kiume upande wa pili ilisikika
Haya semeni mnataka nini!” alisema sasa Gift huku akipunguza mwendo wa gari
“njoo hapa makumbusho kuna baa inaitwa TULIP iko pembeni ya kituo cha kuuza mafuta ukifika hapo ingia kama unataka kuweka mafuta hapo sisi utakuta mtu anakusubiri hapo atakuelekeza cha kufanya”
Gift hakujibu aliindoka kwa mwendo wa haraka kama alikua anacheza sinema vile na baada ya dakika arobaini tu alikua makumbusho akauliza ilipo baa ya TULIP na baada ya muda mfupi alikuwa kwenye kituo cha mafuta alisogeza gari kana kwamba anataka kujaza mafuta wakati akiwa anashangaa shangaa alisikia kioo cha gari yake kikiwa kinagongwa ikabidi ashushe vioo na kumuangalia, Yule mtu alitoa simu yake na kubonyeza bonyeza kisha akamuonyesha Gift ambaye haraka alifungua gair na kutoka, niambie yuko wapi, alisema Sele sasa akimshika shati Yule jamaa
“ahaaa toa mkono wako jamaa” alisema Yule jamaa kwa dharau
“rudi kwenye gari” alisema sasa akiuondoa mkono wa sele
Sele hakuwa na namna isipokuwa kurudi kwenye gari na kuingia ndani Yule jamaa nae aliingia kisha akavuta mkanda wake kuuweka vizuri
“twende” alisema
“wapi sasa mbona kama unanizingua wewe jamaa!” Sele alisema akiwa amekasirika
‘nyosha hapo kwenye huo uzio kama unaenda Bar halfu nitakuelekeza” alisema na sele akatii na kisha wakapita kwenye uzio mmoja hivi baada ya ile bar na kutokea kwenye geti moja jeusi hivi na Yule jamaa akabonyeza Honi mara mbili na gei likafunguliwa
“Karibu sana bwana Gift naomba acha kila kitu chako kwenye gari” alisema Yule jamaa akiwa sasa anashuka kwenye gari
“sikiliza, ujinga wako mmoja tu utasababisha mke wako auwawe , unatakiwa utembee bila kuonyesha mashaka kabisa wakati tukiingia kwenye iyo nyumba” Yule jamaa alisema
Sele sasa aligundua hawa jamaa kuna kitu kingine cha ziada wanapanga maana alikumbuka kule kwenye kamera za usalama nyumbani kwake Esta nae alikua anatembea kawaida kutoka pale nyumbani kwake!
“ngoja tuone huu mwisho wa huu mchezo” aliwaza akitoa bastola yake na simu zake na kuacha ndani ya gari kisha akashuka nje ya gari na kumfuata Yule jamaa kuingia ndani ilikua ni sebule nzuri yeny samani za kisasa baada ya dakika kadhaa walitokea watu watatu mmojawapo akiwa mzee hivi ambaye sura yake haikuwa ngeni sana na Sele alimtambua mara mmoja alikua mgombea wa Uraisi kwa tiketi ya upinzani katika uchaguzi uliopita kupitia chama cha TAI bwana Yahaya Kidude alikua akionyesha tabasamu na Sele hakujali aliuliza tu alipo mke wake
 
Shukraaan
 
Wakuu baada ya huu mzigo kwisha nitatulia kidogo mpaka wakati mwingine
Shusha tu mkuu Kuna amesema anajisikia upweke sijui upweke utatoka wapi kwa vigongo kama hivi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…