Haji Manara ambwatukia "Shaffih Dauda"

Mwambieni manara basi akapige hizo penart
 
Hivi Dick Dauda na Baraka Mbolembole ndiyo Shafii Dauda?
Makala imeandikwa na Dick lakini shutuma kwa Shafii.
Huyu mtu ana ulemavu wa akili!
Mkuu hizo ni kauli za Shaffih Dauda jana kwenye kituo cha Radio cha Clouds FM,so kuniita nina ulemavu wa akili sii sawa na unapaswa kufuta kauli.
Muandishi wa makala amekopy na kupest.
 
Mkuu hizo ni kauli za Shaffih Dauda jana kwenye kituo cha Radio cha Clouds FM,so kuniita nina ulemavu wa akili sii sawa na unapaswa kufuta kauli.
Muandishi wa makala amekopy na kupest.
Nazungumzia Haji sio wewe. Angalia majibu yake. Ilikuwa majibu kwa Dick Dauda
 
Shafii kakaa kishabiki (Yanga & Man U) , Jeuri pia mbishi... inahitaji moyo kuelewa uchambuzi wa huyu jamaa.. Urais TFF hakukosea kuwa dumped.
Ujeuri, ubishi, ushabiki ....... hizo ni sifa mbaya kwa mwanahabari wa michezo. Aliye nazo hapaswi kuendekezwa wala kusikilizwa, hata kama ni Haji Manara.
 
Shafii kakaa kishabiki (Yanga & Man U) , Jeuri pia mbishi... inahitaji moyo kuelewa uchambuzi wa huyu jamaa.. Urais TFF hakukosea kuwa dumped.
Shafi ni ni simba tangu kitambo tena hao simba walikuwa wanamtumi hadi kutafuta wachezaji pia aliwahi gombea uonğozi simba
 
Shafi ni ni simba tangu kitambo tena hao simba walikuwa wanamtumi hadi kutafuta wachezaji pia aliwahi gombea uonğozi simba
Na alifanya majaribio ya kucheza mpira Simba 2003 baadaye akaamua kusoma over kucheza soka.
 
huyu Khadija Manara mtafutieni demu wa kuzodoana naye.

mwenziye Jenny Muro tayari keshampata yule mdada wa ACT!
 

Punguza maneno mengi ,kiasi mengine unayasahau

Ni ww uliyetuhabarisha kuwa usajili wa wachezaji wa Simba ni sawasawa na wachezaji wote waliosajiliwa kwenye vilabu vya ligi juu.

Ni we uliyetumia lugha ya msisitizo kuwa VALUE ya Hatuna Niyonzima ni sawa na wachezaji wote waliosajiliwa na Dar Yanga Afrika.

Sasa nashanga ww tena unaibuka na kuwashambulia waandishi kuwa hawafuatilii thamani za wachezaji wa Yanga wanakalia usajili wa Simba.

Ni muhimu kupunguza maneno na kuweka kumbukumbu sasa iweje utamke tena Chirwa kasajiliwa kwa ada ya dola 100,000 na unathibitisha kuwa Simba haijawahi kusajili kwa gharama hiyo.

Bado unauliza mnajua Ngoma na Kamussoko wmesajiliwa kwa gharama kiasi gani? Au mnakalia kuifuatafuata Simba.

Sisi tuko OPEN usajili wetu tumeweka wazi hatufichifichi sasa KUMBUKA ni mchambuzi ww uliyechambua na kujiridhisha Simba ndo timu iliyosajili kwa gharama kubwa.

Wanachofanya waandishi ni kusherehesha kile ulichokiandika.

Lawama kwa marefa waliosababisha Simba kupata sare mechi ambazo Haji anaamini wangeshinda.

Ingekuwa vzr pia amsifie mwamuzi wa mechi ya Simba na Mtibwa kwa kuchezesha kwa haki mpaka Simba ikasawazisha.

Marefa wetu waliotupiwa lawama hebu tujiulize kwann sasa na isiwe wakati ule ule jibu ni jepesi.

Kufuatilia maneno ya vijiweni, Kamussoko,Tambwe,Ngoma baada ya maneno hata ya mashabiki mtaani wakiwa na Tambo zao.

Na uhalisia wa mechi ilivyokuwa ukiiongeza na ushabiki pamoja na marekebisho ya baada ya dk 90.


Ndo utaona mashabiki Wa Yanga wakijisifu na kuwachezesha kimawazo NGOMA,TAMBWE,KAMUSSOKO huku nako msemaji wa Simba kujibu mapigo.

Naye anatafuta kupitia runinga marejeo ya mechi kukosoa na kurekebisha makosa yenye faida kwa timu yake pekee.

