Hadithi fupi!
SITOSAHAU ALICHONIFANYA DAKTARI WA SARATANI YA MATITI
UKURASA WA KUMI NA TATU
Kesho yake mcha muda wa saa saba, nikiwa ofisini kwangu alikuja yule mwanadada ambaye alikuwa amepanga pale kwa Hemed, ambaye nilikuwa nimemuona jana yake nikahisi kama nilishawahi kumuona mahali.
Yule dada aliingia ndani ya ofisi na kunichangamkia sana βHallo mambo mremboβ ndivyo alivyoniambia
βSafi tu dada karibuβ nilimuambia huku nikiinuka kwenye kiti nilichokuwa nimekalia
βAsanteβ¦..Nilihisi nimekufananisha jana, kumbe ni wewe kweliβ alisema dada
βHahhaβ¦mimi mwenyewe nahisi hii sura sio ngeni kwangu lakini hata mpaka sasa nashindwa kukumbuka vizuri, labda ulishawahi kuniungisha nguo si ndio?β nilimuuliza
βNdio shoga angu, kuna siku nilikuja hapa nikawa nimenunua nguo kadhaa nikiwa mimi na mwanangu mdogoβ
βHahaaβ¦.itakuwa kweli maana hii sura niko familiar nayo kabisa dada anguβ¦.karibu sanaβ
βAsanteβ
Yule dada alianza kukagua nguo pale dukani kwangu, lakini hakuona aliyoipenda hivyo akaamua kuniaga na kuniambia atarudi siku nyingine.
Akatembea hatua kadhaa na kugeuka akaniuliza βHivi unaitwa nani vile?β
βMi naitwa Pendoβ nilimjibu.
βOkay Pendoβ¦.sasa mimi naitwa mama Numraβ
βSawaβ nilisema huku nikimkagua ikabidi mimi naye nimpachike swali βHivi jana kwanini yule housegirl wa Hemed alikuwa analia et?β
Mama Numra alitabasamu halafu akaniambia βMdogo wanguβ¦.pale umeingia cha kike kabisaβ¦.yule mwanaume ana hatari, wanawake ni wengi sana,β¦.ila nashangaa kwanini amekupa thamani kubwa hadi kukuleta nyumbaniβ alisema yule mama na kuingia tena dukani, alionekana mbea sana
βMh kumbe ni Malaya yule?β niliuliza
βMhβ¦.sijajua kama kwako amebadilika lakini yule mwanaume amekuwa hatari, umesema Jacque alikuwa analia?β aliniuliza
βNdioβ
βMasikini mtoto wa watu anapitia mengi pale ndaniβ alisema mama Numra
βKivipi??β nilimuuliza
βNafikiri kilichomuuma Numra ni kwa sababu wewe ulifika pale nyumbani kiukweli wanatoka pamoja, ni kama mke wake tuβ
Haya maneno yalinishtua sana, kumbe Hemed alikuwa anatoka na dada wa kazi, ni kweli ni mzuri yule Jacqueline lakini si angeniambia tu kwamba yuko naye
Nilimtazama mama Numra na kusema βJamani anisamehe tu mimi sikujua chochote kumbe ni mtu wake?β nilisita kidogo na kuendelea βDuuh lakini kwanini anipeleke pale nyumbani wakati kuna mpenzi wake? Ah au alikuwa anataka kumkomoa au kunikomoa mimi?β
βNdio maana nikasema amekupa thamani kubwa sana, huwa ana wanawake wengi lakini kamwe hawaleti nyumbaniβ¦kwa sababu anatoka na yule msichanaβ
βDuuuhβ¦.nilihisi tu maana yule msichana ni mzuri sanaβ¦β¦.asingeweza kuvumilia Hemedβ
βHahaaβ¦ni kweli ni MashaAllah mtoto yuleβ¦sio mtanzaniaβ
βOhβ¦haya dadaβ¦..nashukuru sana kwa ujumbe wakoβ
βHaya mdogo wangu kwa heriβ alisema
βOkβ
Mama Numra aliondoka zake kuelekea nyumbani kwake lakini aliniacha katika mawazo makubwa sana, yule Hemed alionekana sio muaminifu hata kidogo. Alionekana ana wanawake wengi sana, nilishangaa kwa kujua kumbe yule msichana wa kazi alikuwa analia kisa aliniona mimi pale kwaoβ¦.maumivu yalikuwa sio ya nchi hii.
