Taarifa za ndani kutoka uwanja wa Taifa ni kwamba Msemaji wa Simba Haji Manara alizimia kabla ya mechi kumalizika baada ya vijana wa UD Songo kupata goli la kuongoza.
Baada ya kupata huduma ya kwanza alipata nafuu lakini akiwa katika majinzi na msongo mkubwa wa mawazo.
Kiukweli Simba haikustahili kabisa kutolewa katika hatua hi ya awali hasa baada ya uwekezaji mkubwa na usajili uliofanyika na rekodi ya kufika robo fainali msimo uliopita.
Hongera kwa Yanga na Azam kwa kusonga mbele round ya pili.Kila la heri kwa mechi za kwanza na pili ili kuingia katika makundi.