Haiba ya 'brothers are forever' ya mwamba inamuotea matende

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Nilimfahamu kwa karibu kipindi cha ukarabati wa kisasa wa Bills.. Nilikuwa sehemu ya technical team.. Hivyo tulionana karibia kila siku pale site

Mwamba ni mtu makini sana mtulivu asiye na papara, mwangalifu mno anayeepuka kuharibu kwa namna zote!
Ana tunu ya upendo halisi.. Ni mwepesi sana kusaidia kwa wahitaji.

Ana haiba ya kujenga undugu (ndugu wa faida.. Sisterhood and brotherhood) kwamba akikufanyia fadhila basi usimsahau.

Network za maisha zinajengwa hivyo.

Mwamba kwa karama na vipawa vyake amefanikiwa pakubwa kujenga taasisi imara na kwa mafanikio makubwa na kuiweka kwenye ramani ya dunia.

Amewajenga pia wengi sana ndani na nje ya CHADEMA na amewasaidia wengi pia.. Ana nafasi yake kubwa kwenye siasa za upinzani Tanganyika

Pamoja na yote hayo lakini ni binadamu wa kawaida asiyekosa mapungufu yake.. Na ni mapungufu haya ndio maadui nje ya CHADEMA wanayatumia kumyumbisha na kumpotosha

Kwa kukaa muda mrefu kwenye nafasi moja na kutumainiwa kwenye mengi.. Kumemfanya apitiwe kidogo na kuruhusu mianya ya adui kujipenyeza kwenye mamlaka yake na kutengeneza mitego mingi ya kumbomoa

Ni mwepesi kusamehe pengine kulingana na imani yake na hili maadui waliliona na kulitumia vema sana.

Akawapenda maadui zake kama anavyowapenda majirani zake!

Waliokuwa naye ndani ya taasisi ambao wengi kawalea yeye waliona hatari iliyopo mbele kutokana na haiba yake.

Lakini pengine kwa kudhani kawalea kawakuza na kuwasaidia kwenye mengi hawawezi kumshauri sana!

Ama yoyote watakayo kafanya lazima wapate kibali chake!

Kiuhalisia ni kwamba taasisi imeshakuwa kubwa sasa! Kubwa sana! Na kwa hali ilivyo taasisi sasa ni kitisho halisi kwa mamlaka.. Haiba ya undugu wa faida haifai kabisa kwenye hii vita!

Adui amejawa hofu na woga.. Hivyo amedhamiria sana kuiua taasisi mapema iwezekavyo!
Mwamba asiishi tena wakati uliopita na kukumbusha fadhili alizowafadhili aliowakuza..

Hawa si wale walioikimbia taasisi.. Ni wenye mapenzi mema kwake na kwa taasisi. . Na ajaaliwe hekima kuu ya kuwasikiliza ni muhimu sana sana kwa ustawi wa taasisi

Maadui wameshaanza kumbomoa kidogokidogi.. Wamedhamiria kumuondolea legacy yake yote kwa kashfa mbali mbali.. Na hili watalifanya soon!

Muda si rafiki sana lakini bado kuna nafasi ya kukengeuka maagizo na vitisho vya adui kabla hakujakuchwa kisha kukapambazuka!

Sentence yake MOJA tuu itamaliza kadhia yote pale atakaposema.

Kwa maslahi mapana ya chama chetu tulichokijenga kwa damu na jasho nimeamua kujitoa kwenye hiki kinyang'anyiro na kumuunga mkono yule asiyependwa na maadui zetu
Mungu Ibariki CHADEMA.. Mungu Ibariki Tanganyika!
 
Chadema inahitaji mabadiliko ya mfumo wake wa kisiasa, CCM wapo aggressive sana kwa upinzani, ili waweze kujibu mapigo kwa kishindo nao pia wanapaswa kufanya mashambulizi mkali sana, hapa sasa wanamuhitaji sana Lissu
Ndio maana wana side na mwamba ili kuleta ile kanuni ya divide and rule.. Lakini wakati huohuo baadhi wanajisahau na kuanza kumshambulia😂
 
Chadema inahitaji mabadiliko ya mfumo wake wa kisiasa, CCM wapo aggressive sana kwa upinzani, ili waweze kujibu mapigo kwa kishindo nao pia wanapaswa kufanya mashambulizi mkali sana, hapa sasa wanamuhitaji sana Lissu
FB_IMG_1736279771065.jpg
 
Nilimfahamu kwa karibu kipindi cha ukarabati wa kisasa wa Bills.. Nilikuwa sehemu ya technical team.. Hivyo tulionana karibia kila siku pale site

Mwamba ni mtu makini sana mtulivu asiye na papara, mwangalifu mno anayeepuka kuharibu kwa namna zote!
Ana tunu ya upendo halisi.. Ni mwepesi sana kusaidia kwa wahitaji.