Nilikaa kimya, roho inaniuma, penzi halijafikisha hata juma, lakini limeanza kunichoma. Sikuwa na cha kufanya zaidi ya kuamua kuachana na Hemed kabisa, ndiyo yalionekana maamuzi sahihi kwenye maisha yangu.
Niliendelea na kazi yangu mpaka ilipofika muda wa saa kumi na moja ndipo Hemed aliponipigia simu, sikusita, niliipokea na kuongea
βHalloβ nilisema
βNiambie Pendo, mzima wewe?β aliniuliza
βMzimaβ nilijibu kwa mkato kidogo
βMbona umekuwa kimya sana mke wangu?β aliniuliza
βHamnaβ nilijibu
βSawa sawa, jana ulifika salama lakini?β aliniuliza
βNdio lakini nikuulize swali tu, kwanini yule househelp wako alikuwa analia kiasi kile?β hamna
βHahahaβ¦.nilijua tu hilo swali litafuata, anyway yule anadeka sana anasema amemmiss mama yake anataka kwenda kwaoβ
βMhβ¦.ndo alie hivyo?β niliuliza
βYaahβ¦ni mtu wa tofauti kidogoβ
βDuh hayaβ nilisema
Nilikuwa na wasiwasi na Hemed , hata yale mapenzi niliyokuwa nimeanza nayo ya moto sana yalikuwa yameshashuka kwa kiasi kikubwa, nikaona ni kheri nikatafuta namna nyingine ya kuishi bila yeye, niliona ni bora kumkaushia.
Hemed alikata simu kisha akanitumia SMS βusiwe na wasiwasi, penzi lako liko salama, naomba unijibu lile suala la kukuoa mpenziβ
Niliisoma ile SMS mara mbilimbili lakini kamwe sikupata jibu lenye faida, niliishia tu kumjibu hivi βKwa jinsi nilivyoona wadada wanavyokusumbua huko njiani, na mambo mengine ambayo sitaki kuyaandika hapa, naomba suala la mapenzi yangu mimi na wewe liishie hapaβ
Kiukweli nilikuwa natamani kuwa na mwanaume wangu lakini yule hakuwa wangu, niliona ni wetu ndio maana niliamua kumkaushia ili nikae kwa amani moyoni mwangu.
Hemed hakunijibu ule ujumbe alikausha kimya mpaka saa nne usiku ndipo alinitumia ujumbe uliokuwa unasema hivi
βNAJUA UNANIHISI VIBAYA KWA SABABU JANA ULIONA NINA MAZOEA NA BAADHI YA WANAWAKE BARABARANI. KIUKWELI SIO KWAMBA NAWATUMIA LAKINI NIKUAMBIE TU KWAMBA NINAHITAJI UWE MKE WANGU NINAAHIDI KUKUPA FURAHAβ¦NAOMBA ULIFIKIRIE HILI UNIJIBU KESHO ILI NIAHIRISHE NDOA AMBAYO NINATAKIWA KUFUNGA NA MAMA NASRAβ
Nilishangaa kwanini anangβangβana tuoane? Yaani hata hatujachunguzana yeye anataka akaniue na presha tu? Nilimjibu
βLALA HUKO, MIMI SINA RATIBA YA KUOLEWA NA WEWEβ¦..ENDELEA NA JACQUE SITAKI KESI NA MTOTO WA MTUββ¦β¦β¦β¦β¦β¦β¦ITAENDELEA
Hadithi fupi!
