SoC02 Hadithi ya mvuvi na samaki asiyevulika

SoC02 Hadithi ya mvuvi na samaki asiyevulika

Stories of Change - 2022 Competition

Lidafo

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2019
Posts
889
Reaction score
1,789
Katika pitapita zangu na harakati za kutafuta maisha nilijikuta katika Kijiji cha Tupo nyuma, Mji wa Tumechoka, Nchi ya Ahadi nyingi yenye ziwa kubwa sana liitwalo 'Ziwa jeupe'.

Ziwa hili ni ziwa lenye samaki wengi sana wadogo kwa wakubwa, Lakini kuna samaki mmoja mkubwa sana ambaye yasemekana hakuna mvuvi aliyeweza kumvua, Kila mvuvi akijaribu kumvua samaki huyo hushindwa na kujikuta muda wake wa kuvua umeisha hivo kuamua kurudi kijijini na samaki wengine wadogo wenye miiba mingi na kuwapa wanakijiji.

Hali hii ya kula samaki wadogo tena wenye miiba mingi kila siku inawakera sana wanakijiji hawo, Kubwa wanalolalamikia ni kuwa Kila mvuvi wanayemtuma hushindwa kumvua samaki huyo.

Basi nami nikasogea karibu kuliona ziwa hilo na ndipo akaja mtu mmoja jila lake anaitwa 'Msema kweli' ambaye naye ni mwanakijiji wa kijiji Cha tupo nyuma, Baada ya salamu Msema kweli akanihadithia kuwa mara baada ya ziwa jeupe kujulikana kuwa Lina samaki mkubwa Sana watu wengi walikuja kuomba idhini ya kumvua samaki huyo ambaye anaukubwa wa kutosha kula Kijiji kizima na nchi yote ya Ahadi nyingi.

Msema Kweli akasema mvuvi wa Kwanza alijitahidi kumvua samaki huyo lakini wapi, na kipindi hicho mvuvi alikuwa ni lazima atoke katika familia moja tu, Nayo ni familia ya bwana heri.

Mvuvi wa pili naye alitoka katika familia ya bwana heri akajitahidi sana kumvua samaki huyo akishirikiana na wasaidizi wake kutupa nyavu na kuivuta lakini walipata samaki wadogo tu, kabla ya muda wa mvuvi wa pili kuisha wanakijiji walikaa wakaona Kuna umuhimu wa familia nyingine kushiriki katika uvuvi huo, hivyo wakapanga baada ya mvuvi wa pili kumaliza muda wake mvuvi wa tatu atashindanishwa na wavuvi kutoka katika familia nyengine na wanakijiji ndio watakaoamua nani aende kuvua katika ziwa jeupe.

Baada ya mvuvi wa pili kumaliza muda wake, Sasa familia ya bwana heri na familia nyingine zikatoa watu wakugombania nafasi hiyo. Ila kama ilivyo ada mwenye nacho huongezewa familia ya bwana heri ikashinda lakini pamoja na jitihada zote bado samaki hakuvulika. Ikafika zamu ya mvuvi wa nne awamu hii pia mvuvi alitoka katika familia ya bwana heri, Mvuvi huyu alijulikana sana na Kupata umaarufu kwa ushawishi wake kwa wanakijiji aliwaaminisha kuwa safari hii samaki huyo ndio mwisho wake kwani ni lazima wamvue na nyama yake kila mwanakijiji atapata na kula na kufurahia utamu wa samaki huyo.

Ila bado samaki hakuvulika na badala yake mvuvi akarudi na konokono na kobe, Kitendo hiki kilizidi kuwakasirisha sana wanatupo nyuma lakini likaibuka kundi la watu likasema tumekuwa tukiletewa samaki wadogo tena wenye miiba ila awamu hii bora tumeletewa kobe na konokono, Hapo mimi nilicheka kidogo na kusababisha Msema kweli kukatiza hadithi yake.

Basi naye akacheka nikamuomba aendelee kuhadithia. Msema Kweli akaendelea akasema kundi lile lilisema kuwa bora hawa kobe tutawafuga na wengine tutawauza katika nchi za uchina.

Ikafika zamu ya mvuvi wa tano hapa Msema kweli alikohoa kidogo na Kisha kusema katika awamu zote zilizopita hii ndio awamu ambaye mvuvi wake alikuwa watofauti aliamini kuwa samaki atamvua tena kwa msaada wa wanakijiji wenyewe bila kutumia ngalawa, mashua na mawazo ya mataifa ya nje.