Ana haiba ya kujenga undugu (ndugu wa faida.. Sisterhood and brotherhood) kwamba akikufanyia fadhila basi usimsahau.

Network za maisha zinajengwa hivyo.

Mwamba kwa karama na vipawa vyake amefanikiwa pakubwa kujenga taasisi imara na kwa mafanikio makubwa na kuiweka kwenye ramani ya dunia.

Amewajenga pia wengi sana ndani na nje ya CHADEMA na amewasaidia wengi pia.. Ana nafasi yake kubwa kwenye siasa za upinzani Tanganyika

Pamoja na yote hayo lakini ni binadamu wa kawaida asiyekosa mapungufu yake.. Na ni mapungufu haya ndio maadui nje ya CHADEMA wanayatumia kumyumbisha na kumpotosha

Kwa kukaa muda mrefu kwenye nafasi moja na kutumainiwa kwenye mengi.. Kumemfanya apitiwe kidogo na kuruhusu mianya ya adui kujipenyeza kwenye mamlaka yake na kutengeneza mitego mingi ya kumbomoa

Ni mwepesi kusamehe pengine kulingana na imani yake na hili maadui waliliona na kulitumia vema sana.

Akawapenda maadui zake kama anavyowapenda majirani zake!

Waliokuwa naye ndani ya taasisi ambao wengi kawalea yeye waliona hatari iliyopo mbele kutokana na haiba yake.

Lakini pengine kwa kudhani kawalea kawakuza na kuwasaidia kwenye mengi hawawezi kumshauri sana!

Ama yoyote watakayo kafanya lazima wapate kibali chake!

Kiuhalisia ni kwamba taasisi imeshakuwa kubwa sasa! Kubwa sana! Na kwa hali ilivyo taasisi sasa ni kitisho halisi kwa mamlaka.. Haiba ya undugu wa faida haifai kabisa kwenye hii vita!

Adui amejawa hofu na woga.. Hivyo amedhamiria sana kuiua taasisi mapema iwezekavyo!
Mwamba asiishi tena wakati uliopita na kukumbusha fadhili alizowafadhili aliowakuza..

Hawa si wale walioikimbia taasisi.. Ni wenye mapenzi mema kwake na kwa taasisi. . Na ajaaliwe hekima kuu ya kuwasikiliza ni muhimu sana sana kwa ustawi wa taasisi

Maadui wameshaanza kumbomoa kidogokidogi.. Wamedhamiria kumuondolea legacy yake yote kwa kashfa mbali mbali.. Na hili watalifanya soon!

Muda si rafiki sana lakini bado kuna nafasi ya kukengeuka maagizo na vitisho vya adui kabla hakujakuchwa kisha kukapambazuka!

Sentence yake MOJA tuu itamaliza kadhia yote pale atakaposema.

Kwa maslahi mapana ya chama chetu tulichokijenga kwa damu na jasho nimeamua kujitoa kwenye hiki kinyang'anyiro na kumuunga mkono yule asiyependwa na maadui zetu
Mungu Ibariki CHADEMA.. Mungu Ibariki Tanganyika!

Bila kutenganisha chama na biashara binafsi tungalipo sana kwenye makida makida!
 
Miongoni mwa wapambe wa Lissu ni Msigwa na Dr Slaa ,inashangaza.
Nimemsikia Mbowe emesema hatakuwa na shida na hata acha kusaidia chama ikiwa Lissu atashinda.
Kura zitakuwa za wazi kwanini wapambe wa Lissu mnaogopa hili,kwanini mnataka Lissu apite bila kupingwa?
An interested observer
 
Naenda Handeni Muda huu!
Ntapita Kilinge Cha Mkata, Kwegiloko, Kwamsisi, Kabuku Kisha ntaenda amboni

Nikirudi ntawajuza nani ni mwenyekiti wa CDM!

Alee Shabani Mabode anataka Kumsola
... Hiki ni Kizugua Mbwangaa! Simbauliiii
 
Miongoni mwa wapambe wa Lissu ni Msigwa na Dr Slaa ,inashangaza.
Nimemsikia Mbowe emesema hatakuwa na shida na hata acha kusaidia chama ikiwa Lissu atashinda.
Kura zitakuwa za wazi kwanini wapambe wa Lissu mnaogopa hili,kwanini mnataka Lissu apite bila kupingwa?
An interested observer
Kuna mahali nimesema Lissu apite bila kupingwa? Kwani wanagombea wawili tuu?
 
CHADEMA ni mbuyu mkubwa, kamwe hauanguki au kukatika kwa shoka kirahisi! Tundu Lissu na Freeman Mbowe wote wanatambua wanachikifanya. Ukiwa observer na kuwa neutral bila kuwa judgemental uta enjoy na kuelewa kwa kina na mapana kinachoendelea.
 
Back
Top Bottom