Haja kubwa ya ghafla yadaiwa kusababisha Refa kushindwa kuendelea kuchezesha mechi kati ya Kagera Sugar na JKT Tanzania

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Cheza na Vitu vyote ila siyo Haja Kubwa na ikija huwa haiangalii Wewe ni Baunsa au nani bali ikija yenyewe inachochujua tu ni kutoka nje kwa kupenya kwa njia ya Kasi ya ajabu kabisa na ukisema uibishie basi itakavyokuaibisha unaweza hata ukatamani uwe unatembea tu Usiku kwa Usiku ili ujifiche usionekane.

Katika kile kinachoaminika kuwa Refarii Emanuel Mwandembwa aliyekuwa akichezesha Mechi ya Ligi Kuu Tanzania bara kati ya Kagera Sugar na JKT Tanzania katika dakika ya 83 ya mchezo alishindwa kuendelea Kuchezesha Mchezo huo baada ya Kushikwa na Tumbo la Kuhara la ghafla hali iliyomfanya akae chini Kwanza ili nae apate Huduma ya Kwanza ila Watoa huduma ya Kwanza walipoenda Kumsaidia hakutaka kuwachelewesha wala kuwaharibia Hewa pale halafu baadae waje Kumlaumu kama si Kulaumiana ambapo aliwaomba upesi sana wamkimbize Vyumbani ili awahi Chooni akamalize Shughuli kabisa.

Mara baada ya tukio hilo la Ajabu na jipya kutokea hapa Tanzania habari za ndani kabisa zinasema ya kwamba kilichomkubwa huyu Mwamuzi ( Refarii ) ni Kitendo cha Kishirikina kilichofanywa na moja ya Timu hasa baada ya Kuona Mwamuzi huyo kama vile akiwauma / akiwaelemea Kimaamuzi na Kuipendelea Timu nyingine.

Hata hivyo Mwamuzi aliyechukua nafasi ya ghafla ya Mwamuzi aliyeenda Kujisaidia Haja Kubwa Yeye alichezesha vyema tu bila ngendembwe / hila na alizimaliza zile dakika Saba ( 7 ) zilizobaki na wala hakusikia cha Mkojo unakuja au Kimba linakuja kama ilivyokuwa kwa Mwenzie.

Kweli Uchawi upo Tanzania. Huyu Mganga Kiboko yaani anaroga hadi Mwamuzi ( Refa ) ili apatwe na Tumbo la Kuhara!

Nawasilisha.
 
Hizi ni assumptions mkuu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alikula makande nn
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…