Haji manara azimia kabla ya mechi kumalizika

tatum

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2018
Posts
5,786
Reaction score
4,491
Taarifa za ndani kutoka uwanja wa Taifa ni kwamba Msemaji wa Simba Haji Manara alizimia kabla ya mechi kumalizika baada ya vijana wa UD Songo kupata goli la kuongoza.

Baada ya kupata huduma ya kwanza alipata nafuu lakini akiwa katika majinzi na msongo mkubwa wa mawazo.

Kiukweli Simba haikustahili kabisa kutolewa katika hatua hi ya awali hasa baada ya uwekezaji mkubwa na usajili uliofanyika na rekodi ya kufika robo fainali msimo uliopita.

Hongera kwa Yanga na Azam kwa kusonga mbele round ya pili.Kila la heri kwa mechi za kwanza na pili ili kuingia katika makundi.
 
Hakuna hata picha au video
 
Picha kidogo ingependeza zaidi.
 
huyo nae hana lolote...anafanya drama za makusudi za kuwandaa kisaikolojia wafuasi wake wanao mfollow kule instagram maana siku si nyingi kibarua chake cha usemaji wa club kinaenda kuota nyasi.

nimeona tayari emepost eti atawajibika kwa simba kufungwa. [emoji16][emoji16]
 
Amini usiamini jioni hii kuna dada mjamzito hapa banda umiza alipata uchungu ghafla kisa kufungwa kwa Simba na Mungu si Athuman kajifungua salama mtoto wa kiume kapewa jina "Songo"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…