Hafahamu mzunguko wake wa mwezi

AZIMIO

Senior Member
Joined
Jun 15, 2011
Posts
188
Reaction score
52
Nina rafiki yangu wa kike tangu nianze nae mahusiano ni miaka miwili imepita siku moja nilimuuliza kuhusu mzunguko wake aliniambia hafahamu kwa kuwa huwa inamtokea bila ya kuwa na fumula.

Mfano mwezi huu imetokea inaweza kupita miezi mitatu mingine ndio anapata, na kabla ya kupata huwa anatokwa na damu iliyo katika mfumo wa mgando yaani vipande vipande vya damu vidogo dogo.

Nimemshauri aende kwa Dr.na amepewa dawa kwa mara ya kwanza zikatoka kwa wingi lakini baada ya muda akaniambia hazitoki tena zimeacha.

Je tatizo ni nini wanajamvi?na akitaka kupanga kupata mtoto katika hali hii anafanyaje? kwa maana hajui siku salama ni zip na siku sio salama ni zipi?Msaada tafadhari.
 
Tell her or buy her a diary,awe anarecord kila mwezi aone cycle ikoje,.from there ndo mnaweza fanya maamuzi, ila pia kama wakati mwingine anaskip had miez 3 msitegemee sana 'calendar method' itawa-mislead
 
Asante kwa ushauri tutauzingatia
 
Jamani ushauri please, hili tatizo linawagusa wengi humu jamvini, please wenye ideas.
 
Anasumbuliwa na ugonjwa gani nje ya huo???
Je kiakili yupo sawa?? Stress na mambo mengine
Je aliwahi kutoa mimba?

Je ashapima kizazi kama kiko sawa yani ultra sound?
Daktari alivyompa dawa alimueleza tatzo ni nini??

Hebu tuanzie hapa then mengine tutaendelea kutokana na majibu yako...
 
Tell her or buy her a diary,awe anarecord kila mwezi aone cycle ikoje,.from there ndo mnaweza fanya maamuzi,ila pia kama wakati mwingine anaskip had miez 3 msitegemee sana 'calendar method' itawa-mislead

Nadhani haujamshauri sahihi kwa jinsi nilivyoelewa tatzo lake maana anasema inaweza pita miez mi3 hajaona siku ina maana mzunguko wa zaidi ya siku 90...hii ina maana cycle yake haipo sawa kabsa si ya kila mwezi...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…