Haina haja ya kuleana kwenye maisha – Irene uwoya

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Msanii wa Filamu Bongo, Irene Uwoya amefunguka kuhusu tabia ya baadhi ya wanawake kutopenda mafanikio ya wazao badala yake wapo tayari kushuhudia wenzao wakishindwa.

Muigizaji huyo amesema watu wa aina hiyo hakuna haja ya kuwa nao katika maisha ya kila siku na yeye kila siku anawapunguza katika maisha yake kwani amegundua wanawake wengi hawapendani.

“Hivi kwanini wanawake tunakuwa hatupendani??? yaani najiulizaga sanaaa, badala sisi tushirikiane ndio kwanza tunarudishana nyuma, mtu akifanya kitu kizuri au biashara ndo kwanza kuponda,” ameandika Irene Instagram na kuendelea.

“Ukifanya mabaya ndo anakusifia ili uwendeleee kuharibu, halafu yeye akifanya lake anataka umuunge mkono anasahau yeye hakuwahi kufanya hivyo, sasa hivi nimeamua si support mtu yeyote asiye ni-support, na haina haja ya kuleana kabisa mtu asiye kuwa na umuhimu kwenye maisha yako haina haja ya kuwa sehemu ya maisha yako atakurudisha nyuma tuu,” amesisitiza.

Irene amemaliza kwa kushauri wanawake waachane na marafiki wanaowashauri kuhusu starehe pekee siku zote badala yake wakae na marafiki ambao watawashauri namna ya kuingiza fedha.


Bongo 5
 
SIO WANAWAKE TU HATA WANAUME WENGI WA KITANZANIA HASA VIJANA HAWAPENDI KUONDA MWENZAO ANAFANIKIWA.LAZIMA WAIBUE VIKWAZO.
Cc Ruge Mutahaba
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]naona umem cc kabisa mwanaume asiyependa kuona mafanikio ya wenzake
 
SIO WANAWAKE TU HATA WANAUME WENGI WA KITANZANIA HASA VIJANA HAWAPENDI KUONDA MWENZAO ANAFANIKIWA.LAZIMA WAIBUE VIKWAZO.
Cc Ruge Mutahaba
Kwahiyo Ruge ndio muibua vikwazo?

[HASHTAG]#KataaKuwaKaa[/HASHTAG] [emoji14]
 
Umri ukienda akili inakomaa siku hizi anaongea point muke ya dogo janja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…