Hadithi nahadithia leo

hata kama ni hadithi mi nimeshindwa kuona usuhiano kati ya ugonjwa wa mumewe na uhusiano wake na HG

Yaani hilo la kufumania limeingia 'kwa gafla' sana...ukianza kusoma unaona kuwa jamaa anaumwa na mkewe ana sympathy kabisa...

Ina maana, kuumwa kwake kulikuwa feki muda wote huo, I mean hata dawa alikuwa anatupa hamezi au alikuwa anahonga hospitali aonekane anaumwa? Na iweje katika hali ya kawaida ampigie simu mkewe aje nyumbani eti anaumwa huku akijua ako na HG?

Au huenda kweli 'anaumwa' na amekata tamaa na kuwa desparate 'lolote na liwe'? Kha!
 
hii hadithi ni ya kutunga na si ya kweli kabisa, hapo kwenye "red" inaonyesha kuwa ulianza na story ukitafuta muunganiko ili mwisho ulete radha kwa hadhira ila umekosea sana kuleta story ambayo inakinzana kimaana na mwisho wa hadithi, kuumwa homa, malaria, tumbo na kuhara wala havihusiani na kutembea na h/girl,

Issue ya kuumwa na kukwambia umchukulie dawa na kukukuta umelala fofofo na h/girl pia haiingii akilini kwa great thinker funzadume

Kwenye "blue" ndio utata sana unasema uligonga geti mpaka ukachoka bila kupata response na kumwita kijana aje kufungua hapo kuna utata kwani ukigonga sana geti watu kama wako ndani wanachinja kobe lazima wajistukie na kuchukua taadhari (hii nimeongea kutokana na uzoefu mbalimbali) pia unasema ulipoingia ulikuwa na wasiwasi uenda mme wako amezidiwa ila pamoja na wasiwasi wako badala ya kuanzia chumbani kwenu ukaenda kwa house girl, kisha kwa watoto na mwisho ndio ukaenda kwako hii haiingii akilini kabisa maana ulitakiwa kwenda straight chumbani kwenu kujua mmeo anaendeleaje na sio kupitia kote huko as if ulikuwa umejiandaa kufumania

Kingine kwenye "blue" ni issue ya kuingia chumbani na kukuta wamelala fofofo mpka ukawaona na kuamua kutoka kwenda kuita jirani aje kushuhudia wakati huo bado tu wamelala fofofo hiyo kwa kweli aiingii akilini hata siku moja

UJUMBE kwa mwandishi:
Kutunga story ni kipaji tena cha kuzaliwa na kusomea pia usione kina Shigongo wanatunga hadithi ukadhani ni kitu rahisi tu, kile ni kipaji tena unatakiwa uwe genius kuweza kuuteka moyo wa msomaji kwa kupangilia story toka mwanzo mpk mwisho kwa umakini uliotukuka
 


sasa hiyo ndo great thinking walau umeeenda kwan detail zaid mi nimescan nikashindwa kuconnect dots kiongozi

Vipi mpango mzima wa upaja bado ile aleji haijarudi?
 
sasa hiyo ndo great thinking walau umeeenda kwan detail zaid mi nimescan nikashindwa kuconnect dots kiongozi

Vipi mpango mzima wa upaja bado ile aleji haijarudi?

Hommie.......Mombo hapa. Naelekea kule:hungry:
 
sasa hiyo ndo great thinking walau umeeenda kwan detail zaid mi nimescan nikashindwa kuconnect dots kiongozi

Vipi mpango mzima wa upaja bado ile aleji haijarudi?
ile pajaz nimeona niipotezee maana kila jioni mme wako anamfuata job, halafu nilisha kula kiapo kuwa mke wa mtu ni sumu
 

hata wanawake sio wakuaminika may be 1 kati ya 20
 


Funza dume hiyo ni kucut story short, ningeeleza kila details hapa ingekuwa hadithi ndefu sana.

To make things clear, mara nyingi akinituma dawa nitakuja nazo kama kawaida wakati nikitoka kazini, alielewa vizuri sana. Na hii ni kwa sababu huwa nashangaa kwa nini anapokwenda hospitali asichukue dawa huko huko ilhali anatibiwa kwa insurance? Nikadhani ananitega kutest upend wangu kwake, nikasema kama mbwai mbwai, acha ninunue dawa.

Amini usiamini, kuwa niliwakuta wamelala fofofo, niligonga geti na simu zao ziliita-sina hakika kama walizisikia wakachuna au walitopea usingizini baada ya shughuli nzito.

Niliamua kuita mtu wa kushuhudia, sina hakika kama ilikuwa busara au nguvu ilitoka wapi. Hata hivyo sio kama nilitoka kwenda nyumba ya jirani kugonga hodi waje washuhudie, hapana. Jirani alikuwepo hapo nje ya gaei baada ya kugonga sana, ndiye niliyemtumia kijana wake kupanda ukuta na kunisaidia kufungua geti kwa ndani. Kumbuka baada ya kugonga sana, kuona gari ya mume wangu ndani, na msichana wa kazi haonekani, simu zao hazipokelewi, niliingiwa na hofu kubwa pengine mwenzangu kazidiwa na kukimbizwa hospitali au hata kupoteza maisha kabisa. Hivyo jiraji yangu na yule kijana walikuwepo kujua nini kinaendelea japo ndani ya nyumba niliingia mwenyewe.

Kiufupi, hii ilukuwa 40 ya mwizi, Mungu alitaka kunionyesha hali halisi au alitaka kumuumbua yeye.

Hivyo basi ndugu Funza, hii story ni ya kweli, take it or leave it. Labda sina kipaji cha kuelezea kila kitu, lakini kiufupi yalitokea, nimefumania laivu mume wangu na msichana wangu wa kazi wamelala fofofo kitadani kwangu.
 


Uhusiano ni kwamba, huyu bwana alikuwa akijisingizia ugonjwa ili awe na justification ya kuwa nyumbani wakati ambapo anatakiwa awe sehemu nyingine anajenga taifa na kutafuta kwa ajili ya familia. Ni kwamba alionja tunda la beki 3 akanogewa. Sitaki kuongelea beki 3 alivyokuwa akimiss behave hapo nyumbani, nilivumilia tu kwa vile nilikuwa na mhitaji na pia nilijua watu wana tabia tofauti kutokana na makuzi, na matatizo yanayowakuta maishani. Hivyo basi nilimchukulia ndivyo alivyo.

Hakuna kuwa desparate, nilitimiza wajibu wangu kama mke hapo nyumbani, kwa 100%. Kumjali, kumpenda, kumrespect nk. . Hataki kutoka nyumbani, yeye ni kazini na nyumbani, kwenye misiba, harusi, na other social activities hata zinazoihusu familia yake ama yangu, achia mbali za marafiki, hakutaka kwenda. Any way, nilidhani ni kwa mazuri.
 

Ahaa.....sasa hapo kinachogomba ni presentation ya issue nzima, ulivoipresent kama hadithi, siye tumeichukulia kama hadithi na tumaangalia mapungufu yake kama hadithi...

Lakini inaonekana sasa hapa ni kama mkasa hivi ambao ungeuleta kama hapa, tungekushauri kivingine.....karibu
 
kama ni kweli nakupa pole sana naomba nikupe ushauri PM nn cha kufanya
 
Wanaume kwa kumsingizia shetani!!!!!
Kuna matendo mengine 2nafanya hata shetani anaiga toka kwetu inaonesha ni jinsi 2livo zaidi ya shetani!!
Pole saana

 
we hadithia bt hatutaki uongo hapo! Uongo usije, utamu ukolee!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…