SITOSAHAU ALICHONIFANYA DAKTARI WA SARATANI YA MATITI
SEHEMU YA KUMI NA NNE
TULIPOISHIA
Hemed hakunijibu ule ujumbe alikausha kimya mpaka saa nne usiku ndipo alinitumia ujumbe uliokuwa unasema hivi
βNAJUA UNANIHISI VIBAYA KWA SABABU JANA ULIONA NINA MAZOEA NA BAADHI YA WANAWAKE KADHAA BARABARANI. KIUKWELI SIO KWAMBA NAWATUMIA LAKINI NIKUAMBIE TU KWAMBA NINAHITAJI UWE MKE WANGU NINAAHIDI KUKUPA FURAHAβ¦NAOMBA ULIFIKIRIE HILI UNIJIBU KESHO NILI NIAHIRISHE NDOA AMBAYO NINATAKIWA KUFUNGA NA MAMA NASRAβ
Nilishangaa kwanini anangβangβana tuoane? Yaani hata hatujachunguzana yeye anataka akaniue na presha tu? Nilimjibu
βLALA HUKO, MIMI SINA RATIBA YA KUOLEWA NA WEWEβ¦..ENDELEA NA JACQUE SITAKI KESI NA MTOTO WA MTUββ¦β¦β¦β¦β¦β¦β¦
ENDELEA
βJacque????β aliniuliza kwa mshangao kidogo
βNdio, ulifikiri mimi sifahamu?β
βHahaahβ¦.acha mambo yakoβ aliniambia
βMambo gani Hemed? Mimi nimeshaambiwa kila kitu, kumbe ndio maana mtoto wa watu alikuwa analiaβ nilisema
βWaliokuambia hivyo wamekudanganya, mimi sina mahusiano na binti yangu wa kazi jamaniβ
βHahahaa eti eeβ niliuliza
βNdio, kwanini unakuwa hivi Pendo? Hivi kweli wewe utaolewa??β
βNi kheri nisiolewe kuliko kuolewa nikaenda kuzeeka kabla ya muda wanguβ
βHaya poaβ
Tuliachana kirahisi rahisi tu namna ile, lakini vile haikupita siku mbili, nilikuwa nimekaa zangu kazini kwangu naweka midoli ya nguo nje ya ofisi yangu, ndipo akapita yule msichana ambaye pia ni mpangaji wa pale kwa Hemed, alipoona nguo alisogea karibu na mdoli mmoja na kunichangamkia
βJamani mamboβ
βSafiβ¦..karibuβ nilisema huku nikimtazama
βMmhβ¦.nimeona hili gauni jekundu ni zuri nikasema nije hata niulizie beiβ
βHahahβ¦karibu ni shilingi elfu ishirini na nane tuβ
βMmmmhβ¦ni zuri lakini beii mmmhβ
βMh sio pesa nyingi jamaniβ
βhahaaβ¦.nikikupa ishirini hautanipatia shogaa??β aliniuliza
βHapana mama,β¦.ishirini mbali sana. Labda ishirini na tano jamaniβ
βDaaahβ alisema huku akiligusa, mara ghafla nilimuona Jacque akiwa anakatiza barabarani. Ndipo akamuita βWe Jacqueeeeβ¦.Jacqueeβ binti Jacque akageuka kwa mshangao, nadhani moyoni alikuwa anajiuliza ni nani anamuita.
Alipomuona yule msichana mwingine, alichangamka na kumnyooshea kidole akicheka βHalafu weweβ alisema Jacque huku akivuka barabara na kuja kwenye upande wa duka langu
βUmetoka wapi??β yule msichana mwingine aliuliza
βNimetoka kwa bwana anguβ alisema huku akicheka mimi nikawa namuangalia kwa kifupi moyoni ni kama nilikuwa adui yake, alishaninyima tunda langu kwa Hemed lakini sikuwa na namna maana yeye ndiye aliyetangulia.
βKumbe una bwana huku?β aliuliza yule msichana mwingine ambaye baadaye niligundua anaitwa Farida
βHahahaβ¦hapana bana, kuna sehemu kaka aliniagiza nimepeleka helaβ alisema Jacque na kuniangalia.
