Haji Manara atokwa na povu baada ya kulipuliwa na Abdi Banda

Haji Manara atokwa na povu baada ya kulipuliwa na Abdi Banda

py thon

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2016
Posts
2,476
Reaction score
4,448
Kama ilikupita hii.....Povu la Manara kwa Abdi Banda mchezaji wa zamani wa simba anayechezea Baroka fc ya south Africa

" Kumjibu mtu mjinga ni kufanana nae..ila kumwelimisha mjinga ni kumsaidia

Nimeona hyo video ya Salehe Ally na mchezaji wa Baroka fc (Kama nimeiandika vema )ya nchini Afrika kusini Abdi Bhanda

Bhanda alipata kuichezea klabu ya Simba kabla ya kujisajili na timu yake mpya
Kwenye video hyo Bhanda anaulizwa swali na mwandishi ni kitu gani hutatamani kikutokee ktk career yako ya kucheza Soka.. akajibu.jambo nisilotaka kuja kuntokea ni kwa viongozi waliopewa dhamana kuchukua mamlaka ya kwenda kuongea na vyombo vya habari huku wao hawana mamlaka hayo..huku akikiri kuwa kuna watu wameajiriwa kwa kupewa hyo mamlaka.

Halafu akaendelea kwa kuponda kwa mfano wangu eti kulalamikia maamuzi ya refarii aliochezesha mchezo wetu wa Ligi kuu baina yetu na Yanga..mchezo ulioisha kwa sare ya bila kufungana..
Mchezaji huyo alienda mbali zaidi kwa kusema jambo hilo linasababisha mpira wetu usiende mbele..

Nimjuze kwanza wajibu wa kazi yangu..mm ndio msemaji rasmi wa klabu ya Simba na nimepewa hyo mamlaka kama alivyosema yy mwenyew ktk interview yake..nikiongea mm naongea kwa niaba ya kamati ya kamati ya utendaji wa Simba..siongei jambo ila uongozi umeridhia na ndio maana kwa kipindi chote ambacho nipo Simba haijatokea hata kwa bahati mbaya mm kupishana kauli na viongozi wenzangu..
Hvyo dogo aelewe ile ni mamlaka yangu.

Pili mm kwenda kulalamikia maamuzi yale ni stand ya klabu na sikukurupuka kama alivyokurupuka yy ambae hata hajui nani msemaji rasmi wa klabu ya Simba..nimwambie kuanguka kwa mpira kuna sababu nyingi nchini na sio kulalamikia waamuzi pekee..hata huko South unapoomba Mungu watu hulalamikia waamuzi na walalamikaji ni viongozi,mashabiki,makocha na hata wachezaji.

Pia asisahau kulalamika kwangu ndio kulimsaidia asifungiwe adhabu kubwa na TFF baada ya kumpiga George kavila wa Kagera Sugar,hali iliopelekea kupata fursa ya kucheza Cosafa cup ambapo akaonekana na kusajiliwa huko South..

Nimkumbushe pia kulalamika kwangu ndio kulikopelekea utetezi ktk shauri lake kwa uongozi wa Simba ambapo alikuwa afukuzwe timu kitambo kwa kukosa nidhamu na maadili ya kambi..tena nilifanya utetezi mbele ya Bi mkubwa wake na bwana Bosnia ambae ni kama mlezi wake
Na hapo sitaki kumkumbusha huo ulalamishi wangu ulivyomnusuru yy ktk lile shauri lake la jinai..

Nimalizie kwa kumwambia weka akiba dogo..bado hujafika kokote wala usijione ushakuwa Abedi Pele au Lucas Radebe..huwa nazisikia tambo zako mbalimbali ukihojiwa na media za Tanzania..wakati mwingine ukibeza hata ulipotoka!!

Sijui ungekuwa ww ndio Samata ingekuwaje?
Sijawahi kumsikia Samata kwa njia yoyote akiponda hadharani viongozi wa bongo wala Simon Msuva au Ulimwengu..ila ww uliohamishia mpira mdomoni..jifunze kwa waliokutangulia na ujiwekee malengo yako ili ww,familia yako na Taifa kwa ujumla wafaidike,kupambana na mtu mwenye taaluma ya kuongea na kuandika ni kututafuta muhali tukaja kuongea yasioandikika...."

Haji S Manara
FB_IMG_1522335088170.jpg
FB_IMG_1522335066736.jpg
 
jamani tuwe waelewa kuhusu Haji Manara.

psychologically, ni jambo la kawaida kwa maumbile ya kibinadamu kwa mtu mwenye physiological deficiency ku compensate mapungufu ya hali alinayo nayo. it comes involuntarily.

anaweza ku compensate hali hiyo kwa kuwa mgomvi sana, mlevi sana, mtukanaji sana, msema ovyo, nk.

so...niwaase wapenzi wa michezo always tuwe tuna sympathize na Haji Manara badala ya kumwona ana matatizo.
 
Hili jamaa ni lijinga sana, ina maana kama banda alisaidiwa na kupitia mikononi kwa simba sport club hana haki ya kuongea au kutoa maoni???

