Hadithi ya kupuliziana dawa vyumbani upuuzwe?

Hadithi ya kupuliziana dawa vyumbani upuuzwe?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Mchango wa mashabiki uwanjani katika timu kupata ushindi ni asilimia ngapi? Je nguvu hiyo ya mashabiki kwenye timu kupata matokeo inapimwaje?

Je, mashabiki wa Yanga wanaweza kuchangia Yanga kuifunga Barcelona uwanja wa Mkapa?

Hivi zipo dawa ambazo unaweza kuzipuliza chumbani na kusababisha mchezaji apungukiwe na kiwango chake halisi? Kama zipo ni dawa gani hizo.

Lisemwalo lipo kama halipo linakuja, kwanini zipo timu ambazo zikienda mechi za ugenini zinabeba unga, maji, maharagwe na mpishi wao kabisa? Mbona timu zinazofanya hivyo hazijawahi kuhojiwa na tff, CAF wala FIFA sababu za hofu ya kufanya hivyo? Kama zipo dawa za kutia kwenye vyakula ili wachezaji walegee kwanini zikosekane za kupuliza?

Je, zibaki Tu kama tuhuma hadi lini mpaka kitokee nini?
 
Yanga bwana, mkifungwa mnasingizia mmelogwa, mara mmepuliziwa dawa. Mbona Simba wakifungwa wanachukulia ni sehemu ya mchezo?

Ujue wanga ndio wanapenda sana mambo ya kishirikina. Huwezi kulia lia kila siku unadai umerogwa kama wewe sio mrogaji. Endeleeni hivyo hivyo bakini kwenye zama za ujima ni nafasi nzuri ya Simba kujitenga na kuwa level ya kimataifa zaidi.

Simba Bingwa msimu huu. Mwisho wa ligi vyura mtasema.

"Simba wameloga, Simba wamepulizia dawa, Simba wamenunua mechi"

Logeni na nyie basi, pulizeni dawa na nyie basi, nunueni mechi na nyie basi.

Shubamiitttttt
 
Back
Top Bottom