Mvuvi huyu wa awamu ya tano alitumia msemo maarufu sana wa 'Hapa uvuvi tu' Kwakweli mambo yalikuwa ni tafrani kwani kila msaidizi ambaye aliyekuwa hampi ushirikiano au mwenye mtazamo tofauti na yeye alimtosa ziwani.

Wengi katika wanakijiji hasa wenye maisha ya chini walimpenda na wengine walimkosoa wakisema mvuvi kalewa sifa sasa badala ya kujenga anabomoa.

Lakini ni tuseme jitihada haiwezi kuzidi kudra ya mungu na mla mbuzi hulipa ng'ombe kabla ya kumaliza muda wake Mvuvi huyu alifariki.

Kwa kuwa hakumaliza muda wake basi aliyekuwa msaidizi wake akashika nafasi yake na kuwa mvuvi mkuu, Ukistaajabu ya Musa hujayaona ya firauni msemo huu ulijidhihirisha waziwazi katika awamu hii ya sita ambayo ilibadili wasaidizi wengi wa mvuvi wa tano na kuweka wasaidizi wengine hapa Msema Kweli akanambia natamani nikuelezee kiundani kwanini wamebadilishwa lakini nahofia hutaweza kuelewa nami nikamwambia endelea na hadithi . Msema kweli akasema hadithi imeisha kwani Mvuvi aliyopo mpaka Sasa ni mvuvi wa sita.

Basi akaja mzee mmoja aliyeonekana kuchoka sana lakini mzee huyo alifahamiana na Msema kweli tukamsalimia na kisha akanambia kijana mimi naitwa mzee Ushauri lakini wengi huwa hawanithamini na hunipuuza, Mzee Ushauri akasema Ushauri huu ni kwa mvuvi wa sita, Kwanza nilazima mtambue samaki huyo ni mkubwa sana na hivyo ili kumvua kunahitaji mvuvi pamoja na wasaidizi wake wawe na akili kubwa nikamuuliza swali mzee Ushauri unamaanisha akili gani?

Mzee akacheka ha ha haa kijana na maanisha akili ya kuwaza, kupanga na kutekeleza .
Pili, Mzee Ushauri akasema Kama samaki ni mkubwa basi tambueni pia ni mzito, Hivyo wanahitajika wasaidizi wenye nguvu nao ni vijana hapo ni katia neno sasa mbona wanaomsaidia mvuvi wengi ni wazee Kama wewe?

Mzee Ushauri akasema ni Kweli usemalo lakini tambua wazee wanahitajika kwa sababu ya Ushauri Kama huu ninao wapa sasa hivi atanaivyo nguvu ya vijana isipuuzwe kwani ndio chambo cha kumvuta samaki huyo na ndio watakao mbeba.

Tatu akaniambia ilikumvua samaki huyo kunahitajika ngalawa imara ambayo haitazama hata Kama kuna upepo mkali na pia mvuvi na wasaidizi wake wanatakiwa kuwa na nyavu imara na utulivu wa hali ya juu wasiogope mawimbi ya maji na ngurumo za radi hiyo ni hali ya kawaida ziwani.

Mwisho mzee Ushauri akaniambia ungepewa nafasi ya kuwa msaidizi wa mvuvi ungefanya nini? Nikamjibu ningefuata Ushauri wako ningetumia nguvu zangu Kama kijana kumvuta samaki huyo mzee Ushauri akacheka sana na kuniambia kumbuka ' muonja asali haonji mara moja'.

Basi mzee Ushauri akasema Mimi naondoka vijana narudi huko nilikotoka Ila niwaache na maswali machache kwanza jiulizeni kwa Nini wavuvi wote wanatokea familia ya bwana heri?

Je, ipo haja ya kubadili mvuvi atoke katika familia nyingine? , Kwanini kila mvuvi anakuja na wasaidizi wake? Kwani ziwani Kuna siri gani? Sawa wameshindwa kumleta samaki mkubwa basi hata kambale wa kawaida hamna?

Mbona wao wananenepa sisi tunakonda.

Sote tukasema kwa kuwa mvuvi ni bwana heri na ziwa Ni la bwana heri basi yote heri.

Mwandishi: Shafii R. Bakari (Lidafo).
 
Upvote 1
Back
Top Bottom