Hafla ya uapisho wa Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Victoria Charles Mwanziva

Hafla ya uapisho wa Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Victoria Charles Mwanziva

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mhe. Victoria Charles Mwanziva amekula kiapo cha uongozi kwa nafasi ya Mkuu wa Wilaya mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka leo tarehe 30 Januari, 2023 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe.

Mhe. Victoria Charles Mwanziva aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ludewa mnamo tarehe 25-Januari-2023

Katika hotuba yake ya kwanza baada ya uapisho Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mhe Victoria Charles Mwanziva amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumpa nafasi ya kushirikiana na viongozi mbalimbali wa Ludewa kusimamia mipango ya maendeleo.

Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mhe Victoria Charles Mwanziva amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka, amewashukuru viongozi wote waliohudhuria zoezi la uapisho na kwa mapokezi mazuri waliyoonesha kwake

“Ludewa ya Utalii, Uchumi wa Chuma kwa maendeleo yetu”

#LudewaYetu
#LudewaYaSamia
#UongoziShirikishi
#KaziIendelee
index.jpg
indexjki.jpg
indexm.jpg
 
Mbona Ktk Mkoa wa Njombe walikuwepo wengine lkn umerusha picha za huyu mdada tu?
Unataka kutuambia nini bwana mkubwa? sema usikike!
 
Back
Top Bottom