Halafu naona amezunguka sana na hoja butu zisizo na mashiko. Abdi banda amempa za uso kuwa yeye ni moja ya vikwazo vya maendeleo ya mpira wa tanzania , badala ya kujibu hilo jiiwe alilorushiwa matokeo yake ameishia kutapatapa kwa kuwataja wakina samata na msuva.

To be honest haji manara and the likes ni miongoni mwa wadau wanaoshusha soka la bongo. Samuel etoo aliwahi kuwaponda shirikisho la soka la Cameroon kuwa ni kikwazo cha maendeleo kwa soka la cameroon.
 
Kandanda na vtuko vyake ndan ya
Bongo fleva
 
We haji yanga tu..
Banda yuko sahihi na itabaki hivyo.....we mswahili Fulani hivi....mwenzio alikuwa jerry...kuwa pro kama huyu Wa yanga ingawa timu siiipendi
 
jamani tuwe waelewa kuhusu Haji Manara.

psychologically, ni jambo la kawaida kwa maumbile ya kibinadamu kwa mtu mwenye physical deficiency ku compensate mapungufu ya hali alinayo nayo. it comes involuntarily.

anaweza ku compensate hali hiyo kwa kuwa mgomvi sana, mlevi sana, mtukanaji sana, msema ovyo, nk.

so...niwaase wapenzi wa michezo always tuwe tuna sympathize na Haji Manara badala ya kumwona ana matatizo.
Umesharibu. jikite kwenye mada banaa!. Ya nini kumattack personality yake?
 
Hili jamaa ni lijinga sana, ina maana kama banda alisaidiwa na kupitia mikononi kwa simba sport club hana haki ya kuongea au kutoa maoni???

Halafu naona amezunguka sana na hoja butu zisizo na mashiko. Abdi banda amempa za uso kuwa yeye ni moja ya vikwazo vya maendeleo ya mpira wa tanzania , badala ya kujibu hilo jiiwe alilorushiwa matokeo yake ameishia kutapatapa kwa kuwataja wakina samata na msuva.

To be honest haji manara and the likes ni miongoni mwa wadau wanaoshusha soka la bongo. Samuel etoo aliwahi kuwaponda shirikisho la soka la Cameroon kuwa ni kikwazo cha maendeleo kwa soka la cameroon.
Hoja ya banda kuwa anaongea ni Nazi take Kama msemaji Wa club hujainisha anashusha mpiira kivipi,na mfano uliotoa Wa samweli etoo unadhani matatizo yake yanafanana na banda,kutoa maoni ni haki ya banda na pia kujibu maoni ni haki manara
 
Unajua kazi ya msemaji Wa club?
Mkuu unaonaje utufafanulie?
Halafu niulize habari za malalamiko ya refa na mechi ilichezeshwaje naonaga ulaya anaezungumzia ni kocha au kapteni.
Msemaji nahisi ni kutoa taarifa rasmi au kusaidia kwenye branding.
 
Unadhani mifumo inafanana ya uendeshaji Wa club,?
 
Hili jamaa ni lijinga sana, ina maana kama banda alisaidiwa na kupitia mikononi kwa simba sport club hana haki ya kuongea au kutoa maoni???

Halafu naona amezunguka sana na hoja butu zisizo na mashiko. Abdi banda amempa za uso kuwa yeye ni moja ya vikwazo vya maendeleo ya mpira wa tanzania , badala ya kujibu hilo jiiwe alilorushiwa matokeo yake ameishia kutapatapa kwa kuwataja wakina samata na msuva.

To be honest haji manara and the likes ni miongoni mwa wadau wanaoshusha soka la bongo. Samuel etoo aliwahi kuwaponda shirikisho la soka la Cameroon kuwa ni kikwazo cha maendeleo kwa soka la cameroon.
Anashusha soka kivipi??kwani kipindi haji manara hayupo soka lilikuwa juu or lilikuwa linapanda???
 
Simba ni institution, Manara anawakilisha institution, Banda ni kama kuli unamlipa kama hataki kwendraaaaa
 
jamani tuwe waelewa kuhusu Haji Manara.

psychologically, ni jambo la kawaida kwa maumbile ya kibinadamu kwa mtu mwenye physical deficiency ku compensate mapungufu ya hali alinayo nayo. it comes involuntarily.

anaweza ku compensate hali hiyo kwa kuwa mgomvi sana, mlevi sana, mtukanaji sana, msema ovyo, nk.

so...niwaase wapenzi wa michezo always tuwe tuna sympathize na Haji Manara badala ya kumwona ana matatizo.
Sikubaliani na hoja yako. Kuingia kwy swala la uumbwaji ambao mhusika hana mamlaka nao ni aina ya ubaguzi.

Mimi huwa namuelewa na sisi wana Simba tunamkubali sana tu.

Mshambulie kwa hoja zake na si vinginevyo. Mbona alichoongea ni cha kawaida sana na yeyote anaweza kuongea. Hayo ya kwako umeyatolea wapi ktk maongezi yake??

Sipendi kabisa vijidalili vya ubaguzi wa uumbwaji...eti kisa sijui umesomea vitakataka vyako...mhx!

Manara ana haki ya kuchukuliwa mitazamo yake sawasawa na wengine.

Kama unajua sana basi kamwambie na yule kuwa ufupi wake ndio unamfanya "haambiliki" kama hujanyea debe.
 
Back
Top Bottom