Sasa ghafla yule binti akanitazama na kushtuka kidogo halafu akasema βShikamoo dadaβ
Nilitabasamu kisha nikaitika βMarahaba mdogo wangu, mbona umeshtuka uliponiona?β
Jacque akatabasamu kwa aibu kisha akaniambia βSikujua ni weweβ
βMh haya bwanaβ nilisema
Waliendelea kuangalia nguo wakawa wanazisifa ila hawakununua
FARIDA: Basi nisindikize sokoni tutarudi wote shogaa
JACQUE: Mhβ¦mbali kote kule na jua hili? Unataka niwe mweusi (akiwa anachezea nywele zake ndefu)
FARIDA: Mh twende bwana huwezi ukawa mweusi
JACQUE: Haya
FARIDA: (Huku akinigeukia) Kwa heri tutarudi siku moja kununua bwana
MIMI: Sawa karibuni jamani
JACQUE: Kwa heri dada
MIMI: Okay
Jacque na Farida waliondoka kwenda zao lakini hakufika mbali nikaamua kumuita Jacque ili niweze kumaliza tofauti zetu.
Jacque aligeuka na kunitazama kisha akaniuliza βMimi?β nikasema
βNdio weweβ¦.. nakuomba mara mojaβ nilisema
βMhβ Jacque aliguna na kunisogelea lakini akamuacha farida akiwa anamsubiri mbali kidogo na pale, Jacque akanisogelea kisha nikamuambia
βSamahani kipenzi, mimi naamini unanikumbuka nilikuja pale kwenu siku mbili zilizopitaβ
βNdio nakukumbuka dadaβ
βOkay, nilikuja kusikia kwamba nilikukwaza, kwani nilikuacha ukilia pale ndani sikujua kwamba chanzo ni mimiβ
βMhβ alisema huku akinishangaa kidogo yule msichana mdogo na mzuri sana βsijakuelewa dadaβ aliniambia
βYaani ninamaanisha kwamba Hemed hakuniambia kwamba yuko na wewe kimapenzi ndio maana nilikuja pale, mimi sikujua ana mpenzi mwingine maana hakuniambia, naomba unisamehe nimeamua kuachana naye ili niwaache na mapenzi yenuβ nilisema
βMh mimi??β aliniuliza tena kwa mshangao
βNdioβ¦.nimeambiwa wewe ni mpenzi wake, ndio maana siku ile nilipokuja ukaanza kulia nakuomba unisamehe mdogo wanguβ
βHahahaaaβ¦bhaanaβ alisema yule binti kwa mshangao kidogo βMimi mbona sina mahusiano yoyote na boss wanguβ alisema
βKivipi J??β nilimuuliza
βNinashangaa habari ulizoniletea, najua wewe ni mpenzi wakeβ¦mi sipo naye kimapenzi mbona, mh nitamuweza kweli mtu mzima kama yule mimi nina miaka 18 tuβ aliniambia nikamshangaa kwanza nikaguna halafu nikashika kiuno
Nikamuuliza βsasa siku ile kwanini ulikuwa unalia?β
βAhahahaaβ¦.kwa hiyo ulidhani nalia kwa sababu ya wivu??β aliniuliza
βNdio, hasa nilipokuja kuambiwa anatoka na wewe, basi nilijua kabisa ndiyo sababu iliyokupelekea kulia siku ileβ
βHapana dada yanguβ¦.nina matatizo yangu binafsi tu yalipelekea mimi kulia siku ile ninaumia sanaβ
βTatizo nini?β
βNina miaka minne tangu nije hapa Tanzania nimefanya kazi na hii familia kwa utiifu mkubwa, lakini hawajawahi kunilipa pesa, kiukweli nakula vizuri navaa vizuri lakini hata nyumbani sijawahi kuwatumia chochote, ninadai zaidi ya milioni sita za mshahara lakini pia nilitamani wanipe hata hela kidogo mwishoni mwa mwaka huu niende nikamuone mama anaumwa, ila wao hawaonyeshi kunijali, nimepamiss kwetu sanaβ
βMhβ¦kweli??β nilimuuliza
βNdioβ
βOh pole sana my dearβ¦.β
βAsanteβ alisema βKwa hiyo wewe usiwe na wasiwasi kwamba mimi natoka naye hapana, sina hata ratiba hiyo mimi ya kuwa naye usijaliβ¦.β Aliniambia
JE NI KWELI BINTI HANA MAHUSIANO NA HEMEDI??