Haina majotro maana yake ni nini?

Dio

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2011
Posts
1,274
Reaction score
159
Habari za asubuhi wanajamii wenzangu,
kuna kitu kinanitatiza kwenye tangazo la bia moja wanaslogan inayosema
"HAINA MAJOTRO"
mimi mpaka leo sijajua maana ya hilo neno,na hata nikiwaeleza watu wanaopenda kulitumia hili neno hawanipi jibu la kuniridhisha,ndio maana nikaamua kuleta hapa kwa great thinkers wanisaidie kupata jibu
asanteni.
 
Watoto ndio wanajua,ila jaribu kumuuliza anayesema....... Pindi ukimskia
 
Nenda baa ya hapo jirani halafukunywa kama chupa tano mfulilizo then utapata jibu
 
Sio slogan ya hiyo bia, ni slogan ya tamasha la FIESTA 2011/2012 linalodhamiwa na bia hiyo.
 
mtafute fetty au b12 hao fasta tu watakupa jibu au nenda teentz mkuu..
 
Ni kauli ya kijinga tu.........endelea na shughuli zako
 
Haina Majotro aka Majasho=Haina noma=Hakuna Tatizo,yaani haina shida.
 
Hilo ni neno ambalo limeletwa mtaani ili liweze kupata mashiko, kama mengine mfano,,umefulia, masharabaro,masela etc, lakini pamoja na promo, halina mashiko kwa watu wenye akili zao na limebakiwa kutamkwa na wajinga wajinga tu.

kwa sasa linatumiwa na waandaaji wa fiesta,,baada ya fiesta litasahaulika.
 
Semi na Methali za wazee wetu wa kale zote unazijua ? Achana na maneno yanayoanzishwa na malimbukeni hua yanakuja na kupita kisha kusahaulika kabisaa.
 
Haina Credit..........................................................................................................................
 
Asanteni kwa wote mliochangia kwenye uzi huu,angalau nimepata japo kamwanga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…