Undava King
JF-Expert Member
- Aug 11, 2017
- 3,422
- 5,659
HADITHI YA UUMBAJI YA UGNOSTIKI
➖Mojawapo ya mambo yaliyoweka ugnostiki tofauti na aina nyingine za Ukristo wa hivi karibuni ni kuhusiana na Hadithi yao ya kushangaza ya uumbaji ni tafsiri ya Hadithi ya uumbaji ya kitabu cha mwanzo ambayo kiukweli imeyageuza maandiko hayo ya Agano la kale kichwa chini.
➖Baadhi ya watu huiona hadithi hiyo kama kitu cha kupuuzwa au kitu cha ajabu ajabu. Wengine wanaichukulia Hadithi hiyo ya Wagnostiki kama Kufuru kabisa. Wengine huiona yenye kusisimua na kutia moyo.
➖Haijalishi maoni yako au maoni yoyote kuhusiana na Hadithi ya Uumbaji ya Wagnostiki yapoje, lakini ikiwa unataka kuekewa unatakiwa kwenda sawa na masharti yake, ni muhimu kuitazama hadithi hiyo ya Uumbaji ya Wagnostiki vilevile kama wagnostiki wenyewe wanavyo itazama. Lakini yote kwa yote Hadithi hiyo inatoa uwezekano hata majaribio ya kujaribu kuelezea hali ya wanadamu. Kwanini ulimwengu tunao ishi umejaa mateso yasiyo na maana?
Je, tunaweza kufanya nini ili kushinda upuuzi huo na taabu na kuweka maisha yetu katika matumizi yenye kuleta maana?
Je Ni kwwli sisi ni wa ulimwengu huu,
Na kama sisi sio wa Ulimwengu huu, Je, sisi tumetokea wapi hasa?
➖Hadithi ya Uumbaji ya Wagnostiki imetujia katika matoleo mengi tofauti na katika maandiko tofauti tofauti ya Wagnostiki Ni dhahiri na wazi kwamba hapakua na Toleo moja kuhusiana na Hadithi hiyo.Lakini taarifa nyingi tofauti tofauti za Wagnostiki kuhusiana na Uumbaji ambazo zimesalia hadi hivi leo, zinatofautiana kimuundo lakini ni zenye kufanana katika maeneo ya msingi.
Kwa muhtasari kutokana na kielelezo hicho cha msingi; Mungu Baba (The One) alitoa kundi la viumbe wa kiroho walio fahamika kama AEONS ambao waliishi mbinguni (ambapo wagnostiki wanapaita Pleroma, neno linalo maanisha "Fullness" yaani Utimilifu) wakiwemo Mama mtakatifu Pamoja na Kristo. Mmoja wa viumbe hao wa mwisho kutoka kwa Baba, aliitwa SOPHIA, alijifungua kiumbe kipya peke yake bila kumhusisha mpenzi wake au sehemu yake ya kiume au bila kupata Idhini ya Baba. Kutokana na kwamba Kiumbe huyo aliye zaliwa chini ya hali kama hiyo ambapo sophia alijifungua bila idhini ya mwenza wake bila kumhusisha Baba kiumbe huyo hakufanana na Wakaaji wengine walio kamilika wa PLEROMA, Badala yake kiumbe huyo mpya alikuwa mjinga na mkorofi. Huyo ndiye alikuwa "Fundi" craftsman au Mbunifu mkuu wa ulimwengu huu wa kifizikia (Material world) ambaye Wagnostiki walimtambua kama Mungu wa Agano la Kale. Aliumba Ulimwengu wa Kimwili ili kuakisi utu wake mwovu na kunasa cheche za uungu, vipande vya Pleroma, ndani ya wanadamu. Ilikua ni Juu ya kristo kuwaamsha wanadamu kutambua Asili yao halisi ya kweli na kuwakomboa kutoka katika Ulimwengu huu.
KABLA SIJAENDELEA
AEONS ni nini? Aens ni watoto wa Baba kutoka kwa Baba na Mama. Kama alivyo Baba ndivyo walivyo watoto. Watoto hao walikuwa wamekamilika .. kulikuwa hakuhitajiki msaidizi hakuna matengano ... AEONS walikuwa Androgyne yaani mwanamke-mwanaume walikua Jozi au Pair , kwamba Aeon mmoja alikuwa ni mwanamke huyo huyo na ni mwanaume huyohuyo. Hawakuwa na miili walikuwa ROHO SAFI pure spirits emanated from the Father and the Mother.. Kwahiyo SOPHIA pia alikuwa ni Aeon ambae ni mwanamke na pia ni mwanaume. Sehemu yake ya kiume iliitwa KRISTO.
