Haji atakuwa wapi?

ZINDAGI

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2015
Posts
1,118
Reaction score
1,430
Nimekaa najiuliza hivi siku ya leo ya mechi ya Simba na Yanga na kwa hali ilivyo kati ya Manara na uongozi wa Simba, muda huu unafikiri atakua wapi?

Mimi ninavyoona atakuwa zake shamba hataki hata kusikia habari ya mechi na maombi yake ni kwamba muajiri wake afungwe
 
Yupo na remote yake home anaangalia mechi na kama Yanga akifungwa Manara atakuwa na hali mbaya kuliko mashabiki wa Yanga,sababu kwa mpira wetu huu wa kibongo waatamini kweli alikuwa ana wasaliti.
Very true
 
Amesema hatokuwepo, insta inaonyesha yupo Kigali Rwanda
 
Daa Haji namuonea huruma sana. Kwa namna alivyokuwa anazungumza ukimsikiliza vizuri ni kama vile alikuwa anataka Simba ifungwe ili ionekane kuwa yeye ndiye ufunguo wa ushindi lakini anasahau kuwa Simba alipigwa kwa Mkapa na yeye akiwepo uwanjani. Matokeo ya leo kwa kweli kabisa yatamvunja nguvu na chochote kibaya atakachozungumza dhidi ya Simba kitakuwa hakina nguvu kabisa.
 
Kuwa na ELIMU ambayo itaweza kukupa uwezo wa kufikiri ni jambo muhimu sana katika maisha yako.

Yule HAJI mbinu aliyetaka kuitumia katika mgogoro wake na UONGOZI wa SIMBA umefeli vibaya sana. Kwani alishajua kibarua kinaenda kuota majani kutokana na mambo aliye kuwa anatuhumiwa sasa kwasababu anaakili za uswahili swahili akaamua kwa makusudi kutengeneza DRAMA ili aweze ku-attrack attention kwa wanasimba na mashabiki kwa ujumla.

Mtu mwenye akili timamu huwezi kumtumia mkubwa wako kazi VOICEMAIL yenye maneno makali kiasi kile sasa sijui alijua ana deal na MWAJUMA ndala ndefu akajua kwa maneno yale lazima yule C.E.O atamjibu kwa VOICE MAIL sasa akakuta hola hamna majibu ndio akaja na excuse yy hakuisambaza ile VOICE CLIP baada ya kuona amesha feli kwenye hilo sasa tusubiri kesho amesema atafunguka kila kitu hakuna wa kumfunga mdomo.
 
Yupo na remote yake home anaangalia mechi na kama Yanga akifungwa Manara atakuwa na hali mbaya kuliko mashabiki wa Yanga,sababu kwa mpira wetu huu wa kibongo waatamini kweli alikuwa ana wasaliti.

Kafungwa tayari
 
Kitendo cha Simba SC si tu Kushinda Mechi ya leo bali na Kuchukua Ubingwa wa ASFC ni psychological blow kwa Haji Manara.

Kitendo cha Haji Manara kuja na Clips au zile Voice Notes zake ni kwamba alishajua ameshashtukiwa na Usaliti wake kwa Simba SC hivyo alikuwa anatafuta Huruma ya Mashabiki huku pia akijua tena akiwa na uhakika kuwa Ramani ya Vita aliyowauzia Yanga SC Siku ya Jumanne alipoenda Kisiri Kigamboni leo ingefanikiwa na Yanga SC ingeifunga tena Simba SC.

Ushindi wa Simba SC umemfanya Haji Manara aonekane kuwa ni kweli alikuwa akiisaliti Simba SC kwa Yanga SC kwa Kuwauzia Ramani ya Vita na sasa hata akisema aitishe Press Conference ya Kuichamba Simba SC na kutaka Kujisafisha kwa Watu itakuwa ni Kazi bure, hatosikilizwa na tena ndiyo atazidi Kudharaulika na Kuchukiwa na Mashabiki wa Simba SC.

Kitendo cha CEO wa Simba SC Barbara Gonzalez Kunyamaza na kutotaka kabisa Kumjibu Haji Manara ni Pigo Takatifu kwa Kwake Haji kwani dhumuni Kuu la Haji ni kuona CEO akiingia katika Mtego wako wa Uswahili alionao Haji Manara na kutaka Malumbano na Majibizano nae ila CEO Barbara kaonyesha how Smart She is in Corporate World huku Haji Manara sasa akionekana si tu ni Mwendawazimu bali ni Mpumbavu tu kabisa.

Kitu pekee ambacho kwa sasa Haji Manara anaweza Kufanya ni Kuwaomba Radhi wana Simba SC wote, CEO Barbara Gonzalez na Mwandishi wa Habari Prisca Kishamba kisha aachane na Simba SC Kiutendaji na abakie tu kuwa Mwanachama na Mpenzi wa Kawaida kama wengine ila akae akijua tu kuwa ameshadharaulika karibia na 85% ya wana Simba SC wanaojitambua ila 15% ya Wanafiki wenzake bado watampenda na hata Kumuamini.
 
Well said
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…