Kwa msaada Haji hakuna kiongozi wa Yanga uliyejibishana naye kwa njia ya kuita waandishi umejibishana na MASHABIKI.

Kosoa ulimi wako,kosoa timu yako ndipo urukie kada zingine.
 

Well said
 

Sina hakika Kama Manara alikwishazaliwa wakati wahenga wa Dar walipoasa kwa njia ya usanii, 'mtoto wacha kupiga mayowe, wache watu waone wenyewe'. Aya yake ya ufunguzi sambamba na majilabu yanayofuata (ambayo kwa bahati mbaya yamekosa takwimu) inapingana na onyo hilo kutoka jiji analojinasibu ndio kijijini kwao.

Kama mwandishi, Haji alipaswa kufuata wosia wa gwiji la uanahabari duniani aitwaye Joseph Pulitzer anayetaka makala ziwe 'fupi ili wasomaji wazisome, fasaha ili wazikubali, za kisanaa (silo kisanii - picturesquely) ili wazikumbuke na sahihi ili waongozwe na mwanga wake' Sina hakika kama amefanya hivyo.

Kama muungwana, Haji alipaswa kutembea kwenye maneno yake kwamba, miongoni mwa mengineyo, yupo 'kupigania maslahi ya Simba.' Uhalisia sidhani kama anapigania maslahi ya Simba kwa kauli zake zinazochochea chuki/woga wa waamuzi dhidi ya timu, zinazowafanya wanachama wanaojitambua kuichukia timu yao kwa kauli zake za kushadidia uongo/uzushi na upuuzi wa viongozi wenzake kama wa kukata rufaa FIFA na/au kugomea medali za ushindi wa pili wa Ligi, zinazowatia shinikizo wachezaji kwa kuwapandisha kiwango wasicho nacho kupitia maneno yake na zinazowafanya wadau wadharau hata atapotoa madai ya kweli kwa kuwa tayari wameshazowea malalamiko yake ya kila siku.

Kama mwandishi, Manara alipaswa kutumia mtandao wa kijamii kuwasiliana na wadau wa timu yake na siyo kwa malumbano binafsi na anayemwona kuwa ni mbaya wake na wa timu yake. Kama ni kujibu mapigo, alipaswa ama kujibu kwa namna ileile aliyoitumia huyo gwiji kwa kuelekeza hoja zake kwa wasomaji. Au angewasiliana naye kupitia anwani binafsi, iwe mtandaoni au kwa barua ya kawaida.

Kama msemaji wa klabu, huenda amewakosea sana wadau wa mpira na wa Simba kwa kukalia habari muhimu za mapato makubwa ya Simba kwa misimu minne mfululizo, mpaka 'anapochokonolewa' na huyo anayemjibu shakhsia (personally).

Na huenda kama mtoto, Manara hawatendei ndivyo wazee wake anaojisasibu kwamba wamemrithisha umaarufu kwa makubwa waliyoyafanya kimpira, kwa tibia fake endelevu ya kuinanga isivyo kiungwana klabu iliyowafanya wayafanye hayo makubwa.

Na kama mwanadamu, huenda amekosea kutumia falsafa ya jino kwa jino. Kama anaamini alikosewa na huyo gwiji anayemsema, dawa kubwa ingekuwa kukaa kimya, maana moto hauzimwi kwa moto. Au angetafuta naye faragha wakajadiliana jinsi ya kuzika tofauti zoo, hasa ilivyokuwa - kama anavyosema - wote ni Wanasimba. Namsihi afanye hivyo badala ya kutekeleza nia yake ya kuwaeleza Wanasimba kisa cha huyo gwiji kuichukia Simba. Si vyema kuosha hadharani nguo za ndani za Simba, wala kumwaga mtama kwenye kuku wengi. Ifike siku sote tuitikie mwa pamoja mwito wa 'Gwiji Oyee! Manara Oyee! Simba Oyee!'
 
Though me sio mshabiki wa simba ila jamaa huwa namuelewa sana. Ana logic zake flaani hivi za kisomi mno.
Kama kwel unaona logic za manara nizakisomi sishangai taifa hili hususan kwenye ulimwengu Wa soka kuwa bado tunaitwa kichwa cha mwenda wazimu kila MTU anajifunzia kwetu kunyoa cjui logic gani unazozielewa toka kwa huyu MTU tofauti na kupiga kelele kwenye media kila siku na kuwabebea watu li tv likubwa
 
hivi kuna siku shafii ashagawai isifia simba kwel
 
'YOU CANNOT TEACH OLD DOG NEW TRICKS'
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…