Hadithi za zamani

Hadithi za zamani

mahunduhamza

Member
Joined
Aug 25, 2021
Posts
19
Reaction score
46
Imesimuliwa na Zubeda Abdalla Omar

Alitokea Chanjagaa akajenga nyumba akakaa, mwanangu Mwanasiti kijino kama chikichi, cha kujengea vikuta na vilango vya kupita. Hapo zamani za kale alikuwepo bwana mmoja, aliekuwa na wake watatu mmoja alikuwa mwizi. Yule bwana alikuwa anafuga mbuzi, siku moja kati ya wale wake zake mmoja aliiba mbuzi na kumchinja na kumpika bila ya yeye kujua.

Aliporudi safari yake aliuliza nani alimchinja mbuzi? Wote walikataa. Yule bwana akasema basi mimi nitafanya dawa. Wakajibu sawa, yule bwana akafanya mambo yake kisha akawapeleka mtoni. Walipofika aliwambia mmoja mmoja aanze kuingia mtoni na huku akiimba. Aliingia wa kwanza huku akiimba nyimbo: Kachiriri, kachiriri kachiriri kachiriri kachiriri. Mani nenga Kachiri Depala dipolo kachiri Dipolo dabambo kachiriri Kachiriri kachiriri kachiriri kachiriri kachiriri.

Alipomaliza kuimba akaibuka, kwani yeye hakuwa mwizi. Akafuata wa pili huku akiimba: Kachiriri, kachiriri kachiriri kachiriri kachiriri. Mani nenga Kachiri Depala dipolo kachiri Dipolo dabambo kachiriri Kachiriri kachiriri kachiriri kachiriri kachiriri. Yeye pia akaibuka na kukaa pembeni. Akafuata yule wa tatu akaingia huku akiimba: Kachiriri, kachiriri kachiriri kachiriri kachiriri.

Mani nenga Kachiri Depala dipolo kachiri Dipolo dabambo kachiriri Kachiriri kachiriri kachiriri kachiriri kachiriri. Lakini yeye alizama. Kuona vile yule bwana akajua kwamba yule mke wa tatu ndie mwizi. Hapo akafanya dawa zake na yule bibi akaibuka, alimuomba radhi mumewe na kuahidi kuwa hatorudia tena kosa lake. Na yule bwana alikubali na wakaendelea kuishi kwa raha mustarehe.
 
Back
Top Bottom