➖Marejeleo niliyo yatumia hapo chini kuelezea jambo hili yanatoka katika "Kitabu Cha Siri Cha Yohana" , ambacho kinawasilisha na kuwakilisha vyema kabisa mtazamo wa shule za kawaida za Wagnostiki,bHadithi za uumbaji za Wavalentine, Madhehebu ama shule zingine za hivi karibuni za Kikristo zinazo chukuliwa kama sehemu ya Wagnostiko,bado wanafuata mtindo huu wa kimsingi, ingawa maelezo mengi yanatofautiana.
HADITHI YA UUMBAJI YA KITABU CHA SIRI CHA YOHANA.
Hapo mwanzo kulikuwa na Mmoja tu (THE ONE), Baba, ambaye yuko
"isiyo na kikomo, kwa kuwa hakuna kitu mbele yake cha kuiwekea kikomo, Kisichoeleweka, kwakuwa hakuna kitu kabla yake cha kuipima, kisicho weza kupimika, kwakuwa hapakuwa na kitu kabla yake cha kuipima. Kisichoonekana, kwakuwa hakuna kilichoiona, ya milele, kwakuwa iko milele,
Isiyoweza kutamkwa, kwakuwa hakuna kitu kingeweza kuielewa kuitanka, isiyo na jina, kwakuwa hakuna kitu mbele yake cha kuipa jina."
➖Baba alizungukwa na maji ya Kiroho yenye mwanga. Alitazama ndani ya maji na kuona uakisi wake. Reflection yake ikawa BARBELO, Mama, mwwnzake wa kike. Barbelo pia aliitwa "Pronoia", "Forethought", kwasababu alikuwa wazo la kwanza la Baba.
➖Barbelo alimwomba Baba amjalie Kujua mambo ya mbele (kimbele),: kutoharibika, Uzima wa milele na Ukweli. Baba alikubali ombi lake. Kujua kimbele, Kutoharibika, Uzima wa Milele, na Ukweli vilikuja na kumtukuza Baba na Mama yao..
➖Baba alimtazama Barbrlo, na Barbelo akapata Mimba kisha akazaa cheche ya mwanga sawa na Nuru ya Baba. Huyu alikuwa Mwana, ambaye pia aliitwa "Autogenes", "Aliyejizalisha" , kwakuwa alikuwa chini kabisa na Baba. Pia aliitwa "Kristo" , "Jina kuu kuliko kupita kila jina". Kisha Baba akampaka mafuta mwana kwa wema wake, ambao ulipitisha wema wake mkamilifu kwa Mwana wake. Mwana alimtukuza Baba na Mama yake.
➖Kama vile Barbelo alivyo mwomba Baba ampe Aeon mpya, Mwana pia aliomba apewe Mwingine: Akili . Baba na Mama walikubali . Akili iliamka na kumtukuza Baba na Mama yake.
➖Akili ilitaka kuleta kitu kingine (Aeon nwingine) kwa kupitia Neno la Baba. Mapenzi (will) yalizaliwa, yakifuatiwa na Neno.
➖Baba alimfanya mwana kuwa Bwana wa nguvu zote na ukweli. Kutoka kwa Mwana kulikuja kutokea Nuru nne: Harmozel, Oroiael, Daveithai, na Eleleth. Kila mmoja alikuja kuwa na Aeons tatu za ziada pamoja naye. Eons tatu zilizokuwa pamoja na Harmozel walikuwa Neema (grace), Ukweeli (Truth), na Umbo (Form). Na watatu walio kuwa pamoja na Oroiael walikuwa ni Uono (Insight), Utambuzi (perception) na Kumbukumbu (memory). na Watatu walio kuwa pamoja na Daveithai walikuwa Kuelewana, Upendo na Wazo (Idea). Na watatu walio kuwa pamoja na Eleleth walikuwa Ukamilifu, Amani na Sophia (Hekima).
➖Aliyefuata baada ya hapo ni "Mwanadamu Mkamilifu" , Pigeradamas (,"Adamu Mgeni" strange Adam" "Adamu Mtakatifu" , au "Adamu Mzee" , ambaye alikuja kuwa na kumtukuza Baba. Aliwekwa katika Eon ya Harmozeli. Adamu alikuwa na mwana, Seth, ambaye aliwekwa katika Aeon ya Oroyaeli. Aliwekwa ili kusimamia /kwakusimamia "Roho za Watakatifu" , wale walio na Gnosis (Maarifa/ujuzi) katika Aeon ya Daveithai. Roho za wale ambao hawakuwa watakatifu, lakini ambao hata hivyo walitubu hatimaye, walipewa nafasi yao wenyewe katika Aeon ya Ekeleth.
