Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Ukimya wake tangu maandamano ya Gen Z yalivyoanza uliibua maswali na mashaka mengi juu ya uwezo wake, weledi wake yeye na wa jeshi la polisi kwa ujumla, na kwa yeye kuendelea kuhudumu kwenye nafasi alikua nayo jeshini.
Polisi kuwapiga risasi hadi kufa waandamanaji wa Gen Z, kulitia dosari na wasiwasi zaidi uongozi wake kama IGP. alilaumiwa na kukosolewa sana na makundi mbalimbali ya wakenya, ikiwa ni pamoja na vyama vya siasa na mashirika ya kidini ambayo yalienda mbali zaidi na kumtolea wito wa kujiuzulu na kudai kua ndie alie toa amri kwa polisi kutumia nguvu kubwa kupita kiasi na kutumia silaha za moto na kusababisha uharibifu na mauaji ya waandamanaji wa Gen Z.
IGP ni miongni mwa maafisa waandamizi wa ngazi za juu serikalini upande wa jeshi la polisi aliekua akikosolewa na kunyooshewa kidole zaidi ndani na nje ya jeshi hilo kutatiza maandamano ya amani ya Gen Z, yaliyo geuka kua ya ghasia.
ilikua ni suala la muda tu ashinikizwe kuachia ngazi.
Maswali mengi magumu sana ya kiusalama aliyo ulizwa Rais, Dr. William Ruto na vyombo vya habari yalifaa au yangepaswa kua yameshatolewa maelezo ya kutosha au kujibiwa na IGP, kwa kina sana, na mapema sana kwa vyombo vya habari na umma wa wakenya kujua kinachoendelea kwenye maandamano hayo.
Lakini IGP hakuwahi kufanya hivyo, alikaa kimya, licha ya lawama nyingi kuelekezwa kwake na makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na vijana wa Gen z, taasisi za kidini na za kiraia na kumtaka ajiuzulu kwa kushindwa kuwasimamia waandamanaji kuandamana kwa amani badala yake kusababisha vifo.
Je, kuna haja Gen Zs kuendelea na maandamano? au ni wakati muafaka sasa watulie na kujenga nchi yao iliyoharibika kiasi, maana mahitaji yao yameskizwa na yanafanyiwa kazi na serikali sikivu ya MUUNGANO WA KENYA KWANZA chini ya Dr. WilliamRuto?