Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
HAIKUWA RAHISI SAID KASTICO KUPEWA MTAA...KAMA KAWAIDA
Mtendaji wa Mwenge hakuwa kafurahia sana Mzee Said Kastico kuadhimishwa.
Ugomvi ukatokea hadi ukafika kwa Msaidizi wa Mkuu wa Wilaya.
Ukoo wa Mzee Kastico wala hawakuomba mzee wao apewe mtaa bali wananchi wenyewe katika mkutano walipendekeza Mzee Said Kastico apewe mtaa na wakachagua mtaa unaopita nyumbani kwake.
Wanae wakaombwa wachangie shilingi 320,000.00 na wakatoa fedha hizo.
Kilichofuatia baada ya kulipa hizo fedha ni Mtendaji kukaa kimya kwa wiki tatu na alipofuatwa kuulizwa kulikoni akajibu kuwa fedha zimekawia kulipwa na mtaa huo wa Said Kastico akapewa mtu mwigine jina lake Chilumba.
Baada ya kidonda ukafuatia msumari wa moto Mtendaji akasema kuwaambia watoto wa Said Kastico kuwa wanaweza kwenda kokote.
Msaidizi wa Mkuu wa Wilaya akaomba ushahidi kuwa watoto wa Said Kastico hawakutoa ushirikiano wa kutosha kwa baba yao kuadhimishwa.
Ikaamuliwa Mzee Said Kastico apewe mtaa mwingine si ule wa kwanza pale mtaani kwake alipoishi.
Ikawa kheri nusu shari kuliko shari kamili.
Said Kastico rafiki ya baba yangu akapata mtaa.