Hadithi ya bwana mtaro mchafu

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
Wakiwa mtaroni, walimwambia bwana wa mtaro,
Mtaroni ni pachafu
Tuwezeshe tuiondoe harufu

Baba wa mtaro, kwa sauti ya ukali huku akipandwa na mori wa kikwere akang'aka,
Uwezo sina
Msitake kunipima

Wakiwa na ushahidi na uhakika wa madai yao, wakamwambia bwana mkuu wa mtaro,
tunajua kuna reki
tupe tupigane jeki

Akiwa amejawa na jazba na akirusha vidole juu, tena akishabikiwa na sauti za wapambe na wengine waliojichokea na wenye nyuso zisizo na matumaini ya kesho, bwana mkuu wa mtaro akasema
Hilo haliwezekani
Kama hamtaki ondokeni

Halafu kwa hasira akaongeza,
Mwanitafuta lawama?
Nitaishusha zahama
Na yeye atayegoma
Atakiona kiama

Wana wa mtaro kwa unyonge lakini wakiwa na ujasiri mioyoni mwao wakaamua kupambana. Hawakutaka kupambana na bwana mkuu wa mtaro bali na unyonge wao. Ndiposa yule mmoja akitumia mbinu na akili zake akauparamia ukuta uliojenga ukingo wa mtaro na huku akisaidiwa na ujasiri wake, akajivuta mpaka nje.

Ndiposa aliyemo mtaroni akalia kilio hicho kilichosikiwa na LeBron akisema...

Si unaona hatuna pa kukanyaga?..
Kwetu katika dimbwi la uchafu na umasikini,
Tumaini letu ni mkono uliouelekeza kwetu,
Ukituacha wadogo zako tutafia mtaroni,
Hata maji ya mafuriko yajapo hayatotuacha ulipotuona mara ya mwisho..
Tafadhali usituache mtaroni..

Usichoke kutupa mkono wako wenye nguvu..
Ulionona kutokana na hali ya huko ulipo,
Japo nawe ulikuwepo tulipo,
Kujaribu kwako kumekufikisha hapo,
Nasi tnajaribu kila uchwao,
Lakini hatujapata suluisho,
Tafadhali usituache mtaroni.

Japo vina havijazingatiwa,
Naamini washairi watashawishiwa,
Ujumbe kwa kipelu utafikishwa,
Wa mtaroni tutaokolewa,
Nasi tutakuwa nae majaaliwa.
Tafadhali usituache mtaroni​
 
Mkuu hiyo lugha, is not a joke! thanks I managed a bit, ila sijacheka ingawa nimepata ujumbe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…