➖Sophia aliwatazama viumbe hao wa ajabu, wenye kung'aa pande zote. Tamaa ya kuzaa Aeon yake mwenyewe iliibuka ndani yake. Lakini alitenda juu ya tamaa hii bila subira na kwa msukumo; hakujishughulisha kumhusisha mshirika wake (mwenza wake/ sehemu yake ya kiume ambaye ni Kristo) wa kiungu, wala kupata kibali cha Baba. Kwasababu Sophia alikuwa ameshuka kutoka kwa Baba, Alikuwa amejaa nguvu zake kuu, na aliweza kuzaa kiumbe kipya ambacho kilikua na baadhi ya asili yake ya Kiungu. Lakini kwasababu chombo hiki /kiumbe hiki kipya kilibuniwa na Sophia peke yake, hakikufanana na wale wasio kufa. Badala yake, kilikua cha kutisha na kisicho na umbo .. aeon hii mpya ya ajabu ilikua ya kutisha na isiyo na umbo . Kilikuwa kama nyoka mwenye kichwa cha Simba. Macho yake yaliwaka kama umeme.
➖Kwa woga na aibu, Sophia alimtupa mwanawe nje ya makao ya Kimungu (Pleroma, "Utimilifu") kwa matumaini kwamba hakuna hata mmoja wa wakaazi au wakaaji wengine wa mahali hapo pakamilifu angemwona. Ili kumficha zaidi (mwanaye huyo) , alimfunika katika wingu linalo ng'aa na kumweka juu ya kiti cha Enzi katikati yake.
➖Alimwita mwanaye huyo YAKDABAOTH (Jina ambako lina maanisha "Mtoto wa Machafuko"), na tangu wakati huo Yaldabaoth amekuwa akiitwa pia SAKLA, kumaanisha "Mjinga", na pia amekuwa akiitwa SAMAEL, kumaanisha "Mungu Kipofu".
➖Yaldabaoth "alifungamana na kutokuwa na Akili ndani yake" na akazalisha (akawaumba) Archons kumi na mbili, Viumbe wa pepo ambao watakuja kutawala dunia hivi karibuni kutoka kwenye nyanja za mbinguni juu yake; Viumbe hao 12 walikuwa ni Athoth, Harmas, Kalila-Oumbri, Yabel,bAdonaios/Sabaoth, Kaini,bAbeli, Abrisene, Yobel, Armoupieel,bMelcheir-Adonein, na Belias.
➖Kwasababu ya upumbavu wa Yakdabaoth, alikuwa mwovu na asiyejua ukoo wake. Alitangaza kwa Jeuri akisema "Mimi ni Mungu na hakuna Mungu mwingine ila mimi". Archons wake kumi na mbili wa awali walizalisha (waliumba) Archons wapya hadi kufikia 365 ambaoo kila mmoja anatawala siku moja katika mwaka.
➖Akiwa mtoto wa Sophia, Yakdabaoth alikuwa na mfano kama picha wa Pleroma ndani yake . Aliumba Ulimwengu wa kimwili kulingana na mfano huo au kwa kuigilizia kile anacho kiona ndani yake ambacho ni mabaki ya asili ya mama yake Sophia aliko tokea (Pleroma), Lakini kwasababu ya ujinga wake na upotovu, , yote yaliyo tokea yakikuwa ni mabaya. Ulikuwa ni uigaji ulioharibika wa uharibifu na duni sana ukilinganisha na kiekelezo cha Kimungu.
➖Sophia alitazama hayo yote yaliyokuwa yakifanywa na mwanaye na akapigwa na huzuni na akajihisi mwenye hatia. Alilia na kutubu kwa kuzaa mtu muovu kama huyo. (Kwakuwa kuumbwa kwa ulimwengu huu wa kimwili ni jambo baya na wala si mpango wa Baba na hahusiki has nothing to do with this evil world).. Baba, aliyejawa na Upendo mkamilifu, alisikia maombi yake na akaahidi kumsamehe na kumrejesha katika hadhi yake ya awali. Lakini kwanza ilimbidi abaki katika mbingu ya tisa (safu ya anga iliyo karibu zaidi na Pleroma, juu ya Yaldabaoth na mbingu saba zilizo na watu wa Archons chini yake) hadi atakapo patanishwa kwa ajili ya dhambi yake na kurekebisha upungufu wake.
