Hadji Manara simuelewi

Hadji Manara simuelewi

ukikaidi utapigwa2

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2015
Posts
15,265
Reaction score
29,991
mpka sasa nashindwa kumuelewa msemaji wa simba kuhusu swala la Ramadan Sigano kwnn alikurupuka kusema vitu asivyo kua na uhakika navyo pili wao wamepokea uongozi kutoka uongozi wa kina Rage hayo mambo ya simba kumsomesha Rama kayafahamu lini haoni kua kasha haribu sycology ya mchezaji?
kama hii Simba itaendelea kua na vingozi wa aina hii sijui msimu ujao kma hata nafasi ya tatu tutaipata
 
Kuna watu kuwaelewa hadi uwe umeishi magomeni,kariakoo au kinondoni
otherwise hutawaelewa....

Samuel Etoo alilelewa na Real Madrid lakini alienda kuichezea Barcelona

Haji manara ni mtu wa vijiweni ..na anayo yazungumza ni ya kijiweni zaidi
 
Ambao hawaeleweki ni hao wasiyowaelewa akina Haji Manara, Jerry Muro, Tobias Kifaru, Masau Bwire na kama hao. Hamjatambua kwamba kila mmoja ni 'msemaji' wa klabu iliyomwajiri? Tafsiri ya Kiswahili ndiyo imeviponza vilabu, kwa hivyo badala ya kutafuta wasemaji kwa maana ya 'press secretaries/spokespersons' wao hutafuta wasemaji kwa maana ya wasemaji. Kwa msingi huo tutegemee nini? Wacheni 'wasemaji' wa vilabu vyetu waseme hadi waishiwe na maneno! Na Mwadui nao kama watataka ushauri, wasimwachie Julio kuwa kocha tu, bali kocha msemaiji, kwa sababu ni msemaji!
 
Bongo kuna mpira bwana!!! mambo mengine ni kujipunguzia siku za kuishi tu bila sababu yoyote. we msemaji anakwambia leo nimekuja kupiga mkwala tu!!! mala ohhho hao wanaokomalia suala la mesi ni wale walioshindwa uchaguzi uliopita!!! Na hao TANZANIA FITINA ASSOCIATION (TFF) Wameshindwa nini kulitolea ufafanuzi suala dogo kama hili??! kwani kama ni mkataba original uko pale, mala tunalichunguza!!!! FBI, njooni na huku bwana. tulishachoka kwani yamekuwa ni machaka ya watu kupiga tu pesa na si kuendeleza soka.
 
Ambao hawaeleweki ni hao wasiyowaelewa akina Haji Manara, Jerry Muro, Tobias Kifaru, Masau Bwire na kama hao. Hamjatambua kwamba kila mmoja ni 'msemaji' wa klabu iliyomwajiri? Tafsiri ya Kiswahili ndiyo imeviponza vilabu, kwa hivyo badala ya kutafuta wasemaji kwa maana ya 'press secretaries/spokespersons' wao hutafuta wasemaji kwa maana ya wasemaji. Kwa msingi huo tutegemee nini? Wacheni 'wasemaji' wa vilabu vyetu waseme hadi waishiwe na maneno! Na Mwadui nao kama watataka ushauri, wasimwachie Julio kuwa kocha tu, bali kocha msemaiji, kwa sababu ni msemaji!

Huo utaratibu hutumiwa hata katka ligi za wanaojua, ambapo kocha huwa anatoa matamko kuhusu timu yake.
Sasa kwetu, sijui TFF waliutoa wapi huu utaratbu wa kuwa lazima timu zinazoshiriki ligi kuu ziwe na msemaji wake.. Na kwa Mwadui, hawana jinsi lazima wapeleke jina la "msemaji" wake katka ofisi za TFF, pamoja na wasifu wake.
 
Alichokisema msemaji wa simba iwe ni ya kweli au uongo kikubwa ni ile hali yake ya kuongea kama anacheza bao. Huu utamaduni wa wasemaji wa vilabu tff inabidi itafute namna ya kuwarejesha kwenye mstari.
 
kwa aina hii tutaishia kuwaita wachezaji wetu Messi na Rinaldo
 
Kuna watu kuwaelewa hadi uwe umeishi magomeni,kariakoo au kinondoni
otherwise hutawaelewa....

Samuel Etoo alilelewa na Real Madrid lakini alienda kuichezea Barcelona

Haji manara ni mtu wa vijiweni ..na anayo yazungumza ni ya kijiweni zaidi

tusubiri kagame na mtani jembe ndio mwisho wetu kwa Aina hii ya uongozi kamwe hatuwezi fika kokote
 
Back
Top Bottom