Baadhi ya wagombea wa nafasi ya mwenyekiti katika vijiji vya Uswaa, Mamba na Kiselu katika wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro wamelalamika kuenguliwa majina yao huku baadhi yao wakidai fomu zao zimeongezewa maneno na alama, wengine fomu zikionesha kuwa wameweka alama ya kuwa na ulemavu.