Haiwezi kuwa aibu kama watu tupo Mill. 55 walipa kodi wapo Mill 2.2

Mung Chris

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2017
Posts
3,391
Reaction score
3,849
Haiwezi kuwa aibu watu kama tupo Mill. 55 walipa kodi wapo Mill 2.2, na haita kua aibu kwa sababu

1. Wanasiasa wanaingilia maamuzi ya wafanya biashara katika biashara zao

2. Siasa na biashara zinalazimishwa kuingiliana, hata pale ambapo kuna biashara anaweza akalazimishwa mfanya biashara na kumuonyesha ulazima wa siasa kuingizwa, sasa nani anataka siasa

3. Si kila mtu ni mpenzi wa siasa, wafanya biashara wanaweza kulazimishwa waingie kwenye siasa ili mali zao ziwe salama au ndio watapona kitu ambacho wengi hawataki, lazima mfanya biashara achague/ aamue mwenyewe

4. Kusajili kampuni ya biashara na kupata lesseni ya biashara ni gharama kubwa sana sana, ifahamike kodi ndio inatakiwa iangaliwe na izingatiwe kuwa ni kubwa zaidi ya tozo za hapa na pale

5. Inaweza ikatokea mfanya biashara akapata vitisho ili atoe hela hivyo kunfanya asiwe na amani na usalama wa mtaji wake, hapa huwezi tegemea kila mtu alipe kodi, magendo lazima na kodi inaweza isilipwe.
 
Tufanye wote tu wasilipe kodi kabisa, hivi Wafanyakazi nao si wanalipa kodi tena zaidi ya mfanyabiashara?
 
Nakupongeza Mh Rais Magufuli kuleta vitambulisho vya mjasilia mali hakika utakusanya kodi kubwa mno na kila mtu atakuwa na kitambulisho hiki,pongezi nyingi kwako mtukufu Rais wetu wasio jua maana ndo watachangia pumba.Wekeni kumbukumbu tarehe ya leo baada ya mwaka mmoja tafakari hii ya vitambulisho vya mjasilia mali mtapata jibu.
Tufanye wote tu wasilipe kodi kabisa, hivi Wafanyakazi nao si wanalipa kodi tena zaidi ya mfanyabiashara?
 
huyu bwana analalamika mambo ya ajabu mwambieni akemeee chama chake kutumia/kulazimisha wafanya biashara kuichangia ccm kwenye upuuzi wake

hii upelekea ukwepaji wa kodi kwa mgongo wa kufahamiana. maana kuna kesi mtu anakwepa kulipa kodi ccm (kupitia wenyevitu/katibu) wanapitisha vi memo waachwe kwa kuwa ni watu wao.

leo unakuja lalama ujinga wakati ni michezo yenu kuwatumia wafanya biashara kwa manufaa ya chama
 
wewe ndio mbumbumbu kabisa yaani una driving license, una Bank Card/ATM, Una National ID, una Voters registration ID Card, Una kitambulisho cha kazi, Una kadi ya Medical Insurance, Una kadi Mfuko wa Jamii (NSSF na wengine) na sasa una kadi ya Mjasiriamali.....mtu mmoja huyu huyu?? Yaani ndio kikomo cha ububnifu wetu?
 
ID hii ya mjasilia mali najua kwa uelewa wako umeifananisha na ID nyingine ulizotaja hapo juu,ningekuelewesha zaidi ila nishakupima IQ yako inatosha siwwzi poteza muda.kwa kifupi sana nikueleweshe kidogo tu hivyo vitambulisho kwa mwaka 1 tu vinaweza ingiza 1.Tillion,natulipoteza hela nyingi huko nyuma! ni wajasiliamali wangapi wako chini ya 4m kwa nchi yetu? kama si zaidi ya 10 m.Mwisho.

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
 
Yeye anatakaje na inabidi wapungue mpaka wafike laki 1 maana watu lazima wakimbie kuinvest kwa mfumo wa ulipaji kodi uliopo, yaani siyo fair kabisa mauzo madogo, kodi na leseni ya biashara kubwaaaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…