➖Wakati huohuo, Yaldabaoth na Makamanda wake (The Archons) Waliona picha ya Adamu wa mbinguni kutoka katika Ulimwengu safi wa Baba. Hawakujua ilitoka wapi, lakini walivutiwa nayo. Waliamua kujaribu kuunda au kuumba mwanadamu kwaajili yao wenyewe. Lakini mwanzoni kiumbe wao alilala chini bila uhai. Hawakuweza kujua jinsi ya kumhuisha..awe kiumbe hai.
➖Wakiwa wamesimama karibu na ule mwili usio tembea huku wakishangaa nini cha kufanya, wale viumbe wenye neema wa Pleroma walikuja na mpango wa kusaidia sehemu ya Sophia ambayo ilikuwa imenaswa ndani ya Yaldabaoth irudi kwake ili aweze kurudi Pleroma.
➖Wajumbe kutoka Pleroma walimtokea Yaldabaoth na kumshauri apulizie Roho yake kwenye Uso wa Adamu, bbaada ya hapo walimhakikishia, mwili ungeamka na kusimama. Yaldabaoth alifanya hivyo, na nguvu za Sophia zikapepea kutoka kwake na kuingia kwa Adamu, na kumfanya mtu wa kwanza kuwa Hai. Kwasababu ya uwezo wa Sophia ndani yake, tayari Adamu alikuwa na Hekima, alikuwa wa kiroho zaidi na mwenye Akili zaidi kuliko Waumbaji wake.
➖Kwa wivu na chuki, Archons walimfanya Adamu kufa awe anakufa Mortal. Walimweka katika bustani ya Edeni, ambayo waliijaza kila aina ya vyakula vya fahari za kimwili na kumkengeusha kutoka kwenye asili yake ya kweli ya kimungu.
➖Wakuu au THE ARCHONS walitaka kumiliki utambuzi wa Kimungu wa Adamu kwaajili yao wenyewe, kwahiyo wakautoa uwezo huo kutoka kwa Adamu na kuunda au kuumba kiumbe kipya wa kuhifadhi .. cha kuhifadhi uwezo huo ..kiumbe kipya aliitwa HAWA. Adamu alipomwona, mara moja alimtambua kuwa mwenzake wa kiroho. Kwasababu watoto wa Baba walikuwa hapo awali wamekamilika ni mwanamke ni mwanaume.. alicho fanya Yaldabaoth pamoja na wakuu ni kutenganisha sehemu yake moja ya kike kuwa tofauti ili kupunguza uwezo wa Adamu .. baada ya hawa kutokea Adamu alimtambua kuwa ni mwenzake ni sehemu yake yeye mwenyewe ya kiroho imetenganishwa na yeye. Kristo alikuja wakati huo ambaye ni sehemu ya kiume ya sophia kuwasihi Adamu na Hawa kula katika mti wa Ujuzi mti wa maafifa (Gnosis) na kisha kukua katika Ufahamu wao na ubora wao zaidi ya waumbaji wao.
➖Baada ya Kristo kuja kuwaambia Wale tunda la maarifa (gnosis) , Yaldabaoth alichemka kwa Chuki na wivu, alimbaka Hawa na kumtupa yeye na mwenza wake nje ya Bustani. Wana wawili watoto wawili walizaliwa kutokana na ngono hii ya kusikitisha kati ya Yakdabaoth na Hawa. Watoto hao wawili mapacha wa Yakdabaoth aliozaa na Hawa kwa kumbaka waliitwa KAINI na ABELI, ambao pia wanaitwa "YAHWEH" na "ELOHIM" (Majina mawili ya Mungu katika Agano la Kale).
➖Lakini Baadaye Adamu na Hawa walifanya ngono ya upendo, ya maelewano peke yao. Matokeo ya muungano wao walipata Mvulana aliye elimika (Enlightened) ambaye walimwita "SETHI" baada ya mwana wa Adamu wa mbinguni.
➖Yaldabaoth hakuweza kustahimili ukweli kwamba sasa kulikuwa na viumbe watatu katika uumbaji wake ambao walikuwa na Nuru na bora kuliko yeye. Aliwalazimisha Adamu, Hawa na Sethi kunywa "Maji ya Usahaulifu" ili wapoteze utambuzi wao (wajisahau wasijitambue wawe usingizini) . Lakini uwezo wa kufufua Gnosis ulikuwa umelala ndani yao; Yaldabaoth hakuwa na uwezo wa kuifuta (gnosis) kabisa. Na wazao wao wa kiroho miongoni mwa wanadamu wanabaki na uwezo wa kupata tena nuru hiyo yenye kuokoa. Wanacho hitaji tu ni mwokozi, Kristo, ili kuwafunulia kama alivyo wafunulia Mababu zao wa kwanza.
ESOTERIC CHRISTIANITY