Haijawahi kuonekana Simba mbovu zaidi ya hii ya leo

Its Pancho

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2018
Posts
16,911
Reaction score
28,469
I salute you kinsmen

Hivi mnajua kuwa haijawahi kutokea Simba mbovu kuliko Hii ya leo?

Yaani haina tofauti na mbwinde fc ya kwetu kilimagohe kimbiji.

Nachelea kusema wale Gaborone ni kwamba walikuwa wabovu tu nao licha ya kutandaza mpira mwingi sana kama wao ndio wapo nyumbani na hata kuchomoa goli moja bado performance ya simba ilikuwa chini sana.

Wachezaji walioletwa ni wachovu na kama vile wamelewa.

Sasa simba walienda misri kufanyaje? Kama sio kuogelea na kushikana shikana kama sio kutiana kama kale kajamaa Chao kafupi michezo yake?

Simba wanaenda kuumia vibaya sana mbeleni kwa kweli

Kama Gaborone wamechezesha shele nyumbani vipi mkikutana na esperence na ahly ahly??

Si nchi itapepea bendera nusu mlingoti?

Shtukeni simba mtaendelea kutapeliwa mpaka lini??

Mnaletewa wachezaji wa kuokota bar mpaka lini?

Simba imekuwa dampo la kubeba wachezaji hovyo..

Leo simba imecheza kama wamelewa pombe kali ya kisungura.

Kocha wa viungo ana kazi gani???

Its Pancho
 
Acha uhuni kwani wamefunzu au hawajafunzu?? Yanga siyo bench mark ya simba. Kwamba matokeo atakayo yapata Yanga na simba ayapate hayo hayo. PIRA OBJECTIVE
 
Hivi ni utaratibu gani ulitumika kumchukua Hemed Moroco (ambaye ni kocha wa timu ya Taifa) kuwa kocha wa muda wa simba kwenye mechi iliyopita dhidi ya Gaborone!

Na kama kocha wao Fadlu aliondoka, na Matola kulimwa kadi nyekundu! Je, kwenye benchi lao la ufundi hakukuwepo na kocha mwingine wa kuiongiza timu?

Ni kwa nini viongozi wasingekubaliana kwanza na Fadlu kuongoza timu kwenye mechi ya marudio, ndipo aondoke?

Mbona wenzetu wa Ulaya wako very systematic kwenye mambo yao?

Je, ingetokea kocha wa timu ya Taifa akaenda kuwa kocha wa muda wa Yanga, mashabiki wa simba wangetuacha salama kweli? Si ndiyo wangesema Yanga ni timu ya serikali, na ndiyo maana imepewa mpaka kocha wa timu ya Taifa ili kuwa kocha wao wa muda?
 
Kwanza watumbie walitumia kiasi gani kwenye huu usajili maana inawezekana tunawalaumu bure
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…